victor lenard
Member
- May 14, 2017
- 10
- 3
Wanasayansi wachanga wa shule ya Mbeya day wamefanikiwa kugundua kiti chenye magurudumu matatu kinachotumia Umeme kuendeshwa. Kiti hicho kina vitufe upande wa kushoto na kulia vinavyomuwezesha mlemavu kuelekea upande atakao, kiongozi wa kikundi hiki wanacho jiita Young Scientists anasema wameweza kugundua kiti hicho ili kupambana na changamoto wanazozipata walemavu, kikundi hicho kina wanafunzi 27 wakiwemo wavulana 17 na wasichana 10.