Uhandsome bwana sio Tabia!!

Kuna mdada alikuwa anamwambia mwenzake "Mi mwanaume awe handsome tu inanitosha na mambo fulani safi basi ili nizae watoto wazuri, Tabia wala sitajali sana sababu wanaume wote tabia zao zinafanana". akaendelea "Nikishapata watoto wazuri mi basi inatosha mambo mengine namwachia Mungu, maana wapo wengine unakubali wakuoe ukihisi ana tabia nzuri kumbe alikuwa anavaa ngozi ya kondoo".

Haya sasa wanaume tujipodoe.

kumbe nna uhakika wa kujitwalia kadri nnavyoweza....kuwa handsome dili mjini hehehehehehhe
 
Kuna mdada alikuwa anamwambia mwenzake "Mi mwanaume awe handsome tu inanitosha na mambo fulani safi basi ili nizae watoto wazuri, Tabia wala sitajali sana sababu wanaume wote tabia zao zinafanana". akaendelea "Nikishapata watoto wazuri mi basi inatosha mambo mengine namwachia Mungu, maana wapo wengine unakubali wakuoe ukihisi ana tabia nzuri kumbe alikuwa anavaa ngozi ya kondoo".

Haya sasa wanaume tujipodoe.

Heri mwanaume mwenye sura mbayaaa lakini ana akili za maisha na upendo wa dhati kuliko handsome mwenye akili za inzi!
 
Ni mtazamo tu...

Hapo ndio ninapompendea kiumbe wa kike....
Anapokuwa bado kigori 16-19 utamsikia mimi bwana
mume wangu lazima awe mrefu,handsome mwenye pesa
na kila aina ya sifa(akibahatika kumpata alhamdullilah)
Akivuka hapo kuanzia25-30 utamsikia aah mume
ninayemtaka asiwe mrefu sana,sura haijalishi kwa sana
ila tu aweze kunipenda na kunijali(akitokea alhamdullilah
Kuanzia 30-35 kiumbe huyohuyo utamsikia ninayemtaka
sitajali sura mradi tu awe na shughuli yake inayomwingizia kipato
Kutoka 35 na kuendelea kama hakubahatika kupata, kiumbe
huyohuyo utamsikia akisema aah mimi yeyote atakayejitokeza
niko tayari kuolewa naye,sasa jamani tuwaeleweje hawa binadamu..??

NAWAZA TU HAPA KWENYE PC YANGU.....

Ndio maana wakaitwa wanawake!
 
huyo dada ni mshamba tena alie bobea, atapigwa na kuachwa watoto hatapata. Kila handsome atamuona mume
 
Siipendi kabisa hii kauli kuwa wanaume wote mama/baba yao mmoja. Ni upuuzi unaotumika kuhalalisha maamuzi ya kipumbavu. Kila mtu ana mama na baba yake na malezi na mitizamo tofauti ya maisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom