Tee Bag
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 7,220
- 5,627
UHURU NA KUJIAMINI NI WATOTO MAPACHA
Wewe upo huru, yaani wewe ni mtu huru. Hata hivyo, ili uweze kuuhisi huo uhuru wako inabidi kwanza ujiamini.
Unahitaji kuwa huru, unahisi haupo huru. Hata hivyo, ili uupate uhuru unaouhitaji inabidi kwanza mwenye kutakiwa kukupa uhuru awe mwenye kujiamini.
Uhuru na kujiamini ni watoto mapacha; kama mume hajiamini kwa mkewe, lazima atamnyima uhuru. Atambana na kumdhibiti asifanye kazi au kuwasiliana na watu.
Mke hawezi kuwa huru na simu yake kama mumewe hajiamini. Maana ikiita tu mume atatoa macho kutaka kujua mpigaji ni nani na mazungumzo yatakuwaje.
Mume akiwa hajiamini, mke hawezi kuwa huru kukaa na houseboy jikoni. Kinyume chake mume akiwa anajiamini, mke atajisikia huru kuzungumza na yeyote na kuwasiliana na yeyote.
Mume akiwa mwenye kujiamini, mke huwa huru hata kwenye simu yake. Anaweza kuiacha mbele ya mume wake na ikiita atauliza: "hubby nani huyo anapiga?" Maana hana wasiwasi.
Mume akiwa hajiamini, mke hukosa amani hata kupokea simu ya mfanyakazi mwenzake. Maana mume hashindwi kuuliza maswali magumu kutokana na kutojiamini kwake.
Kadhalika mke akiwa hajiamini, mume lazima atakosa uhuru. Simu akiiacha kidogo atakuta imepekenyuliwa. Akikuta namba ya mwanamke 'ataisevu' kwake amtafute.
Mke akiwa hajiamini hata housegirl hukiona cha moto. Dada wa kazi akitaka kukaa sebuleni aangalie TV atafukuzwa, eti asimzoee mumewe. Akiketi kwenye meza ya chakula, ataambiwa akale peke yake jikoni.
Dada wa kazi akivaa na kupendeza, mama mwenye nyumba roho juu. Baba akimwita dada wa kazi ili amtume, mama anakuwa mkali.
Mume akiwa hajiamini hata apewe uhuru upi na mkewe, atakuwa mwenye kujishtukia tu. Hivyo atakuwa anajibana mwenyewe.
Mke pia akiwa hajiamini, mume wake akimpa uhuru, atakuwa anajibana na kujishtukia. Ni kwamba ili mtu ajihisi yupo huru, inabidi yeye mwenyewe awe mwenye kujiamini.
TUTAELEWANA TU
Utakuwa huru kama anayetakiwa kukupa uhuru anajiamini. Vilevile utajisikia upo huru ikiwa unajiamini.
Bosi akiwa hajiamini ofisini, wafanyakazi hawawezi kuwa huru. Atawaweka kwenye presha kila siku. Maendeleo binafsi ya mfanyakazi kwa bosi ni nongwa.
Bosi akiwa hajiamini, mfanyakazi wa chini hatakuwa huru kuonesha kipawa chake. Bosi atambana, ataona mtu wa chini yake anaweza kumfanya yeye aonekane hana ubora.
Maana yake ni kuwa bosi akiwa anajiamini, kisha mfanyakazi naye akawa ni mwenye kujiamini, matokeo yake mfanyakazi atajiona yupo huru kuonesha kila alichonacho.
Kujiamini kuna tafsiri tatu. Anayetakiwa kutoa uhuru akiwa anabana na kumfanya mwenzake asiwe huru, huo ni wivu.
Ndiyo, mume anambana mumewe kwa sababu hajiamini. Kutojiamini kwake kunasababishwa na wivu.
Bosi anamnyima uhuru msaidizi wake kwa sababu hajiamini. Kutojiamini kwake kunajengwa na wivu, kwamba atastawi kuliko yeye.
Mume anapewa uhuru lakini hajiamini, kutojiamini huko ni kujishtukia. Kadhalika mke naye anapewa uhuru ila anajibana kwa sababu hajiamini. Kutojiamini kwake ni kujishtukia.
Tafsiri ya tatu ya kujiamini ni kujitambua. Mume anajiamini na anajitambua, kwa hiyo hana hofu. Anamwacha mkewe awe huru. Vivyo hivyo kwa mke dhidi ya mume.
Bosi anayejiamini maana yake anajitambua. Anaelewa nafasi yake na anaona anatosha, kwa hiyo hahofii wa chini yake. Anawapa uhuru kila mmoja kuonesha karama yake ili kusaka mafanikio ya pamoja.
KUJIAMINI KWENYE UTAWALA
Mtawala akiwa hajiamini, wasaidizi wake na wananchi wa kawaida hawawezi kuwa huru. Maana yake kiongozi mwenye kujiamini ni yule ambaye huwapa watu uhuru wao kamili.
