mimi nina kamshangao kidogo wadau, hizi alphabet on license plate zinasogea kweli na tumeshifikia kama sio kupita herufi "CCM" na "CCJ" ila napata mshangao kidogo.
na kuzurura kwangu kooote kama messenger Dar na mikoani nimefanikiwa kukutana na gari1 aina Toyota Verosa ndio ina herufi za CCM. Kwa hiyo ya CCJ nimekutana nazo mbili, moja ni Land Cruiser VX v8 nyeusii na tinted nyeusiii na ya pili yake nimepishana nayo leo kinondoni Toyota Rav4 short chasis nyeusiii na tinted nyeusiiii.
hivi kuna uhusiano wowote hapa au mawenge yangu tu?
**Naosha kinywa tu wadau, sijaandika kimtazamo wa kisiasa.!