Uhaini wa Mtwara ulipangwa


Kikwete, Prof. Mhongo & Co wameshavuta 10% ya hiyo gas pipe construction from MTWARA to DSM (then BAGAMOYO?) so inakuwa ngumu kuitema!! Think TWICE MEEN! Ukiyasikiliza maelezo yao yote yamejaa sanaa tuu!!. Kwani kama lingekuwa ni jambo la kheri kwa wanaMtwara lingewekwa wazi na watu waengeelewa!! Badala yake maelezo yao yamejaa kejeli, ubabe, majivuno, dhihaka, nk and then wanamtafuta MCHAWI ASIYEKUWEPO!!
 
hata kuiongoza familia y\huwezi wewe kama haya ndio mawazo yako.imepangwa na nani na umesikia wanamtwara for the past 2days walikuwa wanasubiri huyo sospeter aseme neno hapo ndipo walipojianda akili zakushikiwa
 
Utakuwa hayawani kama hujui kuwa vurugu zilipangwa! Vipeperushi vilisambazwa kuhamasisha watu mchana kweupeee! Muhongo akaairisha hotuba yake nao walihairisha pia aliposoma hotuba yake iliyo kinzana na matarajio yao matokeo yake tumeyaona. Hatuitaji darubini kuona mambo kama haya!
 
Kwa akili yako umeona kwamba hapa umetoa hoja yenye mashiko? Ndiyo tatizo la "KUBINAFSISHA AKILI". Wakati wote unatoka na mawazo ya kuwafurahisha MABWANA.

ZINDUKA!!!!

Kama huoni mantiki ya hoja hii, basi wewe ndo unahitajika kuzinduliwa.
 
Naona post nyingi leo zinahamisha issue ya Mtwara kwenye uhaini na kwa kuungaunga nukta, CHADEMA iingie ili, lililopangwa, lifanywe. Nakumbuka uzi wa pasco kuhusu mkutano/maongezi yake na Tendwa, na maneno ya Nchimbi leo.
Think tank wenu CCM kashindwa kazi, mwachisheni, fanyeni yale mliyowaahidi wananchi.
 
ukiona nyumba yako inachomwa moto na mchomaji unamuona unahitaji kumsubiri jirani akwambie la kufanya?:heh:
 
Mm ninachojua wana mtwara wenyewe ndo walipanga kutokana sera na kutokuwa wawazi magamba katika mradi huu wa gesi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Kadri wanavyojaribu kutatua matatizo kwa nguvu ya risasi ndivyo wanavyochochea hasira na kusababisha hasira dhidi ya viongozi wa ccm na hivyo kisasi kulipizwa dhidi yao.
Hakuna damu inayomwagika ikawa kimya. Waliimwaga Arusha, wameimwaga Morogoro, wameimwaga Iringa, wameimwaga Songea, wameimwaga Mtwara na watamwaga nyingine nyingi maana inaelekea watanzania hawaogopi risasi tena.
Hii damu haitabaki inyamaze wala watawala hawatakuwa na amani hata kama wamemaliza mihula yao maana damu haina tabia ya kunyamaza.
Toba ndio ya muhimu badala ya sababu lukuki zinazojengwa. Nipo nasoma kitabu kinaitwa Hitler's hangman nashangaa mengi ninayosoma ndani ya kitabu hiki ndio naona wanafanya watawala wetu na vyombo vya usalama wao.... Tunakwenda kusiko watanzania ndugu zangu... Ngoja tuone mwisho.
 
