Uhuru wa Zanzibar 10 Desemba 1963

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
18,290
25,900
UHURU WA ZANZIBAR TAREHE 10 DECEMBER 1963

Naikumbuka siku hii kama jana vile.

Nilikuwa na umri wa miaka 11 na vitu viwili vitatu ndivyo vilivyonasa kwenye kichwa changu.

Kwanza ni kumuona Mzee Abdulrahman akitoka nyumbani kwake kashika sanduku anaingia kwenye taxi anawaaga majirani kuwa anakwenda uwanja wa ndege safari Zanzibar kwenye sherehe za uhuru.

Mimi na mwanae somo yangu Mohamed Kitunguu tuko barazani kwake na rafiki zetu wengine tunacheza.

Ilikuwa mchana Mtaa wa Gogo moja ya mitaa mifupi sana Kariakoo.

Kitu cha pili kinachonikumbusha siku hii ni nyimbo ya Sal Davis, "Ayayaa Uhuru," ambayo kutwa nzima ilikuwa ikipigwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) ikihanikiza sherehe za uhuru wa Zanzibar na Kenya.

Kwetu sisi watoto tunanyanyukia kuingia "teens,"muziki wa Sal Davis ulikuwa ukitutia wazimu.

Tunamsikia Sal Davis akiimba na radio katika kila nyumba mitaa ya Dar es Salaam zimefunguliwa, "full blast," "Ayaayaa uhuru, ayaayaa Kenyatta, Nyerere, Obote, Shamte..."

Sikumbuki vyema maneno ya nyimbo hii mpangilio wake lakini majina ya viongozi wa Afrika Mashariki yanatajwa na kwa Zanzibar jina la Waziri Mkuu Mohamed Shamte linasikika.

Sauti ya Unguja nayo ilikuwa imefungulia vinanda vya taarab ilmuradi mji ulikuwa furahani.

Katika umri wangu ule mdogo wa miaka 11 sikuweza kutambua kuwa ukubwani Sal Davis atajakuwa rafiki yangu mpenzi na nitakuwa jirani yake milango ya "appartments"zetu zikiangaliana mimi nikiwa mpangaji wake na wake zetu watakuwa mashoga.

Si haya tu nitamkalisha Sal Davis kitako na tutaandika mswada wa maisha yake na mengi tutafanya pamoja nyumbani kwake kwengine Zanzibar na Mombasa Nyali Beach.

Turudi kwenye uhuru wa Zanzibar na nyimbo ya Ayaayaa Uhuru na Waziri
Mkuu wa kwanza wa Zanzibar Mohamed Shamte.

Sal Davis amenieleza kuwa wakati nyimbo yake hii iko juu kabisa kwa kupendwa kote Afrika ya Mashariki, mapinduzi yakatokea Zanzibar na serikali ya Mohamed Shamte ikapinduliwa.

Nyimbo yake kwa kuwa ilikuwa imemtaja Waziri Mkuu wa Zanzibar Mohamed Shamte ikapigwa marufuku Tanganyika na Zanzibar.

Kipindi hiki mauaji makubwa yalikuwa yamepita Zanzibar na baadhi ya viongozi wa iliyokuwa serikali ya Zanzibar wakawa vifungoni.

Baadhi ya viongozi hawa waliofungwa na kutumikia vifungo vyao katika jela za Tanzania Bara nilikuja kufahamiananao kwa karibu sana ukubwani kwangu na nilijifunza mengi kutoka kwao.

Ilikuwa katika Mtaa huu wa Gogo unapokutana na Mtaa wa Mchikichi kwenye baraza ya nyumba ya akina Abdul Kigunya kulipokuwa na barza maarufu ya kucheza bao ndipo kwa mara ya kwanza nilipomuona Abdallah Kassim Hanga.

Hii ilikuwa mwaka wa 1964 na muungano wa Tanganyika na Zanzibar tayari.

Hanga akija hapo kila jioni tena akitembea kwa miguu akija kucheza bao.

Sifa zake kama mmoja wa viongozi wa mapinduzi zilikuwa zimeenea na picha zake katika gazeti la Ngurumo na Mwafrika zilikuwa hazipungui.

Nasi kwa ule udadisi wa kitoto tukimuona pale tutajisogeza kwenda kumshangalia hadi tujazane na wakubwa watuone kero watufukuze.

Haikunipitikia kamwe kama siku itafika nitatafiti historia ya mzalendo huyu pamoja na historia ya "pop star,"mkubwa kupata kutokea Afrika ya Mashariki Sal Davis na nitaandika historia zao.

Inasikitisha tu kuwa katika uhuru wa Zanzibar na mapinduzi yaliyofuatia Hanga aliuawa kikatili na katika utafiti nilikujakujua mengi yaliyopitika.

Si yeye tu.

Marafiki wawili wa baba yangu Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala na wao hawakusalimika.

Nimeishi katika historia hii na ndani yake nimejifunza mengi.

Picha Meneja wa Philips waliorekodi "Ayaayaa Uhuru," akimpokea Sal Davis Uwanja wa Ndege Nairobi mwaka wa 1963 akitokea Ulaya alipokuja kwenye sherehe za uhuru wa Kenya kwa mwaliko wa serikali. Hapa anampigia nyimbo hiyo hapo uwanjani.

Sal Davis na Mwandishi sasa mtu mzima si yule mtoto wa miaka 11 Tanga 2009.

