UHURU: CHADEMA yapasuka

DWSDevelopmentWater2big.jpg
school+kids+getting+drinking+water.JPG
 
Nilidhani wenye habari hii ni gazeti la maana kumbe ni uhuru!Ngoja nijipumnzikie mie.
 
Masikini Uhuru, hata habari ya kenya nayo ni ya kizushi, kenya hawana wagombea uraisi, maana kuitwa mgombea ni mpaka tume ya uchaguzi ikutangaze, sasa wenzetu nadhani muda bado sana tu, sijui uhuru wamayatoa wapi hayooooo?
 
Source: Uhuru mnapoteza muda kwenye mambo ambayo siyo ya msingi baadala ya kushughulika na matatizo ya wapiga kura wenu.
time will tell!

Kwanza gazeti la uhuru ni la kusomwa na watu wambeya na mashakudaku tu,halina mvuto wala tija,ni hasara tupu.Mwenye macho haambiwi tazama,tumeshuhudia magamba wameagwa kusini kwa macho ya watz wengi,uhuru hawana ubavu wa kutupa unbeya tukakubali,wanachadema tulishaweka pamba kwenye masikio juu ya umbeya wowote dhidi ya chama letu mpaka kieleweke.CORTIDE TUNGA KIBAO KUHUSU WANACHADEMA KUWA TAYARI KUSHEREKEA UHURU WA PILI NA WA KWELI 2015.
 
Ziara ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika mikoa ya Kanda ya Kusini, imehitimishwa kwa viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.
Willbroad Slaa kutofautiana.

Hali hiyo ilisababisha msuguano mkali ndani ya kikao cha ndani cha tathmini kilichofanyika mjini Ruangwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi
Likangara mjini hapa.

Kutibuana huko kulitokana na Mbowe kukataa mpango wa Dk. Slaa kutimua viongozi katika maeneo mbalimbali ambako ziara hiyo imefanyika wakiwemo viongozi karibu wote wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Ruangwa, ambapo Mbowe alipinga hatua ya Dk. Slaa kutaka baadhi ya viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya Abdallah Mang'onyola na mlezi wa chama hicho wilayani hapa Juma Lichonyo ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho waachie madaraka.

Kikao hicho kilichoanza majira ya saa 2: 30 usiku hadi saa tano, kilifanyika baada ya kumalizika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kidogo.

Habari za ndani za uhakika zinasema kuwa mahudhurio hafifu ya watu ndiyo yamemsukima Dk. Slaa kuamuru kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi hao akidai wamekisaliti chama hali iliyomfanya Mbowe kupinga, akisema
mpango huo unasababisha chama kulegalega.

Kwa mujibu taarifa za uhakika mkutao huo ulilenga kufanya thathmini baada ya ziara ya viongozi wa Chadema wilayani hapa kukosa watu wengi katika mikutano yao tofauti na matarajio yao hivyo kudai ni hujuma zinafanywa na
viongozi waliowatimua.

CHANZO: NIPASHE
Ngoromiko, siku hizi UHURU inaitwa NIPASHE! Unajua UHURU haliaminiki ukaweka Nipesha siyo? Propaganda uchwara hizo.
 
kufurika kwa watu wengi uwanjani sioni kama ndio sababu kua chama kinapendwa..mnakumbuka kule arumeru mikutano ya ccm ilikua imejaa maelfu ya watu lakini wakapigwa chini kwenye uchaguzi.
 
Katika chama cha demokrasia, kutofautiana sio habari! Kama walitaka 'kupigana' labda hiyo inaweza kuwa habari!
 
Ziara ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika mikoa ya Kanda ya Kusini, imehitimishwa kwa viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.
Willbroad Slaa kutofautiana.

Hali hiyo ilisababisha msuguano mkali ndani ya kikao cha ndani cha tathmini kilichofanyika mjini Ruangwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi
Likangara mjini hapa.

Kutibuana huko kulitokana na Mbowe kukataa mpango wa Dk. Slaa kutimua viongozi katika maeneo mbalimbali ambako ziara hiyo imefanyika wakiwemo viongozi karibu wote wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Ruangwa, ambapo Mbowe alipinga hatua ya Dk. Slaa kutaka baadhi ya viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya Abdallah Mang'onyola na mlezi wa chama hicho wilayani hapa Juma Lichonyo ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho waachie madaraka.

Kikao hicho kilichoanza majira ya saa 2: 30 usiku hadi saa tano, kilifanyika baada ya kumalizika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kidogo.

Habari za ndani za uhakika zinasema kuwa mahudhurio hafifu ya watu ndiyo yamemsukima Dk. Slaa kuamuru kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi hao akidai wamekisaliti chama hali iliyomfanya Mbowe kupinga, akisema
mpango huo unasababisha chama kulegalega.

Kwa mujibu taarifa za uhakika mkutao huo ulilenga kufanya thathmini baada ya ziara ya viongozi wa Chadema wilayani hapa kukosa watu wengi katika mikutano yao tofauti na matarajio yao hivyo kudai ni hujuma zinafanywa na
viongozi waliowatimua.

CHANZO: NIPASHE
Watakubishia!!!!!
 
Ngoromiko, siku hizi UHURU inaitwa NIPASHE! Unajua UHURU haliaminiki ukaweka Nipesha siyo? Propaganda uchwara hizo.

Kuna wana nyinyiemu wanaamini kuwa watashinda mwaka 2015,wanaota mchana kutwa,CDM NI LAZIMA ITASHINDA KWA 50.62% AMINI USIAMINI.
 
Ngoromiko, siku hizi UHURU inaitwa NIPASHE! Unajua UHURU haliaminiki ukaweka Nipesha siyo? Propaganda uchwara hizo.

Naelewa tofauti ya UHURU na NIPASHE. Ni magazeti mawili tofauti. Source yangu ni NIPASHE, nashangaa mnatokwa na mapovu ya bluu kwa kung'ang'ana kuwa si kweli.

MODS waki-prove kuwa source yangu si kweli.... wanifungie maisha.
 
Mkuu humu ndani kuna mi mtu ina vichwa vigumu kama NAZI,sasa inakubishia wakati hata bei ya gazeti lenyewe hayajui...gosh!
 
Nami naunga mkono 100% kwamba kama hii habari haiko kwenye website ya Nipashe, MODS wanifungie maisha.
kama mtoto vile...si uweke link basi watu wakuelewe unang'ang'ana kulazimisha uaminiwe ilihali una kithibiotisho? weka link ya hiyo habari kuwaprove wrong wanaopinga
 
Back
Top Bottom