Uhamisho wa kijana kutoka shule za kutwa (Kata) kwenda shule maalumu.

charrote

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,670
3,639
Wakuu habari za muda huu.
Nina kijana mtoto wa ndugu yangu yuko kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Serikali (Kata), nahitaji kumuhamisha kwenda shule za vipaji maalumu za Serikali mfano ilboru, tabora boys, kibaha boys nk. Naomba kwa yeyote mwenye kufahamu utaratibu anisaidie .Kijana alikuwa na ufaulu wa daraja A.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaishi wapi?
 
Unayo pesa?!?!
wewe unajulikana?

anyway acheni kutuonea kata,
Mbona Mimi nilisoma kata,na nikapiga 1:10?

shule Ni yeye kichwani!
 
Ufupi tu ni kwamba huwezi kumhamishia huko. Mpeleke tu private nzuri kama mfukoni kuko poa. Au umeshasahau matokeo ya csee yaliyotoka mwaka huu zaidi ya shule 30 za mwanzo zote ni za private! Labda ungesema unataka umhamishe kutoka Mzumbe kwenda Ilboru, walau wenye hizo shule zao wangekupa mawazo stahiki.

Hizo shule zinachukua wale wenye ufaulu wa juu tu (kama kuna njia za mkato, mimi sijui). Na bahati mbaya wakwako inawezekana hakufikia huo ufaulu na ndiyo maana amebakia ya kata. All in all, maisha ni popote. Kama kijana wako anajitambua, anaweza kubaki hapo hapo na bado akafanya maajabu.
 
nahitaji kumuhamisha kwenda shule za vipaji maalumu za Serikali mfano ilboru, tabora boys, kibaha boys nk. Naomba kwa yeyote mwenye kufahamu utaratibu anisaidie .Kijana alikuwa na ufaulu wa daraja A.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngumu sana hiyo! Nakumbuka kuna dogo nilimhamisha kutoka Kata kwenda Kibasila tu hapo!!Kilichotusaidia ni matokeo yake mazuri ya Form II vinginevyo wala tusingepata! Sasa vipi kuhusu hizo shule unazotaka??!
 
Back
Top Bottom