UHANITHI baada ya Kitovu cha Mtoto kukatika na kudondokea Sehemu zake za Siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UHANITHI baada ya Kitovu cha Mtoto kukatika na kudondokea Sehemu zake za Siri

Discussion in 'JF Doctor' started by Kipanga, May 20, 2008.

 1. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wandugu,

  Napenda kufahamu kitaalamu juu ya imani au uvumi kuwa mtoto mchanga anapozaliwa lazima mzazi na hasa mama ahakikishe kuwa kitovu cha mtoto huyo kitakapokauka na kudondoka basi kisiguse sehemu nyeti za huyo mtoto. Inasemekana kuwa ikitokea kuwa kitovu hicho kimedondoka na kugusa sehemu hizo nyeti basi mtoto huyo kama ni wa kiume atakuwa bwabwa na kama ni wa kike nae atakuwa msagaji? (hatakuwa na feeling za kuhitaji mwanaume)..

  Nahitaji maelezo ya kitaalamu na hasa kwenu nyie wataalamu wa tiba kuhusu hili kwani yanazungumzwa lakini hakuna justification ya kitaalamu inayotolewa zaidi ya kuonekana ni mapokeo ya imani tu.

   
 2. m

  mgirima Member

  #2
  May 24, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inadaiwa kuwa kitovu cha mtoto aliyezaliwa huwa kinaandamana na mikosi na mabalaa mengi kutoka kwa mama. na ndio maana hutakiwa kuzikwa ardhini (kwa kiasili) na sio kutupa sehemu yoyote. Maelezo haya hayana utaalamu wo wote ila ni mambo ya kimila tu. ajabu ni kuwa makabila mengi hapa nchini yanaamini hivyo!
   
 3. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kitaalamu hilo suala la kitovu kinapoangua na kugusa sehemu nyeti za mtoto na kumfanya awe hanidhi si ukweli. Mie nahisi ni mila za baadhi ya makabila.

  Kitaalam mtoto kila anapokuwa katika kipindi fulani basi kuna mambo lazima atapitia,sasa mzazi ambaye atamkataza huyu mtoto kufanya haya mambo yanaweza kumuathiri kisaikologia.

  Mfano watoto wengi katika umri fulani huwa wanacheza kama vile wazazi katika familia, mtoto wa kiume baba na mtoto wa kike ni mama, so hawatakiwi kukatazwa, kwani ni mambo ya kupitia na baadae wataacha.

  Pia kuna umri fulani watoto huwa wanajisaidia haja kubwa au ndogo pasipo kujielewa. Mzazi hautakiwi kumpiga na kumtisha mtoto, kwasababu hiyo ni hali kutokana na kutokomaa kwa mfumo wake wa fahamu. Pindi mzazi utapokuwa unampiga na kumtishia ili aache hiyo tabia, ni kweli ataacha ila yaweza kuwa ikamuathiri ukubwani.
   
 4. H

  Haika JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  zamani wazazi waliambiwa kuwa kitovu kikidondokea kwenye sehemu za uzazi itasababisha uhanithi kuwatisha kinamama ili wawe waangalifu na kidonda cha mtoto mchanga kitovuni, wasisahau kukiangalia na maendeleo yake kuepusha vifo vya infection, lakini hakuna uhusiano
   
 5. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii nilipata kuisikia siku nyingi kidogo ya kwamba kama mtoto mdogo ataangukiwa na kitovu(Kile kijipande cha nyama kinachodondoka baada ya kitovu kukauka na kupona siku kadhaa baada ya mtoto kuzaliwa),sasa hicho kijipande kikimuangukia sehemu zake za siri,basi kama mtoto huyo ni wa kiume hatoweza kuattain erection maisha yake yote.

  Huyu aliyeniambia akazidi kusema,ndo mana wakina mama uwa makini sana vitovu hivi,vinadondokea wapi?Mnaoshinda mawodini na mahospitalini tuambieni,jee hii ni kweli na kama ni kweli what is the mechanism behind.
   
 6. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  baba watatu
  ...Bora Baba watatu umeweka hii thread hapa tunaweza kupata ufumbuzi wa kitaalam kuhusu hiyo mi naiita imani au mtazamo wa mashaka. Niliwahi kuichomeka thread inayohusiana na hili jambo lakini kwa mshangao ikayeyuka.....Haya matabibu mtujuze kuna connection gani kati ya kuangukia kitovu sehemu ya siri ya mtoto na uhanithi.

  Baba watatu, wengine hudai hata kwa mtoto wa kike pia ikimtokea anapokuja kupevuka hatakuwa na msisimko wa mapenzi???
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. M

  Mwanafunzi Member

  #7
  Sep 10, 2008
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo la kujiuliza Baba watatu na Kipanga ni Je kuna mtu mzima aliyekuwa na matatizo ( kutopata erection au kutokuwa na msisimko) ambaye alisema nilipokuwa mtoto kitovu kiliangukia sehemu za siri?

  Kwa jamii yetu ninavyoielewa, mtu hawezi kusema matatizo yake au kwenda kuuliza mama kuwa nilipokuwa mdogo kitovu kiliangukia wapi. Pia jinsi akina mama kwa imani wanavyo protect hicho kitovu kisiangukie pabaya, ni ajabu kuwa watu wengi wana hayo matatizo.

