Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,417
- 80,122
UHURU NI MUHIMU LAKINI UHURU WENYE MIPAKA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kila kiumbe kinahitaji UHURU. Zaidi viumbe wenye utashi Uhuru kwao ni Moja ya mambo MUHIMU na ya lazima katika maisha yao.
Kwa Sisi Watibeli, Uhuru ni Jambo Pana ambalo ndani yake lazima lisimamiwe na lifafanuliwe na yaleyale mambo Makuu manne, HAKI, UKWELI, AKILI NA UPENDO.
1. UHURU KAMA HAKI!
Hapa Watibeli tunafafanua Uhuru kama Jambo ambalo kiumbe hupewa au huwa nalo vile inavyomstahili.
Asipunguziwe Wala asiongezewe.
Mtu atapewa Uhuru unaomstahili(Haki yake) kulingana na Mambo Makuu yafuatayo;
a) Upeo wa AKILI
Ni kweli kila kiumbe kina Akili. Wapo viumbe wenye wenye Akili Sana, wenye Akili za kawaida na wapo wenye Akili kidunchu za kuwasaidia mambo basic.
Lakini upeo wa Akili kwa viumbe hubadilika kulingana na sababu mbalimbali kama umri na mazingira.
Hii ni kusema Uhuru wa Mtoto mdogo hauwezi kulingana na Uhuru wa Mtu mzima kutokana na upeo wa Akili Zao.
2. MAJUKUMU
Mwenye majukumu makubwa na Mengi hupewa Uhuru Mkubwa na Uhuru katika mambo mengi. Wakati mwenye majukumu madogo na machache hustahili Uhuru Mdogo na mchache
Na hii huingia katika Kanuni ya utawala na Uongozi. Mwenye Uhuru Mkubwa na mwingi au katika mambo mengi ndiye huwa Mtawala na anastahili kuwa kiongozi.
Kibaolojia na kisaikolojia, Ubongo ndio kiungo pekee ambacho kina Uhuru Mkubwa na mwingi kuliko kiungo chochote. Na hii inamaanisha Ubongo ndio hutawala Mwili na viungo vingine. Hii ni kutokana na kuwa majukumu ya Ubongo ni Mengi zaidi kuliko kiungo chochote katika Mwili.
Ingawaje viungo vya mwili vinashirikiana kwa ukaribu.
3. WAKATI
Wakati na muda ni Moja ya nguzo nyeti na muhimu kwenye HAKI. Huwezi utoa wakati au Muda unapozungumzia HAKI.
Uhuru kama Haki unawakati wake.
Kila Uhuru unamuda wake unaostahili.
Haki ya kujieleza, haki ya kujiamulia, Haki ya kujitegemea huamuliwa na kipengele cha Wakati.
Mtoto mdogo anahaki ya kujieleza na kujitegemea kisha kujiamulia mambo lakini Muda sahihi ukifika.
Kifalsafa, mtu huweza kujiuliza kwa nini mtoto mdogo akizaliwa asiongee papohapo au asijitegemee papohapo au kujiamulia mambo.
Kwa viumbe wenye utashi, kuna Uhuru kama Haki unaoamuliwa na Wakati au Muda.
Ingawaje Kanuni hii inaweza kuvunjwa kwa baadhi ya viumbe wasio na utashi ambao huweza kujitegemea na kujiamulia mambo siku tuu walipozaliwa.
4. MAUMBILE
Uhuru kama Haki unakipengele cha Maumbile.
Mwenye maumbile laini hawezi kufanana Uhuru wake na mwenye maumbile magumu.
Mwenye maumbile makubwa Uhuru wake hauwezi kufanana na mwenye maumbile madogo.
Maumbile ya Kike Uhuru wake hauwezi kuwa Sawa na maumbile ya kiume.
Huo ni muhtasari wa maelezo yaliyopo katika Kitabu cha UHURU KUTOKA GIZANI KUIFUTA NURU. Ambacho kimeandikwa na Mtibeli, ambacho kinaelezea zaidi jinsi mtu anavyoweza kuifuata na kuipata Nuru katika maisha yake. Naam kutoka GIZANI kuingia nuruni.
