Uhalisia wetu

Uhalisia wetu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,070
1448708433655.jpg

Nafahamu fika watu watakuwa na tafsiri tofauti kuhusiana na hili na hata nikijaribu kumuuliza kila mmoja atakupa maelezo mazuri na ya kuvutia kulihusu. ..hii ndio hulka ya binadamu kujinenea vema hii ndio kwa kiingereza tunaita true sense of human behaviour.

Lakini leo nataka tulijadili hili kwa muktadha wa ukweli wetu wa ndani kabisa uliofichika kwenye uvungu wa moyo wa mwanadamu, ukweli na chanzo halisi
Tulijadili kwa maana pana zaidi maana ile ya kile kilichofichama kwenye moyo yetu. Hasa pale linapokuja swala la kuguswa kihisia kwa ubaya au kwa wema au kwa taharuki.

Uhalisia wa hisia zenye pande tatu mtenda mtendwa na kitendo na chanzo sababu na matokeo.

Katika viumbe hai kuna makundi matatu hivi , lakini yanayotajwa sana ni mawili 1.viumbe waliostaarabika(binadamu) 2. Hayawani (wanyama) kundi la tatu ni vile viumbe visivyoonekana katika ujumla wao.

Habari hii inawahusu zaidi binadamu na wanyama, binadamu anawekwa kwenye kundi la ustaarabu lakini je ni kweli huyu tunayemfahamu sisi ni mstaarabu kweli kama inavyosemwa?Hapana...huyu anayeitwa mstaarabu anasukumwa na kitu gani hadi afanye mambo ya kutisha na mabaya kabisa? Hasa mauaji...! Je ni choyo? Chuki? Hasira? Wivu? Kisasi? Utajiri? Au je ni majumuisho ya hayo yote?

Ni ukweli usiofichika kuwa kuna wakati maisha yanakuwa hayana maana kabisa na yaliyojaa dhuluma na utupu. Je hiki ndio chanzo cha mauaji ya kutisha na ya kikatili kabisa?

Hebu fikiria kwa mfano ni roho milioni ngapi zimepotea tangu mwanadamu alipoanza kutumia jiwe na fimbo ya silaha ya kuangamiza roho? Huu ndio uhalisia wetu, binadamu ni mtu tuu au ni zaidi ya hapo?

Binadamu hawekwi kwenye kundi la hayawani kwakuwa eti ni mstaarabu....haya ni maelezo ya kukidhi matakwa na mahitaji asilia ya kiumbaji lakini lazima tukubali ukweli huu mchungu kuwa kama kuna hayawani wa kweli kabisa basi hayawani huyo ni binadamu na si mnyama.

Angalia katika dunia hii hakuna nchi hata moja inayokosa silaha kali majeshi ya ulinzi vyuo vya kijeshi viwanda vya silaha mbalimbali. ..haya yote ni ETI kwa ajili ya kujilinda na adui.!!! Adui gani huyo?

Adui wa kweli hayuko mbali , wala hahitaji silaha kali na majeshi bora kabisa kummaliza. Adui yetu ni sisi wenyewe, UHALISIA wetu ni hisia zetu u choyo wetu kisasi na u mimi

Hivi dunia ingekuwaje kama pesa zote zinazotumika kwenye kutengeneza silaha kununua na kutoa mafunzo kwa ajili ya kutekeza roho za waso hatia zingetumika kujenga dunia moja yenye afya amani upendo wa kweli furaha natumaini na mustakabali wa binadamu wote bila kuwa na ajenda ya siri , bila upendeleo bila kujali rangi utaifa au imani..!!!

Lakini binadamu ni kipofu kiziwi na mpumbavu kabisa . Ndio maana hujiona yeye ni bora kuliko chochote.

Binadamu wote tu wanafiki, wazandiki, katili na hatuna kweli ndani yetu, tu waongo kwa kiwango cha kutisha na hayawani hasa...binadamu ni bingwa wa kuonyesha ukatili wa wanyama kama simba , chui nk lakini hii si haki hii ni dhihaka kubwa kwa wanyama, mnyama hana silaha nyingine zaidi ya viungo vyake mwilini.

Ni mnyama gani anaweza kuwafungia wenzake kwenye nyumba na kuiwasha moto au chumba cha gesi au kuwapiga risasi? Au kuwashambulia kwa kila aina ya silaha? Hakika hakuna.