Uhuru wa kutoa maoni na kufanya kazi zao, maana anafahamu nini anafanya, kwa hiyo hawezi kujisumbua kwa mambo ambayo anajiamini hayawezi kumteteresha.
Sifa ya kiongozi mwenye kujiamini utamuona jinsi asivyojishughulisha na vitu vidogo. Kiongozi asiyejiamini huwapa presha mpaka raia wa chini na kuwafanya hisia zao wanong'onezane.
Kiongozi asiyejiamini alidhihirika Italia Karne ya 16. Astorre Manfredi alikuwa mwanamfalme (prince) wa Faenza, Italia. Zaidi, Manfredi alikuwa kijana mzuri na mtanashati.
Watu walimpenda Prince Manfredi kwa vipaji vyake. Alipoongea tu alivutia kumsikiliza. Watu walipenda kumsogelea na walivutiwa na akili nyingi alizokuwa nazo, vilevile namna alivyojiweka.
Mwaka 1500, vikosi vya Cesare Borgia viliivamia Faenza. Watu wote kwenye mji huo walisalimu amri. Hakuna umwagaji damu kwa sababu hakukuwa na mapambano.
Tatizo likawa Borgia kila alipomtazama Prince Manfredi alimwonea wivu, aliona dhahiri watu walimkubali sana kuliko yeye. Kipindi chote watu wakionesha kumpenda Prince Manfredi, mwenyewe hakuonesha mbwembwe wala maringo. Alikuwa mjanja sana, lakini kila alipojitahidi kuficha karama zake, bado Borgia alizidi kumhofia.
Borgia aliendelea kujiona hayupo salama kwa utawala wake mbele ya Prince Manfredi. Kipindi hicho Manfredi alikuwa na umri wa miaka 18 tu. Hapo unaweza kuona jinsi kiongozi asiyejiamini anavyoweza kurukwa akili na kukosa simile anapoona anafunikwa.
Manfredi na umri wake mdogo aliokuwa nao, hakuwa na madhara, wala hakuwa mzungumzaji, lakini Borgia alikosa raha na hakupata usingizi. Jinsi watu walivyompenda Manfredi, ndivyo naye alivyokosa amani na kuzidisha chuki.
Baada ya kuona Manfredi ni tatizo kubwa, Borgia aliagiza atupwe jela kwenye gereza la Roman. Alikaa jela kwa muda mrefu, huko nako Manfredi sifa zake zikawa zinatoka nje na kusambaa, hivyo kufanya watu wazidi kumpenda.
Hali hiyo ilizidi kumtesa Borgia. Baada ya Manfredi kukaa jela mwaka mmoja, siku moja, mwaka 1501, mwili wa Manfredi ulikutwa umetupwa kando ya Mto Tiber, jiwe likiwa limefingwa shingoni, kuonesha kuwa aliuawa na kuzamishwa mtoni ili mwili wake usionanekane.
Kiongozi asiyejiamini anaweza kukupenda sana, lakini ukionesha kitu kumzidi yeye hawezi kufurahi, atanuna.
Mwishoni mwa Karne ya 16, ilikuwa mwaka 1591. Aliyekuwa Mfalme wa Japan, Hideyoshi, alimpenda sana mshauri wake aliyeitwa Sen no Rikyu, ambaye alikuwa msanii wa sanaa ya chai ya Kijapan (Japanese Tea Ceremony) ambayo kwa Kijapan inaitwa Chanoyu.
Kwa mapenzi makubwa ambayo Hideyoshi alikuwa nayo kwa Rikyu, alimpa mpaka nyumba (apartment) kwenye makazi ya mfalme. Waliishi vizuri mno. Hata hivyo, siku Hideyoshi alipogundua kuwa Rikyu alikuwa na sanamu lilichongwa taswira yake, alikasirika mno.
Uamuzi wa Hideyoshi ulikuwa ni adhabu ya kifo kwa Rikyu. Kweli, Rikyu aliuawa. Watu walishangaa mno kwa uamuzi huo kwa sababu ilikuwa ikifahamika kwamba Hideyoshi alimpenda sana Rikyu. Kutojiamini ni mzigo.
Tuombe kuwa na viongozi wenye kujiamini na sisi wenyewe tujiamini ili tuwe huru na tuuhisi uhuru wetu. Tukipewa uhuru, kama hatujiamini hatuwezi kuuhisi uhuru wetu, tutajishtukia, tutajibana.
Tukinyimwa uhuru kama hatujiamini, hatuwezi kujua kama tumenyimwa uhuru. Hivyo, inabidi tujiamini. Kujiamini ni alama ya kujitambua. Asiyejiamini ni yule asiyejitambua.
Ndimi Luqman MALOTO