"Ugumu wa maisha" unaleta hasira?

"Ugumu wa maisha" unaleta hasira?

Ni kweli mkuu.. umepiga mule mule.! Mungu awafungulie milango wote wanaopitia changamoto za kifedha
Amina kaka... hakika wakati wa ugumu ni mateso makubwa
 
Kidogo kichwa kikipumzika mtu anaweza akafanya mipangilio maana amepunguza kwa kiasi kikubwa kuonekana public na kazi inabaki kufikiria namna ya kusimama Tena au kupumzika,,mfano kuandika barua tra kuhusu mkwamo ili wajue umestop biashara Yako kwa hio zile corporate tax,,anual return nk pia vipumzike unastop Kila kitu ili kama ni Kuja kuendelea iwe ni wakati Kuna uwezekano,,Nina Mzee wangu alijaribu kuforce king baada ya kampuni yake kupita misukosuko Sasa hivi stroke ndio imemrudisha ndani,,kwa sababu alishazoea kushiriki mambo mbalimbali hata kuwe na harusi 6/month atachangia zote na minimum utakuta kachanga 400k,,Sasa upepo mbaya ulipokuja hakutaka kurudi chini
Umenena vema sana... Uombe tu huko ndani kuwe na utulivu, usije ukakutana na maswali kutoka kwa mkeo yanayoumiza zaidi... "Utakaa ndani hadi lini?", "Kwanini usitoke kama wanaume wenzako?", "Wenzio wanapambana we umelala ndani?"... na mengine....
 
Kipi hasa huwa kunakufanya unakuwa rude Joannah? Unadhani sababu hasa huwa inakuwa ni nini?
Yaani hata sielewi Ni hormones gani huwa zinanipanda,nakua Nina hasira Sana,yaani kitu kidogo ninakuwa mkali Kama pilipili yaani hapo watoto wacheze kwa step maana hawakawii kulia
 
Juzi nilikutana na rafiki yangu ambaye tunashirikiana kwa mengi tu. Amekuwa ni mfanyabiashara kwa muda mrefu sana wa maisha yake. Hapa katikati, halihalisi imekuwa sio nzuri kibiashara, na ameyumba sana.

Pamoja na mengi ambayo tumekuwa tukisaidiana, kuna jambo moja ambalo nahisi sasa imekuwa tabia yake ambayo hapo awali sikuifahamu.

HASIRA
Siku hizi za karibuni hasa baada ya kuyumba sana kiuchumu, huyu bwana amekuwa na hasira zilizopitiliza. Kwenye kila ambalo tumekuwa tukijadiliana, iwe na mimi moja kwa moja au na wengine, jamaa amekuwa mtu wa kufoka kwelikweli!!! Na hii kumbe imeenda mbali zaidi hadi nyumbani kwake. Haambiliki!! Suala dogo tu linalomkwaza linaweza kupewa majibu zaidi ya kumi ya kashfa nzito nzito.

Tuliachana naye nikiwa nimekwazika sana. Baadae nilipoanza kutafiti tafiti juu ya tabia hii, ikaja bayana kwangu kuwa, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya UGUMU/ MKWAMO WA MAISHA na HASIRA.

Hisia pamoja na tafiti zangu zisizo rasmi zikanipa sababu kadhaa kuthibitisha hizi

1. Hofu ya kudharaulika
Ugumu/Mkwamo unakufanya kuwa na hofu ya kudharaulika. Hata wale unaowaamini unaamini kuwa wameanza kukudharau au kukusema vibaya. Katika kujilinda, mara zote unakuwa na hali ya kuchukia na kukasirika na hii inakupotezea kabisa uwezo wako wa kuhimili hisia zako, hivyo kufoka, ugomvi na kuchukia vinakuwa waziwazi kwako.

2. Kukosa kujiamini
Katika ugumu na mkwamo, unakosa kujiamini. Wewe mwenyewe unashindwa kujitetea hata katika mambo ya kawaida. Matokeo yake, hisia ya kuonewa inakuwa wazi. Inapotokea ukaulizwa jambo lolote hata kazini kisha ukashindwa, unahisi unakandamizwa. Hii pia inajenga hasira.

3. Kukosa majibu
Ugumu unakunyima majibu ya maswali rahisi kabisa. Mfano, mtoto anaweza kukuomba hela ya pipi, akiamini ni kitu kidogo MNO kwako. Unapojaribu katika hali hii kumwelewesha kuwa hauna kitu, huenda akaendelea kukughasi zaidi. Sasa fikiri hali hiyo akiwa nayo mkeo, na akaweka na yale maneno kama "yani mwanaume mzima unakosa hela ya kusuka tu"... Hakika huwezi kuacha kukosa hasira.