2. UHURU KAMA UPENDO!
Kuifuata Nuru na maisha ya Mtu na kuangazwa na miale ya Mwanga wa upendo ni Uhuru unaotafutwa na viumbe vyote Duniani.
Maisha ni mvutano, kuvutwa na kuelekea katika jumuiya yenye kuleta nguvu Chanya ya furaha.
Uliwahi sikia nguvu za uvutano wa kigraviti Kati ya Dunia na mwezi au Dunia na Jua. Au Uvutano wa sayari na sayari, au Uvutano wa Galaxy yetu na Galaxy zingine. Mvutano huu ni sehemu ya kuyafanya maisha yaendelee na yatokee. Kwani nguvu na Nishati mbalimbali huweza kubadilishwa kwa namna nyingine inayoweza kuyafanya maisha yawe Bora zaidi.
Katika mvutano kuna msuguano. Hata hivyo sipo hapa kueleza kinyume chake yaani muachano.
Kila kiumbe kina Njia ambayo kitaipitia. Hii ni kumaanisha kila kiumbe kina Njia yake. Kila mtu ananjia yake.
Ni muhimu kujua kuwa Kila Njia ya Mtu inaelekezwa kwenye chanzo cha Nuru. Hii ni kusema kila kiumbe huitafuta Nuru.
Maisha ya Mtu ni kama Mche uliopo ardhi unapambana Kutafuta upenyo kwenye ardhi ili Mche huo uone Mwanga wa Jua. Nuru! Yes Nuru! Every creature follows the Light. Yes, follow the Light.
Katika kufuata Nuru kwa kila mtu Akiwa katika Njia yake ndipo mvutano baina yake na waliopo katika Njia zingine hutokea. Mvutano huo ni mvutano wa Asili na kamwe hauwezi kutengeneza. Mvutano huo ndio huitwa UPENDO.
Hii ni kusema upendo ni nguvu au Nishati ya Uvutano baina wa viumbe. Nishati hii ndio huzalisha mambo kama furaha, Amani, utulivu n.k.
Uhuru katika kupenda ni Uhuru wa Asili ambao unalugha zake kiasili, ambapo kwa Lugha ya kawaida ya mwili ni ngumu kuielezea.
Katika mvutano wa watu ambapo kunatokea msuguano wakati mwingine hisia za maumivu huweza kujitokeza.
Kama ilivyo kwenye mfumo wa Nyota angani. Mvutano hutokea kwa Nyota zilizo kwenye galaxy Moja au ambazo Njia zake zimekaribiana
Hapa tunafafanua Uhuru katika Upendo. Kwa kufupisha.
Upendo katika Uhuru unajengwa na mambo Makuu yafuatayo;
a). MFANANO
Ingawaje watu wengi husema kuna Uhuru wa kupenda lakini kikanuni za asili upendo unamipaka yake.
Huwezi mpenda mtu ambaye hamfanani.
Kwa sababu upendo moja ya Kanuni zake kuu ni MFANANO.
Sababu nyingine nilishasema kuwa Kila kiumbe kimezaliwa kwaajili ya Kutafuta Nuru. Ambapo Nuru hiyo huweza kuwa na tafsiri nyingi kimantiki. Nuru ni maendeleo au mafanikio kwa wanauchumi, wanajamii na wanasayansi.
Kiimani, Nuru ni Mbinguni, angani, juu kabisa.
Kifalsafa, mtu akikuambia hutoenda Mbinguni au peponi au hatma yako(your Future) haitakuwa nzuri anamaanisha Jambo lilelile la kuwa maisha yako yatakuwa hayakuwa ya maana. Hukuweza kuipata Nuru ya Kweli.
Na ili upate Nuru lazima upate mtu mnayependana. Na ili mpendane lazima mfanane.
Kuwa na mtu ambaye hamfanani ni kujaribu kumaliza future yako. Nuru yako.
Katika MFANANO kuna mambo Makuu yafuatayo;
I) Akili
Uelewa, mtazamo, Msimamo na ufahamu ni mambo ya muhimu Sana kwenye upendo.
