Uhamiaji Nako!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhamiaji Nako!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by AK-47, May 20, 2010.

 1. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa yangu alienda ofisi za uhamiaji leo kutafuta pasi ya karatasi ili aende Uganda cha ajabu akaambiwa karatasi za pasi zimeisha Dar es Salaam yote akitaka aende Kibaha Mkoa wa Pwani. Akaamua kufunga safari hadi Kibaha kweli bwana akaambiwa zipo ila atoe elfu 20 apatiwe kitu... akalia hali akapata kwa shilingi 15 alipotoka nje akasikia wenzie waliotoka Dar wakilalamika kwani kila mtu alipigwa bei yake kuna waliolipa elfu 30, elfu 20 kwa ajili ya pasi hiyo ambayo bei yake halali na ya kwenye risiti ni sh elfu 10 tu. Najiuliza hii nchi sasa inaelekea wapi ? Watanzania tuunganishe nguvu zetu Oktoba kieleweke jamani tuachane na hekaya za maisha bora hewa kwa kila Mtanzania.
   
 2. Edgartz

  Edgartz JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Eebwana eeh me nilijua ni huku mbeya tu kumbe hata uko ishu ndo hizo? Yaani hawa jamaa wamekuwa wasumbufu balaa
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hii ndo Bongo mkubwa kama Dar ndo hivyo najiuliza kwetu Biharamulo itakuwaje!
   
Loading...