UHURU: CHADEMA yapasuka

UHURU: CHADEMA yapasuka

I think badala ya kuwa na denial, CCM wanatakiwa wajiangalie, wakubali mapungufu na kuanza kurekebisha... this denial doesnt take them anywhere, sanasana itawafanya wawe comfortable na excuses plus lies

CCM WANAHITAJI KUJIANGALIA SANA NA HASA WATU WALIOWAKABIDHI KAZI
 
Uhuru ndo kazi yake hio likikosa ruzuku litajifia lenyewe. Hivi umelikuta wapi manake kulipata ni issue
 
Hili neno kuwaka limekujaje?
Issue kama ilikuwa kutofautiana kwenye maoni mbona mambo ya kawaida?
Chadema kama chama makini siku zote inasimamia maamuzi ambayo yamechambuliwa kwa kina, na yanatolewa baada ya kuanyiwa assessment. Au mlitaka mtu moja akiamua kutoa maoni yake ndo maamuzi ya mwisho?
Acheni kupotosha bana.

I stand to be corrected
 
Ziara ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika mikoa ya Kanda ya Kusini, imehitimishwa kwa viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.
Willbroad Slaa kutofautiana.

Hali hiyo ilisababisha msuguano mkali ndani ya kikao cha ndani cha tathmini kilichofanyika mjini Ruangwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi
Likangara mjini hapa.

Kutibuana huko kulitokana na Mbowe kukataa mpango wa Dk. Slaa kutimua viongozi katika maeneo mbalimbali ambako ziara hiyo imefanyika wakiwemo viongozi karibu wote wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Ruangwa, ambapo Mbowe alipinga hatua ya Dk. Slaa kutaka baadhi ya viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya Abdallah Mang'onyola na mlezi wa chama hicho wilayani hapa Juma Lichonyo ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho waachie madaraka.

Kikao hicho kilichoanza majira ya saa 2: 30 usiku hadi saa tano, kilifanyika baada ya kumalizika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kidogo.

Habari za ndani za uhakika zinasema kuwa mahudhurio hafifu ya watu ndiyo yamemsukima Dk. Slaa kuamuru kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi hao akidai wamekisaliti chama hali iliyomfanya Mbowe kupinga, akisema
mpango huo unasababisha chama kulegalega.

Kwa mujibu taarifa za uhakika mkutao huo ulilenga kufanya thathmini baada ya ziara ya viongozi wa Chadema wilayani hapa kukosa watu wengi katika mikutano yao tofauti na matarajio yao hivyo kudai ni hujuma zinafanywa na
viongozi waliowatimua.

CHANZO: NIPASHE

Wewe bwana usifanye watu wajinga. Habari hiyo imetolewa na gazeti la UHURU la leo. Gazeti makini haliwezi kuandika habari ya kuumba. Gazeti la magamba ndiyo kazi yake make halikuona misiba ya kenya na Makani siyo habari.
 
SAM_2487.JPG

Kulumbana kwa hoja si kugombana. Leo hapa msibani walikuwa hivi.
 
kumbe kimewaka tu,mi nilidhani Dr slaa ametangaza kuhamia chama cha mafisadi,kuwaka sio isue!!!!pamoja na kuwaka huko mtaendelea kuvua magamba yenu na kuvaa magwanda yetu
 
Mkuu hii habari umeleta nusu je hili gazeti limeandika kikao kilifanyika wapi na lini? Siliamini gazeti la Uhuru lakini siwezi kukubali wala kukataa kwasababu sina baseline ya kufanya hivyo. Naomba mwenye habari kamili kutoka katika gaezeti hilo aiweke hapa. Naomba wadau munisaidie kuelewa suala hili kwanini nyote mumepinga suala hili, je kuna habari za ndani ya CDM zilizothibitisha hakuna kitu kama hiki au kwasababu ipo kwenye gazeti la magamba tu?.
 
"Waacheni wafu wazike wafu wao"ccm na porojo na Chadema na sera na mipango tunazidi kusonga mbele.
 
Ngoromiko means shetani, ibilisi lusifa, belzebuli.... Nakushauri acha mambo ya CDM yalivyo ujue yeyote anaye wahuzunisha wana wa nchi kwa habari za kutunga ili kuibeba ccm laana haitamwacha. Acha kabisa.


Lolote linawezekana. Kama hamlijui hili, TISS (Usalama wa Taifa) wamepewa kazi maalumu na Serikali ya C C em kuhakikisha wanawavuruga aidha Dr. Slaa Vs Mbowe, Mbowe Vs Zitto au Dr Slaa Vs Zitto. Ni kazi imeandaliwa toka ngazi za Wilaya hadi Taifa.

Naomba tusiibeze habari hii, bali tuifanyie kazi. Huu ni mpango uliosukwa ili kukivuruga CDM kabla ya 2015.

Take it from me and act promptly.
 
Hata kama ni kweli limetokea hili na baadaye kuafikiana basi hiyo ndiyo demokrasia. Si lazima atakalo amua mwenyekitii ama katibu basi kikubalike tu. Kama ilikuwa ni kikao, basi ikitokea kutofautiana ni sawa. Mwisho wa siku mnatoa maamuzi yaliyoamuliwa na kupimwa na wengi kutokana na hoja husika. Nahisi watu mmezoea maamuzi ya kiditekta, yani fulani akisema wote mnafyata hata kama yanamapungufu makubwa.
 
Kipi cha ajabu, kutofautiana mawazo mbona nikawaida 2, si ndo maana ya vikao!
 
kama source ni uhuru,na mtoa mada kasema ni nipashe kwanin thread isifungwe?
 
Katika magazeti yanayotakiwa kusomwa kama barua (sensu Makinda) ni hili la uhuru.
 
ngoromiko ni majini na mapepo na baba yao ni shetani babu yao lusifa na lugha zao ni UONGO MTUPU. (maisha bora kwa kila Mtanzania.
 
Back
Top Bottom