  Je, wote hao vitovu viliangukia pale??
   
 8. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwanafunzi ...Ndio maana tulitaka wataalamu wa tiba watujuze kwani imeshakuwa mazoea kuwa mtu akishindwa ku-erect inaaminika aliangukiwa na kitovu sasa mimi binafsi nashindwa kuelewa kitovu kina nini mpaka kiathiri erection ya mtu ingawa kiukweli erection inaendana sana na jinsi brain inavyosense kile kitendo kinachotegemewa kufanyika (mapenzi/sex)

  Unajua hata wakati mtoto wangu wa pili anazaliwa bibi yake mzaa mimi alimfatilia sana huyo mtoto hadi alipohakikisha kitovu kimekauka na kimedondokea maeneo aliyoita mwenyewe salama....Mi nilikuwa mtazamaji tu kwani si mama wala bibi wa mtoto aliyekuwa tayari kunielezea nini kinachoendelea.....WANA JF hebu tutoeni tongo tongo basi....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Nimepata kusikia huko uswahilini kuwa, eti mtoto wa kiume akidondokewa na kitovu chake ndo basi tena. Yaani jogoo halitapanda mlima. Mimi sioni uhusiano wa kisayansi hapo. Je kuna ye yote ajuaye anisaidie/atusaidie kupata ukweli wa jambo hili?
   
 10. m

  macinkus JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2009
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kitovu kudondoka ndio kufanya nini wandugu

  macinkus
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Hata mimi niliposikia nikakosa jibu,lakini ni jambo la kawaida mitaani kusikika hasa huku Pwani.
   
 12. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kituvo kikidondokea uume kwa mtoto mchanga, basi jogoo hilo litakuwa haliwiki na kama litawika basi litakuwa na walakini. Hizo ni imani za kale
   
 13. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sehemu nyingi tu wanaamini hivyo. Ni kweli kabisa. Kitovu kikiangukia uume wa mtoto mchanga wakati kinapokatika mara baada ya mtoto kuzaliwa mtoto hukua bila nguvu za kiume. Ndo maana wamama huwa wako makini sana na watoto wao. Yaani ndo basi tena, jogoo hatapanda mtungi. Sababu zenyewe ni za kisaikolojia zaidi. Mtoto anakuwa affected kitovu kikigonga uume kinapokatika.
   
 14. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Hii hadithi imakuwa ikisimuliwa for ages, especially kwa wanawake. Na hata pale unapotoka kujifungua nurses wanakwambia namna ya kuangalia kitovu cha mtoto, kusafisha mpaka kikauke, na hapo ndipo wanakwambia kwamba uwe makini kitovu kisidondoke kwenye uume wa mtoto. Sasa hili ni la ki-medical au ki-imani?
   
 15. a

  agika JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mhhhh mwenzangu hata mimi nilipojifungua mwanangu niliambiwa hivyohivyo, ila bwana i culdnt dare kubisha, nikasema hata kama siamini sitaki mwanangu awe ndo test na ukizingatia psychology ya mama anapotoka tu kujifungua akili yote inakuwa kwa mtoto na hutaki baya lolote litokee juu yake,basi nilikuwa nawatch kile kitovu kama nini sijui, kilikatika siku ya saba ndio nikaanza hata kulala usingizi, nadhani ni imani tu ila mama akiambiwa hivyo huwa anaamini kwa wakati ule, nani anyetaka mtoto wake asiwe rijali? akamletea mkwe na vijukulu jamani?
   
 16. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mimi nilisikia kitovu kikimdondokea mtoto wakike kwenye sehemu zake za siri atakuwa anajikojolea mpaka ukubwani sasa sijui kweli.
   
 17. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Anecdote!
   
 18. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  ni kweli ni vigumu kudharau suala hili, hata my wife wangu alipata shida sana kwani alielekezwa hivyo pale Mhimbili, na hatukudhubutu kufikiria kudharau kwani suala lenyewe linagusa mahali pabaya sana (kama Rais Mstaafu Mzee Mwinyi alivyokuwa akisema).
   
 19. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hii ni mila ya siku nyingi sana, na imerithishwa kizazi hadi kizazi.

  Madhumuni haswa ya kina mama kuambiwa hivyo, ni kuwataka wawe makini sana na kidonda kilichopo hapo (Kitovuni), kwani wakifanya mchezo na kidonda kikipata athali yoyote (Bacteria na Vijidudu vya Pepo punda), Mama anaweza kumkosa mtoto wake.

  Ili wazazi (wakina mama) wawe makini na kumuangalia mtoto, ndio ikaja dhana hiyo ya Kitovu cha mtoto kiangaliwe sana ili kisije kumuangukia mtoto na kuwa na matatizo hayo yaliyo tajwa, na hii ni kuwa tunazingatia sana urijali na kuendeleza familia zetu.
   
 20. M

  Malila JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Naweza kukubaliana na wewe,yaani wana-draw attention ya wazazi juu ya kidonda. Kitovu kinapodondoka hakina tena communication na sehemu nyingine ya mwili,kwanza huwa kimekufa,sasa taarifa toka kwenye kitovu mfu kwenda kwenye mwili hai ni ngumu kidogo. Kateni nondo tuendelee kufaidi.
   
Loading...