4. Kutengwa na jamii
Unapokwama zaidi kiuchumi, unashindwa kushiriki baadhi ya shughuli za muhimu kama misiba, harusi, vikao na mengine. Jamii haitakaa kuangalia changamoto zako, bali itaanza kukusema vibaya. Hii mara nyingi sana hulazimisha hasira!!

5. Wivu
Kukwama pia kunakufanya unakuwa na wivu. Wakati hujui familia yako inakula nini, rafiki zako wa karibu unawashuhudia "wakichezea pesa" kwenye vikao vya vileo, kamari na matumizi mengine ambayo kwako "sio ya maana", huwezi kufurahia. Lazima ujikute mwingi wa hasira tu.

6. Madeni yasiyolipika
Hakuna kipindi kibaya cha kuingia katika madeni yasiyolipika kama kipindi unapoyumba kiuchumi. Wakati yale ya awali bado yanakung'ang'ania, unalazimika kukopa upya mahitaji yoote muhimu ili uendelee "kuwepo". Matokeo ya haya ni pale unapoanza kudaiwa. Kuna wakati ni kama unahisi wanaokudai wanakudhihaki, na wanapotokea wale ambao sio wastahimilivu, hapo huna namna, lazima uwake kwa hasira.

7. Kauli Mbaya
Hebu zifikirie kauli hizi zinapoelekezwa kwako, tena wakati huna hata shilingi maishani, na bado majukumu yanakuandama.... Utatuambia nini? We nawe mwanaume mbele za watu? Sa' utakaa hivyo hadi lini? Si ukatafute kazi kama wenzio? Ina maana hujaona kazi za kufanya? Tukuvumilie kwani we kilema? Yani hela ndogo tu hiyo inakushinda? Hizo pamoja na kauli zingine zinazofanana nazo ni sababu tosha kabisa ya kukutia hasira.

8. Kutokusikilizwa
Sio kwamba watu wanakusikiliza mara zote kutokana na busara au nafasi zako. Tunataka busara zako ziendane na vitendo. Ukitushauri tufanye jambo, tunataka nawe uanze kufanya. Unapokuwa kwenye kukwama, kuna wakati hatutaki kusikiliza "ngonjera" zisizo na vitendo. Hili huwa linatia sana hasira.

9. Hofu ya kukosa uthibiti na utawala
Hii ni hofu nyingine mbaya mno!! Hali nzuri ya kiuchumi inatupa utawala na uthibiti juu ya watoto wetu, familia zetu, mali zetu na mengine. Unapokuwa na hali ya kukwama, kuna wakati huwezi kumuuliza mkeo sababu za kutokupika kwa wakati. Unapomuona akiongea na simu, unakosa ujasiri wa kuhoji. Unapomuona amevaa nguo mpya, unaishia tu kusononeka. Utauliza nini?? Unapata wapi ujasiri? Badala yake ni hasira tu itakayokuwa kimbilio

10. Msongo wa mawazo na sonona!!!
Baada ya yoooote ambayo nimejaribu kuyaainisha hapo juu, kukwama kunaweza kuleta msongo mkali wa mawazo na hatimaye, sonona . Katika hali hii ndipo hata wengine hufikia kujiua au kuyadhuru maisha ya wengine. Ni kama kila njia inakuwa haiwezekani. Mtu mwenye msongo wa mawazo hasiti kufanya lolote ovu kwakuwa anakuwa katika hali mbaya zaidi kimawazo, ikiwa ni pamoja na kuwa na hasira kali muda mwingi.

Naendelea kufanya utafiti zaidi kuona namna ya kuja na aina yoyote ya suluhisho kwa haya, lakini kwa kweli, njia ya uhakika kabisa ni kupata kazi na pesa, hata kama ni kidogo kidogo. Kuyumba kunavumilika, lakini kuna wakati kuanguka kabisa kunaweza kumpa mtu sababu ya kujiua.

Sijasema popote kuwa haya yanatokea kwa kila mtu na yanamwathiri kila mtu kwa ukubwa uleule. Ila kwakuwa kuna ambao yamewapata, sio vibaya tukayazingatia.

Wasalaam

Mwenye Kunoa Lubu!!!
Kwani ulikuwa hujui?
 
