Uhuru wa Habari bado ni tatizo nchini, Waziri Gwajima umefanya kosa kuzuia waandishi kufanya kazi yao

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,960
Ni wazi kuwa kuna Habari hazirushwi kwa sababu ya mashinikizo kutoka Serikalini. Moja ya vitu ambavyo vilikuwa vya hovyo awamu ya 5 ni suala la Kuminya Uhuru wa habari, kama habari ipo balanced sioni tatizo kwa nini isirushwe.

Juzi hapa kwenye mahojiano na BBC mama Samia alisema kuwa Uhuru wa habari upo. Ila hayo maneno yanapishana na alichofanya waziri gwajima, kwanza sioni tatizo lolote la kuzia kurusha ile habari ya Mtu kuanguka.

Watu wengi tu walishawahi kuanguka kabla hata ya janga hili la Corona, hivyo sikuona Kama ni tatizo hiyo habari ikirushwa. Kitendo cha kuwaambia waandishi kuwa wasirushe Hilo tukio ni wazi kuwa kuna mengi mnawaambia wasiyarushe hewani. Hii ni ajabu sana, bado safari ni ndefu.

Bado nawaza cha ajabu ni nini pale hadi kuzuia waandishi wasirushe lile tukio? Kwamba watu watahusisha na chanjo? Waziri Gwajima umekosea sana kuwakataza waandishi wa habari, na kuna kila dalili wataendelea kukatazwa kwenye mengine.

Huu Uhuru wa habari tunaosema kila siku upo wapi? Upo wapi? Hili suala linapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Chini nimeweka video Waziri akikataza waandishi wasirushe tukio.

Chanjo ndo imemfanya aanguke , na taarifa hyo ingezagaaa na criticism iliyopo kwenye jamii kuhusu chanjo kampeni ya kitaifa isingefanikiwa , maajabu ya hyo chanjo wanayajua ndo mana wanakusainisha fomu ya kujitoa endapo likitokea la kutokea, sio kwamba wanapenda na wao wapo under pressure of somebody
 
Watu walikuwa wengi hapo, Kuna waliokuwa wanachukua kwa simu na ndio hapo wameisambaza habari.
Uhuru wa habari wa kuchukuwa video kwa mtu anayeumwa? Kweli hii nchi ina wajinga. Yaani unasema kabisa huoni tatizo kuchukuwa vieo mtu anapokuwa kwenye maumivu? Umetoka mbuga gani wewe mtu usiyestaarabika namana hii.

Nyie ndiyo mnachukuwa picha na video za graphic na ku-share kama mnagawiana fedha. Mawazo yako ni kipori sana. Ulimwengu umestaarabika na hakuna binadamu mwenye akili anayeweza kufanya hicho unachotaka.
 
Chanjo ndo imemfanya aanguke , na taarifa hyo ingezagaaa na criticism iliyopo kwenye jamii kuhusu chanjo kampeni ya kitaifa isingefanikiwa , maajabu ya hyo chanjo wanayajua ndo mana wanakusainisha fomu ya kujitoa endapo likitokea la kutokea , sio kwamba wanapenda na wao wapo under pressure of somebody
alikua hajachomwa chanjo
 
Wewe usichanjwe, hii ishu si nihiyari kwanini mnapata shida?
 
Ni wazi kuwa kuna Habari hazirushwi kwa sababu ya mashinikizo kutoka Serikalini. Moja ya vitu ambavyo vilikuwa vya hovyo awamu ya 5 ni suala la Kuminya Uhuru wa habari, kama habari ipo balanced sioni tatizo kwa nini isirushwe.

Juzi hapa kwenye mahojiano na BBC mama Samia alisema kuwa Uhuru wa habari upo. Ila hayo maneno yanapishana na alichofanya waziri gwajima, kwanza sioni tatizo lolote la kuzia kurusha ile habari ya Mtu kuanguka.

Watu wengi tu walishawahi kuanguka kabla hata ya janga hili la Corona, hivyo sikuona Kama ni tatizo hiyo habari ikirushwa. Kitendo cha kuwaambia waandishi kuwa wasirushe Hilo tukio ni wazi kuwa kuna mengi mnawaambia wasiyarushe hewani. Hii ni ajabu sana, bado safari ni ndefu.

Bado nawaza cha ajabu ni nini pale hadi kuzuia waandishi wasirushe lile tukio? Kwamba watu watahusisha na chanjo? Waziri Gwajima umekosea sana kuwakataza waandishi wa habari, na kuna kila dalili wataendelea kukatazwa kwenye mengine.

Huu Uhuru wa habari tunaosema kila siku upo wapi? Upo wapi? Hili suala linapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Chini nimeweka video Waziri akikataza waandishi wasirushe tukio.

View attachment 1890597

Unachoweza kulalamikia ni endapo Waziri au mamlaka husika imezuia tukio hilo lisitangazwe wala kuchapishwa kwenye vyombo vya habari - kama TAARIFA YA HABARI.

LAKINI huwezi kudai hiyo video irushwe kwenye tv tena mubashara. Huo sio uhuru wa habari. Sheria za maadili ya media haziruhusu. Ni kama kumrekodi mgonjwa anapokata roho na kuirusha live.
 
"the internet is forever." hata atoe maelezo gani,watu wameshamsikia akiongea.. Hivi unamuaminije waziri ambaye idea yake ya kwanza ni kuficha ficha,,si kwasababu ya kumsitiri mgonjwa bali kwa sababu zake binafsi.... Tunashukuru jamaa ni mzima, mimi binafsi sihitaji context ya nn kilisababisha
 
Kongamano la masaa nane ndio idea yao ya raising public awareness strategy, only in Tanzania.

Yaani hawa watu ovyo kweli si waende ITV wakamtafute mtaalamu wao wa mass communication awape strategy.

ITV walifanya kazi kubwa sana kwenye kuufahamisha umma kuhusu corona na umuhimu wa kujikinga. Whoever was behind the campaign understands mass communication.

Kumbe hizi ziara za kukutana na viongozi wa dini na haya makongamano ya watu 100 kuongea ndio communication strategy ya kufikisha ujumbe kwa watu kwenda kuchanja.

Aisee
 
Katika research kwenye awareness huwa tunazingatia Sana first mention believing that this is what comes first to his or her mind. Sasa Hawa wote first mention yao ni chanjo. Sijui tuelewe nini hapo kwa kweli.
 
Unachoweza kulalamikia ni endapo Waziri au mamlaka husika imezuia tukio hilo lisitangazwe wala kuchapishwa kwenye vyombo vya habari - kama TAARIFA YA HABARI.

LAKINI huwezi kudai hiyo video irushwe kwenye tv tena mubashara. Huo sio uhuru wa habari. Sheria za maadili ya media haziruhusu. Ni kama kumrekodi mgonjwa anapokata roho na kuirusha live.
Lengo la waziri sio kulinda privacy ya mgonjwa, bali lilikuwa na ajenda yake ndio maana alikuwa anawaambia wasirushe ile habari kwa kuwa huu ni mpango wa taifa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom