Uhuru au mapinduzi?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]Written by Stonetown (Kiongozi) // 19/11/2012 // Kitaifa // 8 Comments

podcast1-564x272.jpg

Wazanzibari wanakaribia kutimiza nusu karne ifikapo January 12 tokea Mapinduzi ya nchi hiyo, kuna fikra tofauti ya kwamba Wazanzibari ni lazima waanze kusherehekea siku yao ya uhuru pia, uhuru ambao ulipatikanwa siku ya December 10, 1963 kutoka kwa Muengereza.
Wale wanaosindikiza kutambulia kwa siku hiyo wengi ni vijana, lakini wengi wa wazee, hususan wale ambao waliopata kushiri katika Mapinduzi wanapinga wazo la kusherehekea Uhuru na kuienzi siku hii.
Haikubaliki kuisherehekea siku ya December 10 kwa Wazanzibari, na wale wafanyao hivi ni lazima wajue wanafanya makosa na wanawapoteza Wazanzibari wenzao.
JEE NI NINI MAONI YAKO?!


[h=4]Related Posts[/h][h=3]Bodi yafungia Hospitali tatu, nyengine yafutiwa leseni.[/h]
[h=3]Ramadhan Qur’an Contest 2012 (1433 A.H.) Apply Now[/h]
[h=3]Mkono wa Pole kutoka ZAWA UK[/h]


[h=3]Viongozi wa SMZ mnabururwa![/h]

[h=3]Tunataka kiti chetu UN[/h]











[h=3]8 Comments on "UHURU AU MAPINDUZI?"[/h]


  1. santorini 19/11/2012 kwa 12:39 um · Ingia kujibu
    Maoni yangu inafaa sana kusherehekea siku hiyo kwani ni siku ambayo wazanzibari wamejikomboa kutoka kwa muingereza ambaye alijipenyeza katika utawala wetu.Mfalme jamshid alikuwa na haki ya kutawala au kuwa mkuu wa nchi kwani babu wa babu yake alikwenda kuitwa na wazanzibari wenyewe, wali kuja kuwakomboa kutokana na mshenzi mreno .Faida kubwa imepatikana lakini asie na shukurani haioni ,faida iliyopatikana ni kudumishwa uislamu na kama sio yeye muarabu angelibakia mreno leo misalaba ingelienea mpaka viunoni kwa mama na dada zetu.
    Lakini pia ustaarabu umekuwa sana kutokana na babu zake jamshid na kama si ustaarabu huo wa kiislamu leo sheni asingelipakaa hapo kwani bila ustaarabu wa kiislamu ingelikuwa ushenzi ushenzi .
    Kwa ufupi iko haja ya kusherehekea siku hiyo adhim kwani uhuru ulipatikana bila umwagaji wa damu na angalieni mfano mzuri wale waliwahi kufaidi utawala wa sultani leo wanautamani ungelibakia ule ule na si huu wa gozi,manjo,kisima ambacho tumetumbukia hatupaoni pa kutokea.




  2. santorini 19/11/2012 kwa 12:47 um · Ingia kujibu
    Mapinduzi yametugubika unyonge ndani ya taifa letu na baya zaidi si tu kugubikwa wazanzibari wenyewe lakini pamoja na taifa letu limeshatumbukizwa mnadani linanadiwa bila idhini yetu wazanzibari.
    Jee huu si unyonge mkubwa tena unashinda unyonge ule wa wakati wa sultani,tunapigwa ,tunavunjiwa nyumba zetu ,tunabughudhiwa ,tunanajisiwa,tunafungwa,tunanyanganywa mali zetu kisha yadumu mapinduzi ,yadumuke juu chini.




  3. fey 19/11/2012 kwa 1:35 um · Ingia kujibu
    Siku inayofaa kusherehekewa ni hayo dec. 10 kwani ndio time pasta uhuru wetu kutoka kwa mkoloni. Na hiyo ya 12 jan. wanayoifahamu wao ni Kua wanajua siri ya hayo mapindizi.
    Hakuna Sultani alopinduliwa siku hiyo, waliopinduliwa na wazanzibar wenye asili ya kiarabu na hao asili yao ilikuwepo kabla ya hata huo utawala.
    Hizi ni pinu za Nyerere kutaka kututawala waZanzibar ndio akatia chuki za uarabu na uafrica, lakini kilikua kinamuuma ni uislamu na akathubutu kuleta jeshi na ni jeshi la bara lilotumika , halafu Hawa vibaraka vyake wanajua nini wanakisherehekewa na ndio maana wakaificha ile dec, na kuwadanganya watu kua haikua uhuru kamili hadi pale tulipopindua ( wanafik) nawawadanganye hao hao kina Bora afya na Baraka Shamte vichwa maji na ubongo sheli sheli
    Na pia wakaona haitosha, Laanatullah Nyerere alikua akitolesha vitabu vya uongo kuhusu Mapinduzi hayo na kutusomesha maskulini.
    Kwa kifupi hiyo siku sio yetu sisi waZanzibar, kwani nini wasisherehekee huko kwao Tanganyika na wao ndio waliopindua na kuuwa waZanzibar? Na kama sio hivyo ilikwendaje wakakubali kujiita chama cha mapinduzi na hawana history hiyo katika nchi yao? Lazima kuna siri nzito!




  4. dk.m 19/11/2012 kwa 1:37 um · Ingia kujibu
    Upumbavu ulioje tunasherehekea siku hata zisizo tuhusu tukaiacha siku yetu adhimu. Eti siku ya mfanyakazi duniani wakati huo huo kazi zenyewe hamna. Eti unasherehekea siku ya mkuli, wakati mkulima ndiyo mtu aliyefanywa duni ktk nchi hii. Na mbaya zaidi ni kusherehekea siku hii ambayo ilisababisha maelefu ya mababu na mabibi zetu kupoteza heshima, utu na thamani zao, kupoteza makazi na mali zao, na wengine kupoteza uzima na roho zao. Nayo ni siku hiyo ya mapinduzi.
    Ipo siku “hakika baada ya dhiki, faraja”




  5. Hamid Aboud 19/11/2012 kwa 1:37 um · Ingia kujibu
    hakuna haja ya kusheherekea uhuru bado tumetawaliwa.




  6. Hemed Said 19/11/2012 kwa 1:47 um · Ingia kujibu
    Mimi naunga mkono kusherehekea siku ya Uhuru wa Wazanzibari na tuwache kusherehekea siku ya mapinduzi, kwani Wazanzibar ndio waliyopinduliwa na kuuliwa ovyo hususani mashamba.




  7. alfola 19/11/2012 kwa 2:12 um · Ingia kujibu
    TAnganyika si wanasheherekea Uhuru wao 09dec, kwa nini -Zanzibar iwe dhambi?




  8. Mohammed Ali Omar 19/11/2012 kwa 2:15 um · Ingia kujibu
    uhuru bado hasa hatujaupata tunatangatanga tu.uko wapi uhuru mie siuoni labda uhuru wa kuzurura vichichoroni njaa kali kila siku saumu.

    Wazanzibar hawahitaji matumizi ya nguvu kutawaliwa kwa , Muungano ni hiari sio kulazimichana au kuchuritichana.
    Kutimia miaka miwili tokea kundwa kwa Serekali ya Umoja wa Kitaifa wa wazanzibar
    Bonyeza Sauti
    AUDIO | DW.DE

 
Back
Top Bottom