Kidogo kichwa kikipumzika mtu anaweza akafanya mipangilio maana amepunguza kwa kiasi kikubwa kuonekana public na kazi inabaki kufikiria namna ya kusimama Tena au kupumzika,,mfano kuandika barua tra kuhusu mkwamo ili wajue umestop biashara Yako kwa hio zile corporate tax,,anual return nk pia vipumzike unastop Kila kitu ili kama ni Kuja kuendelea iwe ni wakati Kuna uwezekano,,Nina Mzee wangu alijaribu kuforce king baada ya kampuni yake kupita misukosuko Sasa hivi stroke ndio imemrudisha ndani,,kwa sababu alishazoea kushiriki mambo mbalimbali hata kuwe na harusi 6/month atachangia zote na minimum utakuta kachanga 400k,,Sasa upepo mbaya ulipokuja hakutaka kurudi chini
Sure!!
 
Yaani hata sielewi Ni hormones gani huwa zinanipanda,nakua Nina hasira Sana,yaani kitu kidogo ninakuwa mkali Kama pilipili yaani hapo watoto wacheze kwa step maana hawakawii kulia
Inabidi kipindi hiki ukae mbali na silaha kwakweli...
 
Kwamba naweza jeruhi mtu?
Kabisa.. Katika kipindi kama hiki anaweza mtu na kauli yake ngumu kama vile: "Wenzio wanafanya kazi wanapata hela, we upoupo tu!!"... Kauli kama hii kama una silaha mkokoni unaweza kusababisha matatizo
 
Kabisa.. Katika kipindi kama hiki anaweza mtu na kauli yake ngumu kama vile: "Wenzio wanafanya kazi wanapata hela, we upoupo tu!!"... Kauli kama hii kama una silaha mkokoni unaweza kusababisha matatizo
😂😂😂😂Dah huyo Kuna kitu atakuwa anakitafuta kwangu
 
Ila Kuna watu Wana kauli mbaya Sana!
Ni kama mwanaume ambaye hana hata mia mfukoni, halafu mkewe amwambie "Niguse kama we mwanaume kweli!", au "Wakiitwa wanaume nawe utatoka!".... Ndio ile unaskia mtu kaua bila kukusudia...
 
Huko kunasababishwa na kukosa hekima pia kunasababishwa na maisha uliyoyaishi ukiwa unaukwasi

Navyojua mimi kama ulifanikiwa kuishi maisha yakawaida namaanisha uliendelea kuwa wewe yuleyule wa mwanzo kabla labda haujawa mkwasi kabla ujayajua maisha flan ambayo yalikufanya ukawa mtu wakuvimba kamwe huwezi pata hasira zisizokuwa na maana

Sikuzote mwanadamu mwenye hekima iliyo ndani yake ufanya mambo kwakuitumia haitegemei ni wakati gani

USHAURI: MUNGU ukifanikiwa kupata hela inatakiwa ujiandae kutokuwanazo pia kwakuwa hukuwanazo kabla endelea kuishi maisha kuwa yuleyule badilika tu kwenye mambo ya msingi yanayosababisha uendelee kiuchumi chamsingi nikuishi na watu vizuri

Usikubali pesa ikakubadilisha siku ukizikosa jambo lakwanza litakalo kutokea nikuishi maisha yalujificha hii itasababisha uendelee kukosa michongo ya pesa mwisho utakua mtu wa hasira na kuona kilamtu ni m baya kwako

Pesa huwa inapokujia kuwa makini huwa inakuja na mambo mengi sana kifo kilema Cha milele au kukosa watu wa msingi kwenye maisha yako usipokuwa nayo makini

Pesa inataka watu makini wanayojua namna ya kuipa heshima usikubali pesa ikakupa heshima siku ukiondoka itaondoka na heshima yote

Maisha yanaitaji ujue mambo matatu tu ya msingi (1)MUNGU
(2)Wewe binafsi (Mimi)
(3)Pesa
Jambo la kwanza nikumjua MUNGU na kumjua MUNGU yalustaili ujue mafundisho yake uwe Muislam au Mkristo ili umjue MUNGU yakupasa usome maandiko yake kwa utiifu na umakini yakupe maarifa yakujaze ujuzi na kutambua unapaswa kuishi namna gani

Mf: unaponunua simu dukani ndani ya box la hiyo simu lazima ukute kijitabu kimeandikwa user manual hicho kijitabu kinakuelekeza namna utaitumia hiyo simu. Ndivyo ilivyo utakapo soma kitabu Cha dini yako haijalishi ni dini Gani

Naposema wewe (Mimi) namaanisha ujitafute ujijuwe wewe ninani upo kwakusudi gani hapa duniani kila mwanadamu kwenye hii Dunia anakusidio lake lakuwepo hapa jua, tambua unapenda kufanya nini jua kipaji chako jitafute kijana

Naposema pesa namaanisha pesa niyamwisho kwenye maisha yako pesa zinakuja zenyewe umjua MUNGU na ukishajijua wewe ninani.
Kwanza jitambue wewe ninani jitafute
 
Back
Top Bottom