Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,106
2,000
Hii sasa ni kali.

Awali Naibu waziri wa fedha ilibidi arudie kula kiapo zaidi ya mara 5 kwa sababu sehemu iliyoandikwa "Baraza la Mawaziri" yeye alitamka " Baraza la Mapinduzi"

Kali ya mwaka ni huyu Naibu waziri wa madini Francis Ndulane ambaye amekuwa akisoma kiapo huku akitetemeka na hivyo kuwekwa pembeni ili waapishwe wengine.

Wakati wa hotuba yake Rais Magufuli amesema atateua Naibu waziri mwingine wa madini baada ya Francis kufeli kula kiapo.

Sijajua manaibu waziri hawa wana mchecheto gani!

Maendeleo hayana vyama!

Updades: Rais Magufuli ateua Naibu Waziri wa Madini Mwininge
= > Rais John Magufuli amteua Profesa Shukrani Manya kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Madini, baada Francis Ndulane kushindwa kuapa
 
Davan

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
1,127
2,000
Hii imetokea leo ambapo naibu waziri Fransis Ndulano alishindwa kusoma vizuri hati ya kiapo akapewa nafasi ya kurudia bado akawa anakwamakwama hadi akaambiwa akakae kwenye kiti chake. Sijui ataapa siku yingine au ndio kibarua kimeota nyasi. Sasa sijui ni uoga au wamemroga.
Fundisho:
Tuwafundishe watoto wetu kujiamini pamoja na elimu walizo nazo confidence ni muhimu.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
22,753
2,000
Hii imetokea leo ambapo naibu waziri Fransis Ndulano alishindwa kusoma vizuri hati ya kiapo akapewa nafasi ya kurudia bado akawa anakwamakwama hadi akaambiwa akakae kwenye kiti chake. Sijui ataapa siku yingine au ndio kibarua kimeota nyasi. Sasa sijui ni uoga au wamemroga.
Fundisho:
Tuwafundishe watoto wetu kujiamini pamoja na elimu walizo nazo confidence ni muhimu.
Hiyo hutokea ukiwa na kiwewe, inaweza kumtokea mtu yeyote, halafu video iweke hapa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom