Utafiti uliofanywa na taasisi ya World Data Lab umeitaja Tanzania kuwa nchi ya sita katika orodha ya nchi ambazo watu wake wanaishi kwenye umaskini uliopindukia (extreme poverty). Lakini wiki iliyopita serikali ilitangaza kuuza hatifungani (bond) ya miaka 25 ambayo ilikuwa inalipa kiwango cha riba (interest rate) cha 12.75%.
Serikali ilitaka kupata bilioni 289 katika mnada huo. Lakini waliojitokeza kwenye mnada huo waliweka jumla ya shilingi trilioni 2.1 kununua hati fungani hizo. Kwa kifupi ni kwamba serikali ilitaka bilioni 289, lakini wanunuzi walikuwa na mzigo wa zaidi ya trilioni 2 na bilioni 100.
Kwa nchi ambayo mifumo yake ya fedha ina "fairness" na ipo "harmonized" haikutegemewa kuwe na kundi la watu ambao wapo tayari kununua hatifungani za serikali kwa pesa nyingi, halafu ndani ya nchi hiyohiyo kuna kundi kubwa la watu waishi katika ufukara.
Kiuchumi hii ni economic paradox. Tafsiri yake ni kwamba kuna kundi dogo la watu limeshika uchumi. Hilo kundi ndilo lenye uwezo wa ku-bid trilioni 2 kwenye mnada wa bilioni 200 tu. Kwa kifupi ni kwamba gap kati ya mwenye nacho na asiye nacho linazidi kuongezeka.
Ukisoma kitabu cha Undercover Economics cha James Brown na Charles Coffin Little, kinaeleza kuwa moja kati ya factors zinazosababisha kwenye nchi moja baadhi ya watu kuwa na pesa nyingi huku wengi wakiwa mafukara ni kushamiri kwa ufisadi, biashara haramu, dili feki, na kukosekana kwa uwazi katika mifumo ya fedha. Je waliyoeleza Little na Brown yanasadifu hali ya Tanzania? Kama sivyo, je nini kinasababisha kundi dogo la watu kuwa na fedha nyingi huku wengi wakiishi kwenye ufukara?