Kama Akili zenu hazifanani ni kwamba hampendani. Huwezi kuvutwa na mtu ambaye Akili zenu hazifanani Wala hazikaribiani. Future yenu haitakuwa nzuri bila Shaka. Hamtaiona Nuru.
Akili ndio huongoza maisha ya Mtu na kiumbe.
ii). IMANI
Msingi Mkuu wa Imani ni upeo wa AKILI. Kwani Imani huja kwa kupitia Milango ya fahamu kama kuona, na kusikia lakini pia Mlango wa fahamu wa tafakuri. Mambo hayo yote huamuliwa na upeo wa AKILI.
Huwezi kumpenda au kupendana na mtu ambaye hamfanani kiimani au Imani zenu hazina ukaribu.
Mambo hayo mawili ndio huunda kitu kinaitwa Utamaduni (Mila, desturi, na miiko).
Huwezi pendana na mtu ambaye hamfanani kiutamaduni (kiakili na kiimani).
Ingawaje unaweza ukajidanganya ukampenda mtu wa aina hiyo lakini matokeo yake yatakujulisha kuwa huwezi.
Ni Sawa useme sumu haionjwi lakini wapo wanaoonja na hiyo haimaanishi kuwa matokeo Mabaya hayatatokea.
b) UKARIBU
Unaweza usifanane na mtu lakini kukawa na ukaribu.
Nilisema upendo ni mvutano. Na vinavyovutwa ni vile vilivyo karibu na vile vyenye mfanano.
Wahenga walitangulia kusema ndege wafananao huruka pamoja. Hiyo ni Kanuni ya Dunia.
Wakasema pia, aliyekaribu na waridi hunukia Waridi.
Na Fimbo ya Mbali haiui Nyoka. Ambapo kimantiki wanarejelea falsafa ileile ya ukaribu na MFANANO ndio Kanuni kuu ya Upendo.
Kisiasa na kiutawala, unapoongoza watu au Jamii Kanuni hizo lazima zizingatiwe kwa Sababu ndio hatma na future yako au future Njema ya chama iliko.
Vyama vya siasa huweka mahusiano yenye Tija na vyama rafiki ambavyo vinafanana navyo kisera na kiitikadi. Pia vinaukaribu wa kisera na kiitikadi hata kama havifanani.
Ni kweli unauhuru wa kumpenda au kupendana na mtu lakini hatuwezi kuukataa ukweli kuwa kuna mipaka ya kupenda na kupendana.
Na hii ni kama Mtu anahitaji kutopotea katika Orbit(Njia) yake na kuangamia.
3. UHURU KAMA UKWELI.
Uhuru kwa Watibeli lazima uzingatie uhalisia wa wakati na mazingira. UKWELI ni muhimu kwenye maisha kwa Sababu maisha yenyewe ni kweli tupu.
Uhuru kama ukweli utazingatia zaidi mambo Makuu yafuatayo;
a) Wakati, Muda na umri.
Ukweli unawakati, umri, na Muda.
Sio Muda wote ukweli unahitaji. Lakini hiyo haimaanishi uwe Muongo.
Ikiwa ukweli utaleta madhara makubwa na kuathiri future yako au ya Jamii ni muhimu ukweli huo kuusubirisha Mpaka wakati ambao hautakuwa na madhara ndipo utolewe.
Ni kweli kila mtu anauhuru WA kuongea ukweli lakini lazima ukweli huo uwe na mipaka. Ili kutoharibu Future iliyobora.
b) MUKTADHA
Wakati, mazingira na Hali ndio huitwa MUKTADHA.
Ukweli lazima uzingatie muktadha.
Sio tuu kwa Sababu ni ukweli Basi utolewe au ufanywe. Na ndipo hapo umuhimu wa Akili unapojitokeza.
3. UHURU KAMA AKILI.
Uhuru kama Akili ni ule uwezo wa Mtu kutumia Uhuru wake kuchambua mambo, kuchanganua, kuyatafsiri, kuyachambua, kuyakumbuka, kutatua matatizo na kuboresha ili kuifikia Nuru au hatma Bora.
Nimechoka Wakuu!
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam