Uhandsome bwana sio Tabia!!

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Kuna mdada alikuwa anamwambia mwenzake "Mi mwanaume awe handsome tu inanitosha na mambo fulani safi basi ili nizae watoto wazuri, Tabia wala sitajali sana sababu wanaume wote tabia zao zinafanana". akaendelea "Nikishapata watoto wazuri mi basi inatosha mambo mengine namwachia Mungu, maana wapo wengine unakubali wakuoe ukihisi ana tabia nzuri kumbe alikuwa anavaa ngozi ya kondoo".

Haya sasa wanaume tujipodoe.
 
DASA huyo atakuwa hajiamini kabisa, kwani hujawah kuona baba na mama sura zimepinda wakapata watoto wazuri? huo ni ulimbukeni square. . .
 
Last edited by a moderator:
mwanaume asifiwi uehandsome...anasifiwa kwenda bank kuweka na kutoa chapaaa....by Original comedy
 
Ndo maana ndoa za siku hizi hazidumu, wanawake wanatafuta ma handsome, ho ma handsome wengi wanapenda kulelewa tu, sasa mwanaume anakutegemea wewe mwanamke siku si nyingi unamchoka mara ooh mwanaume mwenyewe suruali hana kitu, mwisho talaka.
Hata kwa wanaume nataka mwanamke mwenye shepu, haya unaoa huko ndani ya nyumba tabia inakushinda
 
Kuna mdada alikuwa anamwambia mwenzake "Mi mwanaume awe handsome tu inanitosha na mambo fulani safi basi ili nizae watoto wazuri, Tabia wala sitajali sana sababu wanaume wote tabia zao zinafanana". akaendelea "Nikishapata watoto wazuri mi basi inatosha mambo mengine namwachia Mungu, maana wapo wengine unakubali wakuoe ukihisi ana tabia nzuri kumbe alikuwa anavaa ngozi ya kondoo".

Haya sasa wanaume tujipodoe.

Nina mashaka na ufahamu wake huyo aliyeyasema hayo, mwenye utashi na ufahamu ulio kamili hawezi kuhatarisha maisha yake na afya yake kwa uzuri wa sura ya mtu, hao watoto atawatunza lini kama ataletewa watoto na Ukimwi? Kuna faida gani ya kuwa na mtu mwenye sura nzuri na tabia mbaya ambaye mwisho wa siku anakutengenezea mauti na kuwaacha hao watoto wake wazuri yatima, ombamba au watoto wa mitaani inhali yeye umetangulia mbele za haki kwa uzembe? Huu ni ukauzu zaidi ya dagaa!!!

Tafakari!
 
Ukapata watoto wazuri halafu mambumbumbu a.k.a mambulataa , unafurahia tu kweli kuna mijanajike hamnazo kabisa
 
mwanaume asifiwi uehandsome...anasifiwa kwenda bank kuweka na kutoa chapaaa....by Original comedy
Kuna wannawake wenye cash ya kutosha..hawataki hela kutoka kwa mwanaume. Wanachohitaji ni HB!

Kwa wale watoto wa wakulima ambao wengi wao siyo wazuri ni lazima waangalie cash ya mwanaume kwanza!!
 
unajua mie wala simlaumu huyo dada maana watu bana siku hizi kwenye relationship full usanii na kila mtu anaingia kwenye relationship/ndoa kwa malengo yake. basi yeye malengo yake ni kupata watoto handsome/beautiful..who are to object/judge ni choice yake na kwa jinsi mahusiano ya sasa yanavyoenda i dnt blame her
 
mwanamme handsome mm no coz sihitaji presure za kila siku .........tabia ndio mpango mzima!!! pole zake
 
Unajua ukiwa handsome hata tabia zako zitakuwa poa tu, zitakuwa tabia za kihandsomehandsome. Kwahiyo yupo sahihi kwanza uhandsome mengine baadae.
 
usishangae kupata watoto wanaofanana na babu/bibi zao...utajuna na handsome wako, nafikiri tabia nzema ndio dili na sio sura
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom