Nivea
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 7,459
- 4,748
nimeamini hiliKwa kuanzia....Imani hii si ya kweli, japo nachelea kuiita potofu (kiSwahili kigumu sometimes). Siiti potofu kwa sababu haina hasara kwa mtoto, bali ina faida!
Dhana hii ilianza zamani za mabibi zetu walipogundua kuwa kama hutunzi vyema kitovu cha mtoto mchanga basi mtoto huyo ataugua na kufariki. Na hilo ni kweli, kwani mtoto atapata 'umbilical infection/sepsis' na kama hatapata matibabu ya haraka na stahiki atafariki kwa 'septicaemia'.
Kwa hiyo imani hiyo ilitungwa ili wamama wawe makini kuchunga kitovu kisiangukie uume mtoto akawa h*nithi, wakati huo huo mama atachunga kitovu kisipate maambukizi. Hivyo japo si kweli kwamba mtoto akiangukiwa kitovu anakuwa h*nithi, lakini uongo huo una faida kwa mtoto kuangaliwa vyema kitovu chake.