Uhamisho watumishi wa Umma: Waziri Ummy Mwalimu acha usanii na siasa kwenye maisha ya watu

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Nchi hii kuna viongozi wa ajabu ajabu sana, hivi waziri anapata wapi mamlaka ya kuzuia uhamisho wa mtumishi wa umma ambaye mkataba wake unamruhusu kuhamia eneo lolote kisheria?

Utakuta mtu ana miaka mpaka 8 hadi 10 anafanya kazi ndani ya eneo moja, lakini leo hii anaomba kuhama kufuata familia yake anajitokeza mtu mmoja kwa jeuri yake anasema uhamisho umesitishwa. Hivi wewe Ndugu Ummu ungekaa miaka 8 mbali na ndoa yako ungefurahia?

Mnakuwa na statements za hovyo eti mtu akitaka kuhama ni mpaka wabadilishane kituo, kwa utaratibu upi? Mkataba umeandikwa kubadilishana au ni ukuaji wenu tu?

Kwakweli serikali chini ya CCM ni shida tupu. Hatuwezi kuendesha nchi kwa matamko tu bila kufuata sheria, mmeshindwa kuendesha nchi mmebakia na matamko na kusaidiwa na polisi. Hii haikubaliki muondoke tu muache kunyanyasa watu bila sababu.

Mambo ya kusema kama hutaki acha kazi, ni kauli zisizo na uungwana kila mwananchi ana haki yake kutakiwa Serikalini ikiwa ana sifa. Mambo ya kama hutaki kufanya kazi acha si kauli nzuri hata kidogo.
 
Nilimuona kama mtu mwenye kujikweza na sababu zake nyepesi. Hutaki watu wahame? Wewe ni nani the Almighty?
 
Viongozi wa juu ni kikwazo cha ustawi wa maendeleo ya nchi hii..yeye kashiba anjali akitaka kwenda kwa mumewe hata sasahivi anaenda..ila mtumishi kufuata famili yake ni kosa..kuugua usogee mjini kwenye huduma za matibabu ni kosa..eti uhamie sitimbi ili ukafe..hawa viongozi waliokosa maono ni maumivu kwa nchi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukuwasikiliza wanasiasa (hasa hawa viongozi wetu) unaweza jikuta Unachanganyikiwa maana matamko yao mara nyingi huwa yapp kinyume na sheria
 
Nguvu yako ya kura ya kubadilisha mfumo huu huwa unauza kwa ahadi tamutamu na vizawadi vidogo vidogo na kusimamia kwa nguvu na ulaghai uhesabu wa kura,acha kulalamika na mimi binafsi waalimu ni wanafiki(nami nilisomea ualimu)
 
Ummy mwalimu anahusikaje hapa nadhani Ni viongozi wa chini yake wanakwamisha
Kauli ya kukataza uhamisho kutoka vijijini/miji midogo kwenda mjini kaitoa Waziri Ummy Mwalimu na sio wasaidizi wake

Style ya kufanya kazi za serikali kwa matamko yasio ya kisheria iliasisiwa kwenye awamu iliyopita. Kila mtu alikua anatoa maagizo ili kumridhisha "Mkuu" ikiwemo ya ma DC na Ma RC kuweka watu ndani!

Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Miji pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya nao wanatoa matamko kwa watumishi kwamba hakuna kwenda likizo mpaka wakamilishe ujenzi wa madarasa ambao unakadiriwa kuchukua hadi miezi saba!!!!

Ajabu ni kwamba hawawalipi hizo likizo zenyewe ambazo zipo kisheria. Inapotokea kufuta likizo ya mtumishi kuna taratibu zake ikiwa pamoja na kuinunua

Huyu Ummy Mwalimu hivi karibuni alitoa tamko la kuwazuia wakuu wa mikoa kutoka nje ya mikoa yao bila kibali cha Rais au Makamu au Waziri Mkuu!!! Hii haikubaliki na ni uvunjaji haki za binadamu na kanunu na taratibu za utumishi wa umma

Huku ni kudhalilishana kwakweli! Unamzuia mtu kutoka nje ya mkoa amekua ni mtuhumiwa ambaye yupo chini ya uangalizi wa mahakama au polisi?!!! Kwani isingetosha kuwapa malengo ya Wizara na wakawaacha na uhuru wao kama watu huru tena viongozi wa umma!!! Hizi ni athari mbaya kabisa za mind set za watawala zilizoachwa na awamu ile.
 
Serikalini wafanyakazi wanadeka sana mkataba wa ajira kawaida Ni wa mtu binafsi mmoja tu na mwajiriwa lakini serikalini Ajabu eti mtu anajiamlia tu nataka kuhama nifuate mume wangu au mke wangu aiseeee!!! Private sector mleta mada ungepigwa makofi na mateke ndipo upewe barua ya kufukuzwa kazi moja kwa moja.

Oeni full time house wife asiyefanya kazi ili muda wowote uhame naye bila shida na wanawake wafanyakazi serikalini oleweni na wanaume wasio na kazi muwe nao popote
 
Nchi hii kuna viongozi wa ajabu ajabu sana, hivi waziri anapata wapi mamlaka ya kuzuia uhamisho wa mtumishi wa umma ambaye mkataba wake unamruhusu kuhamia eneo lolote kisheria?...
Ummy Mwalimu hajasimamisha Uhamisho amesitisha kwa muda tena ni Uhamisho kwenye Majiji, Miji na Manispaa kwa ajili ya kufanya msawazo wa watumishi.

Kilichopo ni kwamba kwenye Maeneo hayo Watumishi wamezidi ni wengi sana na wanaohitaji kuhamia huko bado ni wengi kitu kinachopelekea upungufu kwenye halmashauri za Pembezoni.

Hata Hivyo uhamisho wa kubadilishana unaruhusiwa
na ule wa kuhamia kwenye Halmashauri za Wilaya unafanyika kama kawaida
 
ushauri wangu kwa vijana,Kama una Target ya kuajiliwa na serikali basi msioe/kuolewa kabla ya kuajiliwa!!, wake/waume zenu mtawakuta huko huko makazini !! kiherehere chenu Cha kuoana mapema kabla ya ajira ,mwisho wa siku mnakaa mbalimbali ,matokeo yake mnakuwa na familia mamluki ,unakuta mwal.anawatoto 3 wawili sio wake!! muwe mnatembelea makazini kwa wake zenu Mara moja moja mjionee sura zinazofanana na watotowenu!!
 
Back
Top Bottom