Uhuru wa Habari Tanzania: Je, Vyombo Viko Huru? Je, Waandishi wa Habari wako huru? Wanathaminiwa?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,669
119,299
Wanabodi

Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha Uhuru wa Habari. Kwa Tanzania, maadhimisho rasmi yanafanyikia jijini Mwanza, katika kuadhimisha siku hii kwa Tanzania tunaadhimisha nini haswa?.

Wakati tukiadhimisha hicho tunachoadhimisha, hakuna ubaya tukitafakari baadhi maswali haya...
1.Jee Vyombo vya Habari vya Tanzania Viko huru?. Kwa kiasi gani?.

2.Jee Wandishi wa Habari wa Tanzania wako huru?. Wako Huru kwa kiwango gani?.

3. Jee Waandishi wa Habari wa Tanzania Wanathaminiwa?. Maslahi ya Waandishi yakoje?. Jee Wanathamani gani katika jamii?.

1.Jee Vyombo vya Habari vya Tanzania Viko huru?. Kwa kiasi gani?.
Japo Tanzania tuna sheria mpya ya uhuru wa habari lakini sheria hiyo bado inavipengele kandamizi, hivyo naweza kukiri kuwa vyombo vya habari vya Tanzania viko huru ila ni uhuru kwa kiasi fulani tuu. Uhuru wa kweli wa vyombo vya habari ni pamoja na uhuru wa kiuchumi. Kwa vile Tanzania ni nchi masikini, then vyombo vya habari vya Tanzania ni vyombo vya kimasikini, hivyo vyombo vikiwa ni masikini haviwezi kuwa huru!.

Kuna huu msemo wa "He who pays the piper may call the tune!". Anayemlipa mpiga zumari ndiye atakayechagua wimbo. Vyombo vingi vya habari Tanzania ni vyombo masikini hivyo nI wapiga zumari tuu, hivyo lazima vifuate matakwa ya mpiga zumari.

Na kama mkuu wa wapiga zumari amaishatoa onyo kuwa media isijidhanie iko huru kiasi hicho!. Nani atakohoa?!.

2.Jee Wandishi wa Habari wa Tanzania wako huru?. Wako Huru kwa kiwango gani?.
Ili vyombo viwe huru lazima viundwe na Waandishi huru, Jee Waandishi wa habari wa Tanzania wako huru na kama wako huru, wako huru kwa kiasi gani au kwa kiwango gani?.

Jibu la swali hili ni kama jibu la lile swali la kwanza, ukiwa na media masikini hoi bin taaban, haziwezi kuwa huru, then vyombo masikini vya habari vyenye Waandishi poorly paid, wasio na vitendea kazi bora, Waandishi wenye njaa, hawawezi kuwa Waandishi huru.

Ukiondoa vyombo vichache vyenye uwezo na vinavyowalipa vizuri Waandishi wake, vyombo vingi ni masikini hivyo Waandishi wengi wanalipwa malipo duni na wana Maslahi duni, hivyo hawawezi kuwa huru, ndio maana kumeibuka kada ya waandishi ma kanjanja wanao practice "petty cash journalism" ( habari zinazolipa), au "yellow journalism" (udaku) badala ya kuandika habari za muhidin kwa jamii na sio ajabu kukuta Waandishi wanakimbizana na bahasha ili angalau nao kushibisha matumbo yao!.

Hali hii ya umasikini huu umepelelea kila taasisi ukiandaa tukio la kihabari, unatenga na bahasha za Waandishi.

Waandishi wenye njaa wanaotegemea bahasha kuandika habari hawawezi kuwa huru kwa sababu uhuru wao utakuwa compromised na mtoa bahasha kwa mtindo ule ule wa he who pays the piper may call the tune!.
Angalizo:Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco wa JF!.

3. Jee Waandishi wa Habari wa Tanzania Wanathaminiwa?. Maslahi ya Waandishi yakoje?. Jee Wanathamani gani katika jamii?.
Waandishi wa Tanzania, hawathaminiwi, uandishi wa habari ni kazi nzuri na kazi rahisi, haswa utangazaji, hauhitaji kuwa na elimu kuubwa kivile, elimu ya form four inatosha sana kwa utangazaji wa kawaida, kinachotakiwa ni good look, good voice na kipaji. Utangazaji wa serious programs ndio unahitaji elimu nzuri, na specialization, very unfortunate, kwenye electronic media ya Tanzania, hatuna such serious programs zenye kuhitaji specializalization, kinachofanyika ni watangazaji kuwatumia professionals na kuwasilisha vipindi. Watangazaji wa TV na redio angalau, wanathaminiwa thaminiwa na jamii, ukienda mahali unajulikana, unapewa preferential treatments. Kwenye vinywaji unakula sana offers, na kwenye mambo ya ujana, kama ni mtangazaji wa kiume, unagombewa, na kama ni wa kike, wenye vipochi vinene, wanagombea. ila kuthaminiwa kote huku ni superficial tuu, mtangazaji akipata matatizo akaishiwa uwezo wa kutangaza, kiukweli utamuhurumia, wale marafiki waliokuwa wakikutafuta kukupa offers za kinywaji, simu zako hawapokei.

