Ugonjwa wa ‘Phobia Attack’ ambao huenda ulimkumba Naibu Waziri mteule wa Madini , Francis Ndulane na kupelekea kushindwa kuapa

w0rM

Member
May 3, 2011
68
164
Mheshimiwa kwa namna ya kipekee nikupongeze kwa uteuzi bora kabisa wa Mawaziri na Manaibu Waziri wapya ambao ni vijana wasomi ambao kwa jicho la tatu watakusaidia sana katika kujenga Taifa hususan kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo.

Mheshimiwa Rais leo nimeshuhudia moja Kati ya wateule wako Bw. Francis Ndulane akishindwa kuapa kutokana na sababu ambazo hakuna aliyeweza kuelewa kwani mheshimiwa kwa kuangalia wasifu wake tayari alishakuwa Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Mji Ifakara ambapo alihudumu hapo kwa muda mrefu mpaka anaamua kwenda kwenye masuala ya siasa.

Mheshimiwa Rais, kitaalam kuna uwezekano mkubwa wa jambo hili kutokea hasa inapotokea ugeni kwenye nafasi kubwa kama aliyopata mheshimiwa Ndulane.

Kuna kitu kinaitwa...."PHOBIA ATTACK"

Phobia Attack Imegawanyika katika makundi 3. Ambayo ni;
A. Social phobia
B. Specific Phobia
C. Agoraphobia

A-Social phobia.
Huwakuta wengi, pale unapotakiwa kufanya Jambo Mbele ya Jamii, Hofu inapitiliza na kushindwa kufanya jambo au mabadiliko ya mwili, Pressure inapanda, una Sweat, na pumzi kukata. Huwezi kufanya lolote. (Hii ndo ninahisi imemkuta Mh. Ndulane)

B-Agoraphobia
Humkuta yeyote ukiwa mazingira yasiyo salama anayohofia Maisha yake hata na familia yake. Mfano Uingie mahali Kuna Wanyama wakali.

C-Specific Phobia
Hofu hupanda kutokana na Jambo ambalo hukutegemea Sehemu husika. Baadhi ya Wanaume huwatokea yupo na Binti ambaye haamini angeweza kumpata na anashindwa hata kuongea. (Normal blood circulation interrupted). Au Chumba cha mtihani, unashindwa kuandika/kujibu mtihani ilhali ni maswali hayo huyajibu kila siku.

Hivyo basi:
Naomba kuchukua nafasi hii kwa heshima na taadhima Mkuu wangu wa nchi, kumuombea msamaha Francis Ndulane ili aweze kuendelea na uwajibikaji katika nchi yetu penda.

Sina maslahi nae Simjui kifamilia lakini ninahisi amepata shida za kibinadamu za namna nilizoelezea hapo juu.

Dhana za kutokujua kusoma Inawezekana ni sahihi ila sio sababu kubwa sana kuliko ukweli wa aina ya hofu ziwakutazo BINADAMU.
 
Kama kashindwa kupambana na ile hali atawezaje issue za madini? ndio point ya mkulu
 
Hii ilimkuta hata Barak Obama, pale aliposhindwa kutamka vyema maneno ya kiapo nadhani hiyo ni katika term yake ya pili ya uraisi, hadi ikabidi siku ya pili aapishwe tena the white house nje ya kadamnasi.

Mambo hayo yanatokea, wenye busara wangalimfanya aape mwishoni.
 
Nishaona mtu anashindwa kupresent paper aliyoandaa mwenyewe, ile ni hali ya kawaida hasa kwa mtu anayefanya mara ya kwanza, kizungu wanaita stage flightening, aliyemteua ndio alikosea alipaswa kutambua yule ni mara ya kwanza anaapa kwa nafasi ile hivyo msongo unakua mkubwa
 
Hii ilimkuta hata Barak Obama, pale aliposhindwa kutamka vyema maneno ya kiapo nadhani hiyo ni katika term yake ya pili ya uraisi, hadi ikabidi siku ya pili aapishwe tena the white house nje ya kadamnasi.

Mambo hayo yanatokea, wenye BUSARA wangalimfanya aape mwishoni.



Hako kaneno kanafikirisha sana
 
We Baki hivyo hivyo.
Tunguri zipo na zinafanya KAZI.
Au unataka kusema cheo alichopewa ni kikubwa kuliko uwezo wake ndo maana ameshindwa kujiamini?
 
Na degree yake inaenda kukaguliwa, dah! so sad...kama ndo ana hiyo Phobia mbaya hivyo alipigaje kampeni?
 
Back
Top Bottom