UHANITHI baada ya Kitovu cha Mtoto kukatika na kudondokea Sehemu zake za Siri

tumetoka kujadil hapa,na tumekubaliana tusimfunge,mwanangu ana siku kama 5 tangu azaliwe.Wanasema hospital wanafunga wenyewe now days
 
zamani wazazi waliambiwa kuwa kitovu kikidondokea kwenye sehemu za uzazi itasababisha uhanithi kuwatisha kinamama ili wawe waangalifu na kidonda cha mtoto mchanga kitovuni, wasisahau kukiangalia na maendeleo yake kuepusha vifo vya infection, lakini hakuna uhusiano

Wazee walishakuwa intelligent toka kitambo
 
Naomba jibu je ni kweli kitovu cha mtoto wa kiume kikidondokea uume kina madhara yaaani kinaweza kumsababishia hasizae na kuwa na uume mlegevu?
 
Hizo ni mila tu hakuna scientific evidence. na wamama wanaamini hiyo kitu balaa.eti mpaka alale na mama yake mzazi ndio inakubali.
 
Je! Huwa inatokea kweli ama haitokei kabisa ama imekaa vipi hii japo kisayansi hakuna ki2 kama hcho
Japo kisayansi tunaambiwa hakuna kitu kama hicho, wazazi wengi wanapopata watoto wa kiume wanakuwa makini sana na kitovu kutomdondokea mtoto kinapoanguka kutokana na imani iliyopo, kwa hiyo labda apatikane mzazi ambaye mtoto wake alidondokewa na kitovu atupe mrejesho ilikuwaje.
 
Kama unaona inakusumbua au ki mila iko hivyo kwenu ongea na wazee wakuambie wanafanyaga nini, bali pia usiache kusali na muombe Mungu azuie kitu hicho afute fute yote yalio katika mila yenu. Kuwa na imani ametenda hivyo na acha kuifikiria mtoto atakua salama tu. Mungu ndie awezaye yote duniani.

Mie ndio najua hii kitu inasemwa kwa kusoma ulichoandika. Kisayansi kama walivyosema wengine hakuna hiyo.
 
Hakuna ukweli wowote, mimi naamini walisema hivo ili tu mama awe na uangalizi mzuri kabla kitovu hakijatoka maana katika wakati huo mama asipokuwa makini ni rahisi mtoto kupata maambukizi. hakina madhara hata kingekatika na kukaa siku mbili kama mtoto ni rijali atabaki kuwa rijali.

Ndivyo nilivyofundishwa clinic, ndio maana tunaita ni mila potofu.
 
Asanteh sana wanajf kwa kunitoa wasiwasi na msaada wenu juu ya jambo ili nimefanya kupitia naona asilimia kubwa wamekataa kuwa jambo ili si la ukweli
 
Imani huzaa sheria bila shuruti!
Hii ndio imeishakuwa sheria ki_aina, na haina budi kufuatwa.
 
Hizi biti za mibibi na mababu zinasaidia sana

watu wanadharau tu, wale mabibi wana PhD zao za kuzaliwa! wee si umefundishwa kuwa ni mwiko kabisa kwa mtoto wa kike kutoosha MWIKO baada ya kusonga ugali? mungu awape maisha marefu mabibi ote ambao bado mnadunda!
 
watu wanadharau tu, wale mabibi wana PhD zao za kuzaliwa! wee si umefundishwa kuwa ni mwiko kabisa kwa mtoto wa kike kutoosha MWIKO baada ya kusonga ugali? mungu awape maisha marefu mabibi ote ambao bado mnadunda!
 mie pia umenijumuisha kwa mabibi wanaodunda au? :(:(:(
 
Back
Top Bottom