Kama kweli kinana anahusika kwenye issue ya artumas mtwara,ccm imechafuka sana
 
Nadhani lazima tujiulize kunapokuwa na uwekezaji kisha tukasema haya ni matunda ya watanzania wote tunawatendea vipi haki wakazi wa eneo husika?
Ni kweli watanzania wote tunahitaji kupata manufaa lakini kama hakuna masilahi kwa eneo husika tusemeje?
Tunajua siku zote eneo husika la uwekezaji ndilo upata madhara ya kemikali na maafa mengine yatokanayo na uwekezaji kweli kwa dhamila safi mioyoni tuna hakika kuwa eneo la uwekezaji linafaidi vizuri?
Mbona nasikia vilio vya wabunge kila kuliko na uwekezaji hasa wa madini?
Ebu niambieni kwa nini bei ya sukari Kyaka au Bukoba ni kubwa kuliko hata ya Dar es salaam? Wakati bei ya sementi inayozalishwa Dar ni ndogo kuliko ile ya Bukoba?
Mara ngapi tumeaminishwa uwekezaji kwenye nchi kutapunguza makali lakini badala yake ndio hali imekuwa ngumu?
Tuambizane ukweli bila unafiki enyi watanzania wenzangu, hivi tuna hakika uwekezaji huo wa gesi utapunguza bei ya umeme?
Watanzania tukubaliane namna ya kugawana keki yetu na tusianze kuitana majina machafu kama uhaini, ugaidi na majina ya hovyo ya namna hii. Mazungumzo yatatupeleka kuzuri, ulaghai utamwaga damu zetu na wanetu.
 
Nasikitika tu kwamba wabune wetu wa ccm wanadhani eti wananchi wa mtwara hawawezi kufanya kilichofanyika, lazima kuwe na mkono wa mtu. haya ni matusi kwa wana mtwara kwani ni sawa na kusema wanamtwara hawajitambui, hawajui haki yao, hawajui wanachokitaka na kwamba wao ni watu wa kupokea tu. CCM msijidanganye watu wanawaelewa sana kwa ufisadi wenu. Hadanganyiki mtu hapa
 

  • Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao. Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
  • RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari


 
Kwa hiyo wewe ndio unajua kuwa jeshi la tanzania tuu ndio limejifunza kuua,la misri lilijifunza kubembeleza watoto,la libya lilijifunza kumwagilia mchicha,na la syria limejifunza kutawaza wazee...pumbavu wewe unajua pipoz power wewe?acha vitisho vya kijinga...haujui tuu hii nchi imebakia nani amfunge paka kengele...
 
Ingekuwa wanamtwara wamekubaliwa na kufikia muafaka kuhusu hoja yao halafu wakaendelea na fujo hapo ningesema huo ni UHAINI lakini kuuita uhaini wakati wanamtwara wana hoja ya msingi ya kuzungumzika lakini WATAWALA hawataki kuwasikiliza ni UFEDHURI WA KUTUMIKA KISIASA TU!
 
....kaka mtwara na lindi sasa ndio uwanja rasmi wa mapambano ya kisiasa(zaidi) kati ya vyama vikubwa vya kisiasa (C.C.M, C.U.F, NA CHADEMA)....vijana wanatumiwa na watatumiwa...!wakijipanga (vijana hao wa lindi na mtwara), wanaweza kabisa kupata, ""furaha ya kunguru kwenye ugomvi wa panzi"..lakini wakishindwa....(na hili linanitisha sana!), basi wao ndo watakuwa "panzi wanaopigana na kuwafurahisha, na kuwarahisishia kunguru kazi ya kujipatia mlo"....amkeni vijana wa lindi na mtwara..kumbukeni alichokisema bob marley..."as we've been taken for the granted, much too long....rebel...!" ujumbe huo uwe ni wito...! wanasiasa (na wajanja wachache wenye maslahi haramu ya kiuchumi katika mtwara) wanataka kuendelea kuwatumia...! daini haki zenu, lkn bila kusimamiwa nao..chagueni viongozi miongoni mwenu...! na mtashinda..!
 
Tuko pamoja mkuu wana mtwara wanahaki na ni lazima wasikilizwe kwani mikoa yote yenye madini wananchi wake wanaongonza kwa umasikini na matokeo yake wananufaika vigogo wa ccm na serikali tumechoka na upuuzi huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…