Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Tanzania nchi nchi inayoongozwa kibabaishaji haitakosa kupata sababu za kuhalalisha jambo baya kama hili.
 
"Mwalimu ni mwenye nguvu,ana nguvu kuliko askari mwenye bunduki. Mpumbavu hawezi kuona nguvu zake. Mwalimu ana nguvu kwa sababu anashona vazi la akili."

Walimu wanaendelea na mgomo wao kimya kimya, matokeo yake ni kuwa watoto wetu wanatembea uchi, uchi wa akili; madhara yake tumeanza kuyaona katika matokeo ya kidato cha nne. Madhara mengi zaidi yatazidi kuonekana katika nyanja mbalimbali.
Wazazi tuibane serikali iwape walimu haki zao, ili wafundishe watoto wetu. Tuisheni hazisaidii kitu, mtoto hufundishwa shuleni kwa utaratibu maalumu.

Shime serikali,rekebisha mfumo mzima wa haki na masilahi ya walimu, ili tuokoe taifa letu.
 
Hao walimu hata serikali iwape m2 net kwa mwezi bado wanafunzi watafeli tu.Sababu za kufeli wanafunzi wa kidato cha nne ni zaidi ya mgomo wa walimu (kama kweli upo).
 
Aha aha aha aha...hii strategy mliotumia walimu ime prove success 100%....Sasa majibu ya Tume yatakua kama:-
1. Ongeza mishahara ya walimu
2. Tatizo maslahi kiduchu ya walimu
3. Walimu hawana Motisha
4.Walimu wana migomo baridi
5.walimu wamedharaulika ndo maana kwa kwa sasa bora liende
6.walimu wa sayansi soko lao kubwa ktk sekta nyingine maslahi yao yaongezwe saaaaana ili wabak






 
Hao walimu hata serikali iwape m2 net kwa mwezi bado wanafunzi watafeli tu.Sababu za kufeli wanafunzi wa kidato cha nne ni zaidi ya mgomo wa walimu (kama kweli upo).

Mgomo upo,tena umekommaa, kama si kushika kazi. Juulize,
1. Ni kwa kiasi gani walimu wanatumia muda wao kufuatilia maendeleo ya kielimu ya wanafunzi wao?
2.Ni mazoezi mangapi na test ngapi walimu wanatoa kwa wanafunzi wao?
3. Fanya utafiti,hata hao walimu wakitoa test na mazoezi yanakuwa ya masuali mangapii?
4.Ni kwa kiasi gani walimu wanaandaa vipindi?, hawana muda huo.
5.Ni vitu gani walimuwanafundisha darasani, na kwa unani upi au ufasaha upi?
6. Kumbuka walimu hao ndio walewale wanaofundisha St.Fransis au Marian.
7.Ni mwalimu gani leo anajihangahisha kufuatilia maadili ya mwanafunzi. Leo hii mwanafunzi akisililiza muzilki darazani-mwalimu sawa tu!!, Mwanafunzi asipofanya mwaswali - Mwalimu anashukuru na kufurahi.

Tafakari hayo, tutaendelea
 
view yangu ni tofauti kabisa kwamba walimu ndo chanzo cha wao kufeli eti mgomo..ni kwamba hata private skulls watoto wameanguka.. Mwaka jana ulikuwa ni wa kizazi cha facebook so nadhani ndo maana wengi wameteleza.. Kila dogo yuko fb kila dogo yuko fb yaani.m hadi saa 9 usiku.. Makampuni ya simu yakazidi itangaza so..m facebook ndo chanzo.. Imao
 
view yangu ni tofauti kabisa kwamba walimu ndo chanzo cha wao kufeli eti mgomo..ni kwamba hata private skulls watoto wameanguka.. Mwaka jana ulikuwa ni wa kizazi cha facebook so nadhani ndo maana wengi wameteleza.. Kila dogo yuko fb kila dogo yuko fb yaani.m hadi saa 9 usiku.. Makampuni ya simu yakazidi itangaza so..m facebook ndo chanzo.. Imao


Unakubaliana nami kuwa wa akina dogo hawana mwelekezi , na hawana walezi; ambao inawapasa kuwaelekeza namna bora ya kutumia facebook, simu n.k. Hivyo akili zao wako utupu(uchi). Mtu pekee wakuwaelekeza hayo ni mwalimu. Huyo mwalimu hafanyi hiyo kazi, amegoma. Si mwalimu wa serikalini au wa binafsi( Hata wao wanacholipwa ni duni).

Shule cha binafsi waliofanya vizuri, fiatlia mishahara ya walimu, na mazingira ya kazi. Pia angalia utaratibu wa utendaji kazi unao tumika.

Bila ya kutatua tatizo la walimu, haka kama tukibadilisha mitaala na kurudika vitabu na madawa ya maabara matokeo yatakuwa ni yaleyale. Unamrundikia nani ? ikiwa wa kuvitumia hataki, kagomaa?
 
nchi km singapole mwalimu ndo highly paid person.km serikali na wadau wanaona mshahara duni si tatizo acheni tuendelee hv hv.tutakuza taifa la watumwa kwa jirani wanaotuzunguka na slave masters wachache wa ndani wanaosoma sekondari za mil 3 na wanaopelekwa nje ya nchi.
 
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
1.Elimu ni ufunguo wa maisha na serikali yetu yatambua hilo,Hivi tafakari mwanafunzi aliyepata daraja la nne unampeleka awe mwalimu hivi kweli hii si njia ya kuharibu kitovu cha elimu
2.Fikiri wanafunzi wajafanya mitihani na matokeo yanaonyesha kafauli,Hivi kweli tunaenda wapi hii inapelekea untrusted kwa wazazi na wanafunzi kiujumla.
3.Mungu ibariki Tanzania
 
We hizi sababu umetoa wapi? Wakati wahusika wenyewe wamesema ni facebook na tweeter ndo imesababisha.

Ndo maana vijijini wote wamepata div 1 kwakuwa hawaju facebook na tweeter, ndo maana ulaya na amerika wanafunzu wanafeli wote kwa kuwa facebook na tweeter zimeanzia huko.
Itabidi mitihani ya mwaka huu iwekwe kwenye facebook na tweeter ili angalau wanafunzi wafaulu kidogo
Uciwe unakalili,kwan fb na twitter ndo imewafelisha,think big!
 
Uciwe unakalili,kwan fb na twitter ndo imewafelisha,think big!
Bwana jeromy SIJAKALILI kama ulivyosema, hayo siyo maneno yangu, kama ungesoma kwa makini kidogo tu nini nimeandika mate yasingekutoka hivyo, au na wewe ni muathirika wa haya maafa nini?
 
Back
Top Bottom