UHANITHI baada ya Kitovu cha Mtoto kukatika na kudondokea Sehemu zake za Siri

Imani ni ngumu sana kuthibitisha kwa njia za kawaida za ufahamu.
Ili kujua kitovu kina madhara hayo, wajitokeze watu ambao wapo tayari kujitolea watoto wao kuwa sehemu ya utafiti huo ili kuondoa sintofahamu hii.
Mimi naamini kuwa kitovu kina madhara kama kikianguakia uume wa mtoto mchanga. Kwa upande wa wanawake hilo sijui na sikuwahi kusikia ila naweza kuamini pia.
 
Kama hamuamini shauri zenu watoto wenu waje kuwa ma Bwabwa hapa town.
 
Mimi mtazamo wangu ni njia ya kumfanya
Hii hadithi imakuwa ikisimuliwa for ages, especially kwa wanawake. Na hata pale unapotoka kujifungua nurses wanakwambia namna ya kuangalia kitovu cha mtoto, kusafisha mpaka kikauke, na hapo ndipo wanakwambia kwamba uwe makini kitovu kisidondoke kwenye uume wa mtoto. Sasa hili ni la ki-medical au ki-imani?
Mama wa mtoto asisahau majukumu yake kwa mtoto wake kwani, anapoambiwa kua kitovu pindi kinapodondoka kwenye uume husababisha uanisi inamfanya awe makini sana katika uangalizi huo na kumfanya mwanae awe katika hali nzuri ya uangalizi na usafi pia.!
 
Wandugu,

Napenda kufahamu kitaalamu juu ya imani au uvumi kuwa mtoto mchanga anapozaliwa lazima mzazi na hasa mama ahakikishe kuwa kitovu cha mtoto huyo kitakapokauka na kudondoka basi kisiguse sehemu nyeti za huyo mtoto. Inasemekana kuwa ikitokea kuwa kitovu hicho kimedondoka na kugusa sehemu hizo nyeti basi mtoto huyo kama ni wa kiume atakuwa bwabwa na kama ni wa kike nae atakuwa msagaji? (hatakuwa na feeling za kuhitaji mwanaume)..

Nahitaji maelezo ya kitaalamu na hasa kwenu nyie wataalamu wa tiba kuhusu hili kwani yanazungumzwa lakini hakuna justification ya kitaalamu inayotolewa zaidi ya kuonekana ni mapokeo ya imani tu.
Si kila jambo linahitaji ushahidi wa kitaalamu,ayo mambo mimi kwa sasa nayaamini na wala sidharau... nilitaka ushahidi wa kisayansi nilipoambiwa nikizini nje ya ndoa kisha nikamshike mtoto wangu hom anadhurika, Nikafanya experiment kabla ya kufika hom nikabeba mtoto wa rafiki yangu, nikafika hom wangu sikumbeba alinipokea kwa kunikumbatia miguuu (aliniwao) kilichitokea kesho yake asubuhi aliamka kalegea unatokwa na udenda kama teja, kwani vipimo vya hospitali vilipata ugonjwa
 
Ndugu zangu poleni na majukumu ya kila siku,

Inasemekana kuwa mtoto mchanga anapodondokewa na kitovu chake wakati kinaelekea kupona huwa uwezo wake wa sehemu za siri umepotea tena, yaani hususani kwa mtoto wa kiume hawezi kusimamisha tena.

Hapa nazungumzia ile sehemu ya placenta ambayo hufungwa baada ya kukatwa wakati mtoto anapozaliwa, huwa kuna wakati unapofika inakatika yenyewe na baadaye kitovu kitovu kinabaki ktk uhalisia wake.

Kina mama wengi huwa makini sana kabla ya kitovu kukatika maana wanaamini hivyo na hii si kwa vijijini tu hata akina mama wa mjini baadhi wanaelewa sana juu ya imani hii.

Ugumu wa imani unakuja katika solution ikitokea kimeangukia mzazi ukaona (mama) eti inabidi ufanye haraka uende sirini umjaribishie kwenye sehemu yako ya siri.

Imani hii imekaaje wadau maana tunazaa lakini kumbe kuna mengi.
 
