Uhuru wetu kama ni umri wa mwanadamu unakwenda kuumaliza mwendo

Vumilika

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
1,558
1,873
Amani iwe nanyi,

Tumeshatimiza miaka 62 toka tupate uhuru wa nchi yetu pendwa ya Tanganyika na baada ya kuungana na ndugu zetu wa Zanzibar tukajiita Tanzania.

Katika safari yetu ndefu hii kama angekuwa mwanadamu basi tunasema anakwenda kuumaliza mwendo, lakini tunashukuru nchi yetu bado inastawi lakini kwa kujikongoja na kwa baadhi ya sehemu tu!

Kwani kuna sehemu nyingine hadi hii leo huduma ya maji ya salama tu haipatikani na ajabu yenyewe ni kuwa wanaishi karibu kabisa na vyanzo vya maji! Kuna mataifa ambayo tulipata nao uhuru au wao walichelewa, kwa sasa wapo mbali kimaendeleo kuliko sisi.

Tanzania ni nchi iliyojaaliwa kila neema ambayo mwanadamu anaweza kuneemeshwa nayo, lakini bado wananchi waliyo wengi hali zao za kiuchumi ni mbaya. Tatizo huenda tunalijua lakini tunalificha au tunaoneana aibu kuambizana ukweli, hali hii itaendelea mpaka lini?

Ifike wakati tupige mstari kuwa hapa ndiyo mwisho wa haya, ili tuanze mwanzo mpya wenye mwanga wa matumaini ambayo kwa wengi yamekufa kuona siku moja mtanzania ataishi nchini kwake akiwa yupo salama salmini na kiuchumi yupo sawa.

Kwani Idadi yetu ni milioni 64, kama inavyokadiriwa kutokana na sensa, tunaweza kugawana vizuri tu keki ya taifa ikiwa mipango mizuri ikiwekwa.

Kwani tuna madini mbalimbali, lakini hatufaidiki nayo, tuna ardhi yenye rutuba lakini hutaifidiki nayo, tuna vyanzo vingi na vikuu vya maji lakini hatufaidiki navyo, tuna bahari lakini hatufaidiki nayo, tuna mbuga za wanyama lakini hatufaidiki nazo, tuna nguvu kazi ya kutosha lakini hatufaidiki nayo.

Tuna taasisi za elimu lakini hatunufaiki nazo mpaka tuna mvua za kutosha lakini hatunufaiki nazo na badala yake zinaleta maafa kwa kushindwa kutengeneza miundo mbinu ya kupitisha maji ya mvua na kuyahifadhi kwa matumizi mengineyo.

Sisi tunajiita wabongo kwa kuwa tunatumia ubongo, hivi kweli si tungekuwa tuna wanataaluma wa kuwafundisha ulimwengu kunako maendeleo?
 
Lakini kuna wengi wazuri pia ndani ya CCM wanaoweza kutuvusha kuelekea nchi ya ahadi.
Nimini mimi! Ndani ya CCM hakuna wa kutuvusha kuelekea nchi ya ahadi. Yaani ni kama tu ilivyo kwa upande wa vya upinzani.
Wa kututoa Watanzania kutupeleka nchi ya ahadi, hatakiwi kutoka chama chochote kile cha siasa.

Badala yake anatakiwa kuwa Mtanzania tu Mzalendo kwa nchi yake. Mtu ambaye atayaweka maslahi ya nchi mbele, badala ya maslahi yake binafsi au yale ya chama chake.
 
Nimini mimi! Ndani ya CCM hakuna wa kutuvusha kuelekea nchi ya ahadi. Yaani ni kama tu ilivyo kwa upande wa vya upinzani.
Wa kututoa Watanzania kutupeleka nchi ya ahadi, hatakiwi kutoka chama chochote kile cha siasa.

Badala yake anatakiwa kuwa Mtanzania tu Mzalendo kwa nchi yake. Mtu ambaye atayaweka maslahi ya nchi mbele, badala ya maslahi yake binafsi au yale ya chama chake.
Ninakuamini kwa kuwa haya ni maoni yako ambayo utakuwa una hoja nayo, hata hivyo tukimtegemea mtu mmoja kufanya haya itakuwa haina faida, kwani binadamu ana uhai na umauti, ana afya na maradhi, ni bora kuwa na mpango kabambe wa kutengeneza taasisi madhubuti ambayo itatupeleka kwenye nchi ya ahadi. Na si vibaya tukiwa na sheria ya mgombea binafsi ili kuwapa nafasi wasiyokuwa na vyama na wanauwezo na ushawishi wa kuendeleza maendeleo ya nchi na wananchi.
 
Back
Top Bottom