Lakini tukija kwa uandishi wa habari za magazeti, hii ni kazi inayohitaji elimu, na haswa uandishi wa habari za uchunguzi ni kazi ngumu na ya hatari, lakini sijui kama kuna media yoyote Tanzania, waandishi wake wana bima ya maisha. Kiukweli kabisa, ukiondoa sekta ya waalimu ambayo ndio inayoongoza kwa kuwa poorly paid, sekta ya habari ndio ya pili kwa malipo duni ukilinganisha na kinachofanywa, hivyo mkisikia waandishi wanagombea zile bahasha, naomba msiwashangae.

Kiukweli katika jamii, waandishi tunathaminiwa sana, when in need, lakini need ikiisha, tunadharauliwa na hatuna thamani yoyote. Hata kwenye hiyo mikutano, semina, warsha na kongamano, bahasha za waandishi huwa nyembamba ukilinganisha na bahasha za wajumbe wengine.

Paskali
 
Mkuu, Mayala wewe ni mwana habari kwa muda kiasi, sasa kwa maswali yako naamini unamajibu yote ila unajaribu kutuchora katuni.
.....keep it watch it ...
NJE YA MADA
Tatizo tunawaandishi wa habari wachache sana wengi kutokana na
Refer "your not ..fr to that extend
 
Lakini pia bwana Pascal Mayalla ningependa ungeuliza maswali katika upande wenu ili na sisi walaji wa habari toka kwenu mtuteendee haki
1.,Je waandishi wa habari wetu wanakidhi sifa ya uandishi wa habari?

2. Je waandishi wa habari wetu wana credibility (wana aminika)??
 
Bwana Paskali, kabla ya kuanza kukurupuka kujibu maswali yako muhimu tungepata tafsiri ya neno uhuru kwanza. Maana kinachotoa huo uhuru ni Katiba na Sheria. Sasa wakati tunajibu haya maswali tujiulize, katiba yetu imetoa uhuru? Kama imetoa uhuru ni kwa kiasi gani? Na hicho kiasi tunakipima kwa kipimio kipi? Parameters za huo uhuru ni zipi? Na ninyi wanahabari mlitaka uhuru wa namna gani? Kipi kikifanyika mtajiona mko huru?

Maswali ni mengi, utakapoanza kutiririka uje na majibu haya pia.

Mzito
 
Pascal Mayalla,

Nadhani ungeishia tu hapo katika kutuuliza maswali ingetosha ili sisi Wadau sasa tuweze ' kutiririka ' vizuri ila kwa kitendo cha Wewe huyo huyo kutuuliza maswali hayo halafu tena hapo chini ukaanza kujibu kwa ufafanuzi kidogo kimetufanya utufunge ' kimtazamo ' na badala yake wote sasa tunaweza kujikuta tukitoa majibu yanayoambatana na huo ' ushawishi ' wako wa awali.
 
Nadhani ungeishia tu hapo katika kutuuliza maswali ingetosha ili sisi Wadau sasa tuweze ' kutiririka ' vizuri ila kwa kitendo cha Wewe huyo huyo kutuuliza maswali hayo halafu tena hapo chini ukaanza kujibu kwa ufafanuzi kidogo kimetufanya utufunge ' kimtazamo ' na badala yake wote sasa tunaweza kujikuta tukitoa majibu yanayoambatana na huo ' ushawishi ' wako wa awali.
Naungana na wewe 100% na kwanza inaondoa kabisa maudhuo ya mada yenyewe.
 
Media inayofanya kazi ipasavyo siku zote haipendwi na tabaka linaloongoza nchi. Wasaidizi wa Trump siku za karibuni wamekuwa na uhusiano mbaya na baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani kwa sababu tu ya vyombo hivyo vinasimamia taaluma.

Vyombo hivyo vimepigwa mkwara kwa kuambiwa kwamba habari inayotoka hewani iwe ni ya uhakika vinginevyo kuna watu wanaweza kushtakiwa.

Journalism ya Tanzania ipo kwenye mchakato wa kutoka kwenye makucha ya mfumo wa chama kimoja. Bado masalia ya mfumo wa chama kimoja yana nguvu na ushawishi kwenye mienendo ya media yetu.

Nchi inapopata ongezeko la watu wa kada mbalimbali ambao wanao uelewa wa kada zao vilivyo, na media yetu inakutana na changamoto za wakati husika. Vinginevyo media inaweza kujikuta ikibakia kwenye hulka za wakati wa chama kushika hatamu wakati hii ni dunia ya utandawazi.

Yapo mambo ambayo hayaitendei haki media, na kibaya zaidi yanafanywa na mamlaka za juu lakini mambo hayo hayawezi kuwa ndio kigezo cha media yetu kutopigana kwa nguvu zetu katika kuimarisha weledi wa wanahabari.
 

Wanabodi, japo tukio hili waandishi tumedhalilishwa, haya ndio mambo niliyoyasema kwenye bandiko hili, waandishi wa habari hatuthaminiwi hadi kutupiwa pesa kama mbwa anavyotupiwa nyama!.

Sasa every Tom, Dick and Harry anaweza kuwa mwandishi, matokeo yake, makanjanja ambao hawakupita shule yoyote ya habari, hawajui maadili, wanatupiwa pesa kama mbwa na kuanza kugombania, hivyo kutuaibisha waandishi wote tuonekane ni watu wa hovyo, hatuna maana!..
P.
 
Back
Top Bottom