Uholanzi: Familia iliyokuwa ikisubiri 'mwisho wa dunia' kwa miaka tisa yapatikana ikiishi chini ya ardhi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
n9Axxu_1.jpg

Polisi nchini Uholanzi imegundua chumba cha siri cha chini ya ardhi kilichokuwa kikitumika na familia moja kwa zaidi ya miaka tisa.

Taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari ilisema kuwa chumba hicho kimegunduliwa jana Jumanne Oktoba 15 na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, familia hiyo ilikuwa ikiishi chini ya ardhi kwa kile walichodai kuwa ilikuwa ikisubiri siku ya mwisho wa dunia.

Shirika la Utangazaji la BBC, liliandika kuwa mwanaume wa miaka 58 na watoto wake sita walio na umri kati ya miaka 16 hadi 25 walikuwa wakiishi katika chumba hicho kilichopo katika shamba lao katika lililopo katika Mkoa wa Kaskazini wa Drenthe.

“Walipatikana baada ya kijana wake mkubwa kuenda kununua pombe katika baa moja karibu na kijiji cha Ruinerwold na kumfahamisha mhudumu wa kwamba anataka usaidizi,” kituo cha Televisheni cha RTV kiliripoti.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa muhudumu huyo alimuona kijana huyo kama amechanganyikiwa na kupuuza ombi hilo mpaka pale alipotokea mwanakijiji mwingine na kumsikiliza kwa umakini.

"Aliagiza chupa tano za bia na kunywa zote. Baada ya hapo nilizungumza nae kidogo ndipo alipofichua kuwa ametoroka na kwamba anaomba usaidizi. tukapiga simu polisi," mmiliki wa baa hiyo Chris Westerbeek alikifahamisha kituo cha RTV.

Aliongeza kuwa, “alikuwa na nywele ndefu, ndevu chafu, nguo zilizochakaa na alionekana kana kwamba amechanganyikiwa. Alisema hajawahi kwenda shule na kunyolewa nywele kwa miaka tisa.

"Alisema ana ndugu na dada zake ambao wanaishi katika shamba hilo. Pia alisema anataka kukomesha jinsi familia yake inavyoishi."

Wakizungumza na waandishi wa habari majarani wa familia hiyo walisema wanaamini watu hao walikuwa wkaiishi kula mboga za Majani pekee ambazoi zimepandwa katika shamba hilo.

Maafisa wa polisi waliootembelea makazi hayo ili kufanya upekuzi zaidi waligundua ngazi iliokuwa nyuma ya kabati katika sebule ya nyumba hiyo ambayo inaelekea chumba hicho chini ya ardhi ambako familia hiyo ilikuwa ikiishi.

Ruinerwold ni kijiji kilicho na wakazi chini ya 3,000. Shamba hilo lipo nje kidogo ya kijiji hicho ana inaweza kufikiwa tu kupitia daraja lililoko juu ya mfereji.

Shamba hilo ambalo kwa upande mmoja limefichwa na miti mingi pia limepandwa mboga nyingi.

Jirani mwingiune aliviambia vyombo vya habari vya Uholanzi kuwa alimuona mtu huyo peke yake na kwa alifikiria hana watoto.

Chanzo: Mwananchi
 
Akili za wazazi wengine zinawafanya watoto waishi kwa mateso makubwa. Sasa ndo nini
 
nimependa hayo mazingira nataka ninunue shamba nitengeneze mji wangu wenye mazingira ya kuvutia kama hayo
 
Kwahiyo kujificha chini ndio alikuwa anaukwepa au anausubiria ukija utapitia chini kuja juu?kuna haja ya kujua dini au Imani wanayoiabudu...
 
Back
Top Bottom