Screenshot_20211210-074713_Facebook.jpg
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
8,799
28,928
Kwa maana kuwa Zanzibar ilipata uhuru wake 1963 kutoka kwa muingereza kama Tanganyika ilivyopata uhuru wake kutoka kwa mwingereza 1961. Hii ni historia muhimu inayopaswa kufundishwa na kuelezwa fasaha kwenye jamii zetu, hivyo tarehe hiyo inapaswa kuenziwa na kusheherekewa kitaifa.

Kwa miaka mingi serikali ya Tanzania imekuwa ikipotosha kwa kuogopa kusema wazi kuwa sherehe za uhuru za tarehe 9 Disemba ni sherehe za uhuru wa Tanganyika, badala yake inasema ni sherehe za uhuru wa Tanzania au Tanzania bara!

Vivyo hivyo kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuogopa kutamka na kusherekea kumbukumbu ya uhuru wa Zanzibar (10/Disemba/1963) na badala yake msisitizo uko kwenye sherehe za mapinduzi. Toka lini mapinduzi yakawa mbadala ya uhuru?

Historia iliyopotoshwa ni hatari kwa mwelekeo wetu wa kifikra wa leo, kesho na keshokutwa.
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,859
4,366
Sheikh Mohammed huyu Sal Davis zamani tukimsikia tulidhania ni mzungu, tulikuja kugundua baadae kumbe ni jamaa wa Zanzibar.

Ukiandika kitabu tafadhali utujulishe na sisi tupate kukuunga mkono tununue.
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
18,290
25,900
Sheikh Mohammed huyu Sal Davis zamani tukimsikia tulidhania ni mzungu, tulikuja kugundua baadae kumbe ni jamaa wa Zanzibar.

Ukiandika kitabu tafadhali utujulishe na sisi tupate kukuunga mkono tununue.
Biti...
Huyo ni Shariff Salim Abdallah kwao Makadara Mombasa.

Nina mswada wa kitabu chs maisha yake.
Sal Davis ni rafiko yangu sana.
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
18,290
25,900
Sheikh Mohammed huyu Sal Davis zamani tukimsikia tulidhania ni mzungu, tulikuja kugundua baadae kumbe ni jamaa wa Zanzibar.

Ukiandika kitabu tafadhali utujulishe na sisi tupate kukuunga mkono tununue.
Biti...
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,087
5,328
Kwa maana kuwa Zanzibar ilipata uhuru wake 1963 kutoka kwa muingereza kama Tanganyika ilivyopata uhuru wake kutoka kwa mwingereza 1961. Hii ni historia muhimu inayopaswa kufundishwa na kuelezwa fasaha kwenye jamii zetu, hivyo tarehe hiyo inapaswa kuenziwa na kusheherekewa kitaifa.

Kwa miaka mingi serikali ya Tanzania imekuwa ikipotosha kwa kuogopa kusema wazi kuwa sherehe za uhuru za tarehe 9 Disemba ni sherehe za uhuru wa Tanganyika, badala yake inasema ni sherehe za uhuru wa Tanzania au Tanzania bara!

Vivyo hivyo kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuogopa kutamka na kusherekea kumbukumbu ya uhuru wa Zanzibar (10/Disemba/1963) na badala yake msisitizo uko kwenye sherehe za mapinduzi. Toka lini mapinduzi yakawa mbadala ya uhuru?

Historia iliyopotoshwa ni hatari kwa mwelekeo wetu wa kifikra wa leo, kesho na keshokutwa.
Tarehe 10 dec 1963 waingereza walikabidhi zanzibar kwa usultan wa walowezi wa kiarabu kama walivyokuja kufanya kumkabidhi ian smith rhodesia. Sultan akiongoza zanzibar miaka yote chini ya ulinzi wa waingereza. Kwa hivyo zanzibar ilikua inarudishwa tu kuendelea na ukoloni wa kisultani uliyofika zanzibar na kuendesha biashara ya watumwa tangu karne kadhaa zilizopita.
Ndio maana ili kua huru waafrika waliyo wengi wakafanya mapinduzi april 26, 1964.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
7,082
5,424

Mpaka lini utaendelea kuwa mjinga?
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
7,548
8,399
Kwa maana kuwa Zanzibar ilipata uhuru wake 1963 kutoka kwa muingereza kama Tanganyika ilivyopata uhuru wake kutoka kwa mwingereza 1961. Hii ni historia muhimu inayopaswa kufundishwa na kuelezwa fasaha kwenye jamii zetu, hivyo tarehe hiyo inapaswa kuenziwa na kusheherekewa kitaifa.

Kwa miaka mingi serikali ya Tanzania imekuwa ikipotosha kwa kuogopa kusema wazi kuwa sherehe za uhuru za tarehe 9 Disemba ni sherehe za uhuru wa Tanganyika, badala yake inasema ni sherehe za uhuru wa Tanzania au Tanzania bara!

Vivyo hivyo kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuogopa kutamka na kusherekea kumbukumbu ya uhuru wa Zanzibar (10/Disemba/1963) na badala yake msisitizo uko kwenye sherehe za mapinduzi. Toka lini mapinduzi yakawa mbadala ya uhuru?

Historia iliyopotoshwa ni hatari kwa mwelekeo wetu wa kifikra wa leo, kesho na keshokutwa.
Hahaha
Sasa utasikia " kombe la mapinduzi" yaani zanzibar wanasherehekea mapinduzi na sio uhuru????
Nyerere bwana???
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom