Uharamia wa CCM: Mbunge Highness Kiwia afanyiwa operesheni masaa 6

Nadhani mleta mada na baadhi ya wachangiaji humu hawaelewi na hawana ufahamu kwa wanayoyaongea.
Ni kweli Mh Kiwia alivamiwa na kuumizwa. Kwa binadamu yoyote mwenye hofu ya Mungu,hilo ni jambo baya na linapaswa kulaaniwa bila kujali lilitekelezwa na nani.
Imani yangu, na naamini wengi hamjui ni kwamba si Mh Kiwia, wala chama chake cha CHADEMA, wala mashahabiki wa Chadema au ninyi washadadiaji aliyetoa hata senti tano nyekundu kwa safari yote ya Mh Kiwia tena na msindikizaji wake kutibiwa India.
Hiyo serikali mnayoishutumu na kuitukana utadhani mmezaliwa na wazazi mabazazi wakati wazazi wenu ni watu wema na wenye heshima tu,ndiyo imegharamia na inaendelea kugharamia safari na matibabu yote ya Mh Kiwia.
Hivi hiyo serikali pamoja na kuinyonga kwote kwa nini wakati mwingine msiipe haki ya kuishukuru pale inapobidi? ?

Mkuu nnaomba tuende sawa ,ni kama unafurahia kwa sababu Serikali ina pesa basi iwaue na kuwajeruhi wananchi wake kwa sababu ina pesa za kuwagharamia ,wanacholaumu wachangiaji hapa ni kuwa hakuna hatua zozote kali zilizochukuliwa dhidi ya wale waliomshambulia mbunge huyo kutoka Chadema pia hakuna hatua zozote kali zilizochukuliwa dhidi ya askari waliokuwa eneo la tukio na waliacha kulizuia wakati uwezo walikuwa nao wa kufanya hivyo.Sasa ni nini maana ya usalama wa raia na mali zake?.Uwajibikaji nchi hii hakuna tena ,wapinzani na raia masikini hawana tena haki na wakiitaka wanatakiwa kuinunua.
 
Bahati mbaya sana haya manyang'au ndo wanatawala nchi, halafu umoja wa mataifa upo kimya tu raia wanateswa na serikali!
 
Eti CHADEMA wanadai uharamia wa CCM.

Yaani CCM imfanyie uharamia, halafu hiyo hiyo CCM kupitia serikali yake impeleke India kupata matibabu.

Hajatoa hata senti moja kutoka mfukoni mwake kwa ajili ya matibabu. Pesa yote inalipwa na serikali ya CCM ambayo mnadai imemfanyia uharamia.

CHADEMA wanashangaza sana.

Propaganda zimewashinda, kwa sasa mmebakiwa na vioja.

Cha muhimu ni mbunge Kiwia kupata matibabu ili arudi mapema kuwatumikia wananchi wake.
 
Haki huinua taifa bali dhambi nia aibu ya wote. Ukatili wowote unaofanywa na dola, ama dola yenyewe ambayo imeapa na kupewa jukumu la kulinda haki za raia, au kwa dola kupuuzia haki za watu ilizoapa kuzilinda; mwisho wa siku aibu na mzigo wa dhambi hulilemea Taifa zima na hatimaye Taifa huanguka.

Vv
 
Mkuu nnaomba tuende sawa ,ni kama unafurahia kwa sababu Serikali ina pesa basi iwaue na kuwajeruhi wananchi wake kwa sababu ina pesa za kuwagharamia ,wanacholaumu wachangiaji hapa ni kuwa hakuna hatua zozote kali zilizochukuliwa dhidi ya wale waliomshambulia mbunge huyo kutoka Chadema pia hakuna hatua zozote kali zilizochukuliwa dhidi ya askari waliokuwa eneo la tukio na waliacha kulizuia wakati uwezo walikuwa nao wa kufanya hivyo.Sasa ni nini maana ya usalama wa raia na mali zake?.Uwajibikaji nchi hii hakuna tena ,wapinzani na raia masikini hawana tena haki na wakiitaka wanatakiwa kuinunua.

Nakushukuru sana.
Kwanza unaonyesha ni mwelewa na muungwana na siyo kama hawa vijana watumwa wa siasa ambao kwao wanachokijua ni matusi.
I hate them irrespective of being opposition or ruling part followers.
Kilichopo kwa Mh Kiwia,kama anaona haki inacheleweshwa kwa kutumia jeshi la Polisi, there are always alternatives. ie private prosecution.
Kwa mtu mbunge kama Kiwia, usiniambie haiwezekani.
Tatizo hapa ni ignorance, kwa mashabiki wa Kiwia na huenda kwa Kiwia mwenyewe.
Polisi wanasema, investigation on the matter is still underway. ... Kiwia anasema, all evidences against the curprits are vivid. ....why doesnt he go for the alternatives? ???
Anyway, get well soon Mh Kiwia.
Taifa linakuhitaji, chama chako Chadema japo kina wahuni na wavuta bhangi wengi kinakuhitaji, Ilemela kwa wastaarabu wanakuhitaji, na familia yako pia wanakuhitaji.
 
Pole sana Kamanda. Mungu akupe uhai na kupona kabisa. Aibu magamba nyie.
 
Sipati picha siku tukiwa na silaha...... Nimejisemea tu
 
Bahati mbaya sana haya manyang'au ndo wanatawala nchi, halafu umoja wa mataifa upo kimya tu raia wanateswa na serikali!

Madini/gesi/ wanyama wetu vyote tumeshawapatia ,hata hawa mawakala wao wakituua sisi raia hutasikia lolote mkuu.
 
slaa alivyo anguka bafuni na yeye mpeleke apolo pia msimsahau lema kurekebishwa tigo network tangu avumbuliwe
Hivi wazazi wako wanaposoma uliyoyaandika humu wanajisikiaje ? NATANGAZA KUKUDHARAU RASMI NA MOJA KWA MOJA KUANZIA LEO HADI PALE UTAKAPOKUFA , UMEUTIA AIBU UKOO WAKO WOTE .
 
Hansard inaonyesha kwamba pamoja na polisi kusimamia mauaji hayo pia ametajwa mbunge wa viti maalum MARIA HEWA kuwa nyuma ya mpango huo , mwisho wa kunukuu .
 
Back
Top Bottom