Lisemwalo lipo. Hauna anayeweza ku-verify moja kwa moja ukweli au upotofu wa imani hii. Ila wewe fanya kama inavyoshauriwa ili usije kujuta baadae kwa kuwa mtoto wako dudu lake halisimami. Unaweza usijue, ila yeye akija kujua sababu ilikuw ni wewe, nadhani atakuchukia sana. Fedheha ya iutokusimamisha dudu kwa mwanaume ni kubwa kuliko kutokuwa na fedha wala mali. So kina mama wawe makini, waweke uzungu pembeni, acha tuamini hivyo tu kwa sasa. Ikija njia nyngne tutafuata.
 
Kitaalamu hilo suala la kitovu kinapoangua na kugusa sehemu nyeti za mtoto na kumfanya awe hanidhi si ukweli. Mie nahisi ni mila za baadhi ya makabila.

Kitaalam mtoto kila anapokuwa katika kipindi fulani basi kuna mambo lazima atapitia,sasa mzazi ambaye atamkataza huyu mtoto kufanya haya mambo yanaweza kumuathiri kisaikologia.

Mfano watoto wengi katika umri fulani huwa wanacheza kama vile wazazi katika familia, mtoto wa kiume baba na mtoto wa kike ni mama, so hawatakiwi kukatazwa, kwani ni mambo ya kupitia na baadae wataacha.

Pia kuna umri fulani watoto huwa wanajisaidia haja kubwa au ndogo pasipo kujielewa. Mzazi hautakiwi kumpiga na kumtisha mtoto, kwasababu hiyo ni hali kutokana na kutokomaa kwa mfumo wake wa fahamu. Pindi mzazi utapokuwa unampiga na kumtishia ili aache hiyo tabia, ni kweli ataacha ila yaweza kuwa ikamuathiri ukubwani.
na iwapo kazaliwa mzima na kabla hajaanza kucheza ki baba baba tuseme ana miezi mi 2 halafu inakuwa gojogojo je nayo ni mzazi kumkataza jambo fulani lililo muathiri kisaikolojia?
 
Inadaiwa kuwa kitovu cha mtoto aliyezaliwa huwa kinaandamana na mikosi na mabalaa mengi kutoka kwa mama. na ndio maana hutakiwa kuzikwa ardhini (kwa kiasili) na sio kutupa sehemu yoyote. Maelezo haya hayana utaalamu wo wote ila ni mambo ya kimila tu. ajabu ni kuwa makabila mengi hapa nchini yanaamini hivyo!
Nitafanya research juu ya hilo jambo na kupublish matokeo hapa

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wanajanvi
Ukweli ni kwamba kila Jamii wana taratibu zao na Imani zao kuhusu Namna ya kumlea Mtoto wa Kiume pale anapozaliwa!

Ila kuna huu uvumi ambao naona kama asilimia nyingi ya Jamii za Kitanzania wanauamini!

Je ni kweli kuwa mtoto wa kiume akikatika kitovu kikidondokea katika Dushe hawezi kusimamisha ukubwani mwake au ni Mambo tu ambayo watu wanajitungia tu?

Naomba wazoefu wa uzazi tuambiane hapa maana Mwanangu amekatika kitovu usiku wa kuamkialeo nikakuta kimedondokea kunako Dushe sasa hapa nilipo nimekosa amani kabisa na ndio first born wangu jamani hebu tusaidiane kama ni kweli nitamwokoa vipi
 
Inadaiwa kuwa kitovu cha mtoto aliyezaliwa huwa kinaandamana na mikosi na mabalaa mengi kutoka kwa mama. na ndio maana hutakiwa kuzikwa ardhini (kwa kiasili) na sio kutupa sehemu yoyote. Maelezo haya hayana utaalamu wo wote ila ni mambo ya kimila tu. ajabu ni kuwa makabila mengi hapa nchini yanaamini hivyo!
Kama kinaandamana na mikosi na mabalaa toka kwa mama. Sasa inakuwahe mimi mtoto ambae nimezaliwa na huyo mama, nimekula na kupumua kupitia hicho kitovu????
 
Back
Top Bottom