Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Benki Kuu ya Tanzania imezitaka benki zote nchini kuhakiki taarifa za wateja wao, sote tunajua jinsi ilivyo rahisi kwa mtu kuchonga muhuri feki mtaani na jinsi watendaji wa kata na mitaa wasivyo makini katika kuwathibitisha watu wanaokwenda kwao kuomba utambulisho.
Naamini Benki Kuu (kupitia UWT) wanayajua yote haya na kama ningekuwa Gavana nisingepoteza muda kuziomba benki zihakiki wateja wao badala yake ningeiomba serikali iharakishe mchakato wa kuleta vitambulisho vya uraia, pamoja na zoezi la kuhakiki anwani za makazi ya watu.
Naamini zoezi hili litafanyika na pesa haramu zitaendelea kuingia kwenye mfumo wa benki zetu bila wahusika kugundulika, kama kweli lengo ni kudhibiti fedha haramu serikali ianze kwanza na uhakiki wa vyanzo vya mapato vya wamiliki wa magorofa yanayoota kila uchao mitaani.