Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Ni wazi kuwa kuna Habari hazirushwi kwa sababu ya mashinikizo kutoka Serikalini. Moja ya vitu ambavyo vilikuwa vya hovyo awamu ya 5 ni suala la Kuminya Uhuru wa habari, kama habari ipo balanced sioni tatizo kwa nini isirushwe.
Juzi hapa kwenye mahojiano na BBC mama Samia alisema kuwa Uhuru wa habari upo. Ila hayo maneno yanapishana na alichofanya waziri gwajima, kwanza sioni tatizo lolote la kuzia kurusha ile habari ya Mtu kuanguka.
Watu wengi tu walishawahi kuanguka kabla hata ya janga hili la Corona, hivyo sikuona Kama ni tatizo hiyo habari ikirushwa. Kitendo cha kuwaambia waandishi kuwa wasirushe Hilo tukio ni wazi kuwa kuna mengi mnawaambia wasiyarushe hewani. Hii ni ajabu sana, bado safari ni ndefu.
Bado nawaza cha ajabu ni nini pale hadi kuzuia waandishi wasirushe lile tukio? Kwamba watu watahusisha na chanjo? Waziri Gwajima umekosea sana kuwakataza waandishi wa habari, na kuna kila dalili wataendelea kukatazwa kwenye mengine.
Huu Uhuru wa habari tunaosema kila siku upo wapi? Upo wapi? Hili suala linapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Chini nimeweka video Waziri akikataza waandishi wasirushe tukio.