Nimejaribu kusikiliza maelezo ya zito ktk video ya tuhuma dhidi yake na ambayo ipo hapa jamvini, nimegundua yafuatayo:
Ushauri kwa CHADEMA:
Wewe unayehitaji mabadiliko katika Tanzania unaishauri nini CHADEMA?
[*=1]CHADEMA kuna tatizo la mifumo sawa na matatizo ya mifumo tuliyonayo ktk taifa letu
[*=1]Zitto anautumia vizuri udhaifu huo wa mifumo kwa sababu zake binafsi ambazo nadhani anazielewa mwenyewe kwa maana mtu ambaye ni NAIBU KATIBU WA CHAMA ansema:
- Yeye amekuja kwenye siasa za kitaifa akiwa na umri mdogo sana, jiulize kuna mahusiano gani kati ya umri na IQ
- Chadema hakuna migogoro lakin anapigwa mishale ndani ya chama kwa kuwa uchaguzi umekaribia na kuna nongwa kwa sababu yeye aliwahi kugombea nafasi ya mwenyekiti
- Yanayotokea chadema yalishawahi kutokea vyama vingine na kimsingi hakuna jipya maana waliowahi kuitwa WASALITI leo ni makamanda wa chadema eg marando
- Anapambana uswisi kutetea pesa za watz an Africa na anahitaji kupewa moyo lakin anakwamishwa na baadhi ya CDM, jiulize ANAPAMBANA na siyo km chama au timu TUNAPAMBANA
Ushauri kwa CHADEMA:
- Zito anatumia udhaifu huo wa mfumo kufanikisha kazi aliyotumwa na ccm. Kwa hiyo ikiwa kweli atapambana kuwa mwenyekiti wa chama na ukweli ni kuwa hawezi kupata lakini atatumia yanayotokea sasa ku justfy kuwa aliundiwa mgogoro ili mbowe mtu wa kaskazini aendelee kuwa mwenyekiti
- Mbowe umeshafanya kazi kubwa sana na huhitaji sana kuwa mwenyekiti ili uweze kuendelea kutoa mchango wako ktk harakati za kuwakomboa watz maana CHADEMA ni timu na siyo individuals. Kwa hiyo ikiwa zito atafanya kweli epuka kupambana na zito katika nafasi ya mwenyekiti kwa kuwa lengo lake siyo kushinda bali kushindwa ili kushindwa huko kuwe mtaji wa kufanikisha mradi maalum wa kuibomoa CHADEMA. Chama kina watu wengi sana makini ambao misimamo yao wameshaonesha kwa vitendo, Lissu, Mnyika, Msigwa, Prof Safari, etc etc.
Wewe unayehitaji mabadiliko katika Tanzania unaishauri nini CHADEMA?