Kilichotokea Hiroshima Japan si unyama tu bali ni uhayawani wa kiwango cha juu kabisa....madhara ya lile bomu bado yapo mpaka hivi leo
Kadiri maarifa ya mwanadamu yanavyozidi kukua ndio ari ya kupiga kutesa na kuua inavyozidi kuongezeka...maarifa ya sasa si ya kuua mtu mmoja au wawili bali maelfu kwa wepesi na kwa wakati mmoja.

Tu wapuuzi kuweka mustakabali wetu kwa maisha mema yajayo wakati tunafanya kila aina ya juhudi kuangamiza kizazi hiki. ...tukiendelea hivi kizazi kijacho kitakuwa mashakani...na huu ndio uhalisia wetu

RIP Kamanda ALPHONCE MAWAZO
 
Nitaweka baadhi ya picha za mauaji ya halaiki au mauaji ya watu wengi kutokana na visasi dhuluma imani uadui nk
Sina nia mbaya ya kuziweka picha hizo....Natanguliza huzuni na masikitiko yangu...Mungu awarehemu pale walipo wakiwa pweke
Japo picha ni chache nitakazoweka hapa lakini maudhui yake yanavuka mipaka hii na kwenda mbali zaidi duniani kote..hii ni sehemu ndogo tu ya kile kinachotokea kila siku kila saa na kila dakika katika ulimwengu huu uliochoka
Picha hizo ni kiwakilishi cha matendo halisi asilia ya binadamu zikileta mwangwi wa uumbaji maisha na uhalisia wake
Uhalisia wetu unajengwa kwenye hizo picha na dhana nzima ya mtu aitwaye binadamu
 
Once a day nimevamiwa na ufahamu kukumbuka kuwa siraha zote zilizo/zinazotengenezwa ni kwa ajiri ya binaadamu wa sayari hii hii,ndipo nnapouona upungufu alionao binaadam ni mkubwa kuliko akili alizojaliwa.
 
Kwa wale wenye imani ya kikristo kama mimi sishangai sana kwani yalishatabiriwa yatatokea haya ikiwa ni ishara ya siku za mwisho....Watu hawana hofu ya Mungu tena binadamu tumekuwa ni zaidi ya wanyama....Soma 2 Timotheo 3:1-5 Inaeleza watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, Wenye kupenda pesa, Wasiowatii wazazi,Wasio washikamanifu, Wasio na upendo wa asili, Wasio jizuia, Wakali n.k.
 
Once a day nimevamiwa na ufahamu kukumbuka kuwa siraha zote zilizo/zinazotengenezwa ni kwa ajiri ya binaadamu wa sayari hii hii,ndipo nnapouona upungufu alionao binaadam ni mkubwa kuliko akili alizojaliwa.

Kwa wale wenye imani ya kikristo kama mimi sishangai sana kwani yalishatabiriwa yatatokea haya ikiwa ni ishara ya siku za mwisho....Watu hawana hofu ya Mungu tena binadamu tumekuwa ni zaidi ya wanyama....Soma 2 Timotheo 3:1-5 Inaeleza watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, Wenye kupenda pesa, Wasiowatii wazazi,Wasio washikamanifu, Wasio na upendo wa asili, Wasio jizuia, Wakali n.k.

1448718890980.jpg
 
Mzizi upo kwamba anasukumwa na nini?kutenda wema au ubaya?Hivyo vinavyomsukuma binadamu kutenda ubaya wa kutisha ndio vibaya.Binadamu ni kama computer ukiiweka programs Nzuri ataegemea Kwenye mazuri na ukimwekea program mbaya atakuwa mbaya.
 
Once a day nimevamiwa na ufahamu kukumbuka kuwa siraha zote zilizo/zinazotengenezwa ni kwa ajiri ya binaadamu wa sayari hii hii,ndipo nnapouona upungufu alionao binaadam ni mkubwa kuliko akili alizojaliwa.

1448733961669.jpg1448733972542.jpg kazi ya mikono ya mwanadamu anayejinasibu kwa ustaarabu na kumcha Mungu na kushika dini
 
Je kati ya mnyama na binadamu ni nani hayawani?
... as a superorganism, humanity is searching for the stars while, here on earth, we have totally failed to control our population and share the little our planet can provide to eradicate poverty on our planet!
While technology is almost advancing to levels almost out of our hands, the only best use we make of it is finding better ways of killing one another!
BINADAM NI TAKATAKA!
 
Back
Top Bottom