Uharibifu huu Uwanja wa Taifa haukubaliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uharibifu huu Uwanja wa Taifa haukubaliki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 11, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  JumapiliI iliyopita, baadhi ya mashabiki waliokosa ustaarabu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam walichomoa viti 152 na kuvunja 11 kati ya hivyo katika kile kilichodhaniwa kuwa ni matokeo ya utani wa mashabiki wa klabu za Simba na Yanga.

  Tukio hilo la kusikitisha lilitokea wakati wa mapumziko wa mechi ya marudiano ya hatua za awali za Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu ambapo wenyeji walishinda 2-1 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.
  Kufuatia uharibifu huo, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo ndiyo inayosimamia uwanja huo, ilitoa

  taarifa kuwa hasara ya Sh. milioni 5 ilipatikana kutokana na kadhia hiyo na kwamba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliandikiwa barua ya kutakiwa kulipa gharama zilizotokana na uharibifu huo.
  Siku chache baadaye, TFF ikachukua hatua ya kukata mapato ya Simba ya mechi yao ya Jumatano ya Ligi Kuu ya Bara dhidi ya

  Kagera Sugar ili kufidia hasara ya uharibifu wa viti.
  Hata hivyo, hatua hiyo imeibua mgogoro baina ya Simba na TFF. Viongozi wa klabu ya Simba wanapinga kukatwa fedha za kulipia uharibifu ambao wanadai kwamba hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuwa ulisababishwa na mashabiki wa timu yao; hasa kutokana na

  ukweli kwamba walishakatwa Sh. milioni 25 za kulipia ulinzi na usalama uwanjani hapo lakini hadi sasa hakuna yeyote aliyekamatwa kwa kuhusika na tukio hilo na kubainika kuwa ni mwanachama wao.
  Si nia yetu kuzungumzia mgogoro huo wa nanianayepaswa kulipa gharama za uharibifu uliofanywa na mashabiki katika mechi baina ya

  wenyeji Simba dhidi ya Kiyovu. Bali, tunadhani kwamba sasa ni wakati muafaka wa kukomesha vitendo vya aina hiyo. Mashabiki wa soka wanapaswa kutambua kuwa Uwanja wa Taifa ni mali yao na kwamba, gharama zozote zinazojitokeza kutokana na kuharibika kwake huathiri mapato ya Serikali, ambayo kimsingi hutokana na kodi zinazolipwa na Watanzania wote kupitia njia mbalimbali.

  Kwa sababu hiyo, tunadhani kwamba mashabiki wote wanapaswa kujua kuwa wanaposababisha uharibifu kwenye uwanja huo uliojengwa kwa mabilioni ya pesa, au kushuhudia wengine wakiharibu miundombinu ya uwanja huo na kutochukua hatua za kuwadhibiti, hawana wanayemkomoa isipokuwa ni wao wenyewe.

  Isitoshe, mechi moja kama ya Simba dhidi ya Kiyovu haimaanishi kwamba uwanja huo hautatumika tena katika mechi nyingine ambazo bila shaka, na wao watakuwa na fursa ya kwenda kuzishuhudia. Kuruhusu uharibifu maana yake ni kwamba siku nyingine, kuna uwezekano wa kuathirika kwa kukosa viti na kusimama uwanjani hapo.

  Kwa ujumla, madhara ya uharibifu huo kwa Watanzania wote, hasa mashabiki wa soka, ni makubwa na yanajulikana wazi.
  Kila mmoja anapaswa kuwa askari wa kulinda miundombinu ya uwanja huo wa kisasa ili udumu kwa muda mrefu na kuwafaidisha Watanzania wote badala ya kubadilika na kuwa gofu katika kipindi kifupi kijacho.

  Tunashauri kwamba Serikali, TFF, klabu na wadau wengine wote kushirikiana katika kukomesha vitendo vingine vyovyote vyenye ishara ya kuharibu uwanja huo.

  Ni wakati muafaka sasa kwa vyombo vya usalama kushirikishwa kwa karibu ili kubaini waharibifu na kuwachukulia hatua kali za kisheria. Kama hiyo haitoshi, elimu iendelee kutolewa kwa mashabiki juu ya umuhimu wa kupokea matokeo yoyote yale kiustaarabu, kwani kufanya vurugu na kuharibu miundombijnu ya uwanja kutokana na furaha ya kushinda au hasira za kufungwa ni dalili wazi ya kukosa uungwana.

  Isitoshe, mashabiki wanapaswa kujua kuwa vurugu zozote uwanjani, kama zile zilizosababisha uharibifu wa viti vya uwanja huweza kusababaisha adhabu kali kwa timu mwenyeji, ikiwemo ya kufutiwa matokeo, kutakiwa kucheza bila mashabiki na hata kufungiwa.

  Adhabu ya kucheza bila mashabiki wanayoitumikia sasa Zamalek ya Misri ilitokana na vurugu zilizofanywa na mashabiki wao msimu uliopita katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Club Africaine ya Tunisia. Mashabiki wa Simba, Yanga, Azam, Mtibwa

  na timu nyingine zote wanapaswa kuelimishwa kuwa juu ya hatari hii.
  Kwa pamoja, sote tunapaswa kusema kuwa sasa inatosha. Uharibifu kama uliotokea juzi kwenye Uwanja wa Taifa haukubaliki na hivyo ni lazima ukomeshwe.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tumlaani Ismael Rage kwa kushabikia uharibifu wa viti
  QUOTE=MziziMkavu;3477836]JumapiliI iliyopita, baadhi ya mashabiki waliokosa ustaarabu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam walichomoa viti 152 na kuvunja 11 kati ya hivyo katika kile kilichodhaniwa kuwa ni matokeo ya utani wa mashabiki wa klabu za Simba na Yanga.

  CHANZO: NIPASHE[/QUOTE]
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wana jf tumlaan Ismael Rage kwa kushabikia uharibifu uwanja wa taifa
   
Loading...