Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemwandikia Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres, akimuomba kujadili juu ya kuanzisha Kinga ya Kutoshitakiwa (immunity) kwa Viongozi walioko madarakani. Endapo hoja hiyo itakubaliwa, Mahakama ya Haki (ICJ) inayochukuliwa kama Mahakama ya Dunia, italazimika kutekeleza uamuzi huo.
Lengo la kutaka kujadiliwa kwa hoja hiyo ni kutokana na suala la Immunity kusumbua sana katika miaka ya hivi karibuni. Uamuzi huo, umekuja kwa wakati ambao Nchi za Kiafrika zimekuwa zikiipinga Mahakama ya Makosa ya Jinai (ICC) juu ya msimamo wake wa muda mrefu wa kumshitaki Rais wa Sudan, Omar al-Bashir kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji ya kimbari (genocide) na uhalifu wa kivita.
Je, CHADEMA wanakubaliana na maamuzi hayo ya Role Model wao? Je, siyo vizuri wakatoa tamko?
Na hapa ndipo pa kumtofautisha Rais Magufuli dhidi ya wanafiki. CHADEMA toeni tamko kama ambavyo mmekuwa mkimuunga mkono Kenyatta.
Je, angekuwa Rais Magufuli ndiye amepeleka petition hiyo, ingekuwaje.
Wajuvi wa mambo ya haki za binadamu, pamoja na wazee wenzangu wa kutoa mapovu tusaidiane juu ya hili.