UGONJWA WA SONONA (DEPRESSION): Usiyoambiwa na jinsi ya kupambana na tatizo hili

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,926
7,961
depressed-woman.jpg

Neno ''depression'' limetafsiriwa katika maana nyingi katika lugha ya kiswahili, wakati mwingine hutafsiriwa kama msongo wa mawazo, huzuni au shinikizo la damu. Lakini maana halisi ya depression au sonona kwa lugha ya kiswahili ni ‘tatizo la kiakili’ ambalo humpata mtu kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha na za kimaumbile.

Ugonjwa (kasoro) huu humpata mtu yeyote yule aliyefikia umri wa kujitambua. Matukio ya kijamiii, familia, mahusiano na maisha binafsi pia yanaweza kuwa ni chanzo kikuu (trigger) cha tatizo hili; kwa maana ya kuwa yanaweza kusababisha tatizo hili kuanza kujitokeza. Mathalani pale mtu anapompoteza mtu muhimu katika familia au jamiii au mtu kukosa/kufukuzwa kazi, kuharibika kwa rasilimali zake au kupatwa na ugonjwa sugu kwa muda mrefu na hata kuvunjika kwa mahusiano kunaweza "kuamsha" tatizo hili.

Natambua uwepo wa mijadala kadhaa hapa JF (na mingine nimeiweka kwenye thread hii kwenye uchambuzi wangu), baadhi ni hii:

1) Dawa ya kuepuka msongo wa mawazo na sonona
2) Kwa wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo (sonona) vitamin B complex ni 'dawa' yenye msaada mkubwa sana! (ambayo sipendi kuwambia ni kweli kitaalamu)
3) Watu wanaokuwa na mawazo ya kujiua ni wa kuwasaidia...
4) Mdau mwingine alichambua vema hapa: Justification kwenye swala la huyu kijana aliyejirusha rock city mall

Sonona sio Msongo wa Mawazo

Ugonjwa wa Sonona (DEPRESSION) sio msongo wa mawazo (stress) kama ambavyo watu wengi hufikiri. Hata hivyo Msongo wa mawazo (stress) uliopitiliza au wa muda mrefu unaweza kusababisha Sonona.

Tatizo hili limekuwa likihusishwa pia na kasoro ya kimaumbile. Watafiti wa ugonjwa huu wameweza kugundua tofauti ya kimaumbile ya baadhi ya wagonjwa wa Sonona (Depression) na wasiokuwa na tatizo hili, wameonesha kuwa kuna baadhi ya wagonjwa wenye Sonona muundo wa ubongo wao una kasoro ambapo sehemu katika sehemu za ubongo itwayo Hippocampus ambayo ni sehemu ndogo sana katika ubongo. Sehemi hii huhusika na utunzaji wa kumbukumbu kuonekana kua ndogo kupita kiasi kinavyotakiwa hivyo basi kupelekea vipokeo vya serotonin (serotonin receptors) kuwa vichache na matokeo yake kushindwa kusafirisha na kutambua baadhi ya taarifa muhimu.

Aidha, utafiti mwingine unaonesha kuwa sehemu hii ndogo ya ubongo (hippocampus) inaonaonekana kuzalisha kwa wingi vichocheo vya mwili aina ya cortisol na hivyo husababisha kukandamiza na kuharibu kabisa baadhi ya vipokeo katika Ubongo.

Utamtambuaje mtu mwenye Sonona?

Mgonjwa/Mwathirika wa Sonona anaweza kuonyesha dalili kadhaa kati ya zifuatazo:-

> Kuwa na huzuni muda wote/mwingi

> Kukosa raha

> Kukosa hamu ya kula au kula kupita kiasi

> Kukosa usingizi wa kutosha au usingizi kukatika usiku na inakuwa vigumu (Insomnia)

> Kulala tena, au kulala sana na kushindwa kuamka asubuhi (anaweza kulala hata siku mbili mfululizo)

> Kutofikiri vizuri, kichwa kuwa kizito na kujisikia kama hawezi kufikiria chochote cha maana, hata kufanya maamuzi madogo inakuwa shida

> Hisia ya kukata tamaa ya maisha au kuwaza/kutaka kujiua (Soma pia Sababu zinazowapelekea Watu kufikia hatua ya kujiua)

> Kujilaumu/kujiona mwenye hatia/makosa

> Kutojiamini

> Kujiona hafai maishani/kama mtu wa kushindwa au kufeli katika kila kitu

> Kukosa hamu mambo uliyokuwa ukiyafurahia awali kwa mfano, hamu ya tendo la ndoa, kukaa na marafiki, kusikiliza muziki n.k

> Kutokuwa na hamu/utayari wa kufanya vitu vya kawaida ambavyo alikuwa anafanya kila siku kama vile kuoga, kufanya usafi wa mahali anapoishi, kwenda kazini, shuleni au sehemu ya kujipatia kipato.

> Pia anaweza kulalamika kuwa anasikia sauti za watu ambao hawaonekani (mfano sauti zikimwambia kuwa yeye hana thamani, yeye ni wa kufa tuu, ni bora tu ajiue, na kadhalika). Mfano mmojawapo ni mdau aliyejieleza hapa - Masaada wa haraka kabla hali haijawa mbaya zaidi

> Kuwa na wasiwasi bila sababu ya msingi

> Anaweza kuwa na ongezeko la utumiaji pombe au wa dawa za usingizi/za kulevya kama valium, heroin, cocaine, bangi n.k

> Kukaa peke yake/kujitenga/kutostahimili usumbufu/kelele hata kidogo

Ni bahati mbaya sana pia kuwa mara nyingi hali hii ya Sonona mara nyingi hugundulika wakati mtu akiwa amefika hatua za mwisho kabisa... Kwa mfano pale anapojaribu kujiua (suicide attempt). Pia, mtu akifika katika hatua hii inahitajika pia nguvu kubwa zaidi ili kumtoa huko na hata uwezekano wa kufanikiwa kumtoa katika hali hiyo pia unapungua. Hivyo basi, ni muhimu sana ukiwa na wasiwasi kuwa ndugu au rafiki yako anaweza kuwa na shida hii, uweze kufanya kitu mapema sana, bila ya kuchelewa.

Kesho tutaangalia jinsi ya kupambana na Sonona
 
Yupo bwana mmoja alisimamishwa kazi, ikatokea wakatofautiana na mkewe kwa sababu ya kushuka kipato cha yule bwana, jamaa akaona kuepusha shari bora akakae kwao na mama yake, mama nae akaona mwanae kawa mzigo, ingawaje hiyo nyumba ambayo mama anaishi alijengewa na huyohuyo mwanae aliyeporomoka kiuchumi, mama akawa anamtamkia maneno ya kumfedhehesha mtoto wake.

Bwana yule kuna nyakati namkuta kajiinamia analia, kwakuwa ni mshikaji basi namchukua tunatoka kutembea hapa na pale, anachangamka, akirudi nyumbani mama yake ni kumpa mineno ya kishenzi shenzi, jamaa anavurugwa upya, mpaka akawaza kama huenda yule si mama yake, nikamwambia mwamba yatapita.

Kweli yakapita baada ya miaka miwili ya msoto heavy, mwamba karudishwa job, katupa jongoo na mti wake, hana mpango na mke wala mama mzazi, mkitaka mgombane mwambie awasamehe hao watu wawili.
 
Back
Top Bottom