Uhuni huu wa TANAPA mpaka lini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuni huu wa TANAPA mpaka lini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mku, Apr 28, 2011.

 1. mku

  mku Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  WATUMISHI 181 wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), wameajiriwa kinyume cha taratibu za ajira. Ajira hizo zisizofuata taratibu ndani ya shirika hilo, zimebaInika wakati wa ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
  Kwa mujibu wa Utouh, Tanapa ni mfano wa mashirika mbalimbali ya umma yanayotoa ajira za watumishi kwenye sekta mbalimbali kinyume cha taratibu. Utouh anabainisha kwenye uchambuzi wa usimamizi wa raslimali watu katika mashirika mbalimbali ya umma, kuna mashirika ambayo ajira za kazi zilifanywa bila kufuata taratibu za uwazi. Anabainisha taratibu hizo zinazokiukwa na mashirika hayo wakati wa ajira kuwa, ni kutangaza nafasi zilizo wazi, jambo ambalo linawanyima watu wengi nafasi ya kushindana. "Mfano mzuri ulibainika Tanapa ambapo menejimenti ilitangaza nafasi 19 za kazi kuwa uwazi, lakini kufikia mwisho mwa zoezi la uajiri, wafanyakazi 32 zaidi waliajiriwa; "Uchambuzi zaidi ulibaini kuwa wafanyakazi walioajiriwa na Tanapa mwaka huu wa ukaguzi bila nafasi zake kutangazwa ni 181" anasema Utouh.


  SOURCE: MWANANCHI


  Napata sana wakati mgumu wa kujua ni nini hasa kilicho pale Tanapa maana hizi habari ziko mtaani siku nyingi na hakuna wala anayewajibishwa. Na hii najua ingawa angalau imepata kuibuliwa kwenye media sina hakika kama kutakuwa na uwajibikaji wa wahusika. Ni jambo la kusikitisha na kushangaza hasa tunapowaona wahitimu wa uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori pale SUA na UD vijana wanaishia kufundisha na wengine kuajiliwa kama mabenki teller huku wale wasiokuwa na sifa hizo wanapewa nafasi kinyemela. Kuna kipindi TANAPA walikuwa wanaajiri wahitimu kutoka MWEKA tu na kuwapa mgongo wale waliohitimu SUA na UD, Hii issue alishaipigia kelele Beatrice Shelukindo bungeni ila kwa sababu zao naona waliziba masikio na yeye kwa sababu zake naona akapiga kimya....sasa swali la kujiuliza ni kwanini tupoteze rasilimali nyingi sana za kuwasomesha wataalamu kwa fani tunazozitaka na mwishowe hizo fani zinaishia kwenye KABURI la sahau kwa kuwapa watu wasiostahiki hizo nafasi? Nawasilisha
   
Loading...