johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 93,985
- 164,232
Kuna vitu viwili vya msingi ambavyo waziri alipaswa kuviangalia, mosi vyeti vya kughushi na plli vyeti vilivyopoteza uhalali.Mtuhumiwa mwenye cheti cha kughushi ni tofauti kabisa na mtuhumiwa mwenye cheti kilichopoteza uhalali na huyu wa pili "anasameheka" so kuwaweka kundi moja si halali.Mfano mtu aliyefeli std 7 akakariri darasa kwa kubadili jina, huyo cheti chake ni halisi lakini si halali na kwahiyo anasameheka hata kwa kulipwa mafao tu.Sasa sielewi kwa nini waziri aliwaweka watenda jinai na wakiuka taratibu kwenye kapu moja na hivyo kupewa adhabu moja hii siyo haki.Jambo lingine ni wale wenye degree bila kuwa na vyeti vya sekondari, japokuwa wameachwa waendelee kuchapa kazi lakini mimi naona hawa ndio hatari zaidi, kwanini?TAFAKARI kidogo!Mods naomba msichanganye huu uzi ili wale wazee waliorudia madarasa enzi za Mwalimu wapate pa kusemea/kusemewa, ahsante.