Ugonjwa wa kuku nisio uelewa

Ugonjwa wa kuku nisio uelewa

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,473
Reaction score
4,007
Mwenye kujua huu ugonjwa wa kuku kifaranga kuvimba miguu anisaidie kujua aina ya ugonjwa na dawa yake.
 
Attachments

  • 20250822_075331.jpg
    20250822_075331.jpg
    276.3 KB · Views: 27
  • 20250822_075239.jpg
    20250822_075239.jpg
    592.6 KB · Views: 28
  • 20250822_075234.jpg
    20250822_075234.jpg
    626.1 KB · Views: 29
Huo ugonjwa unaitwa kwa kingereza Bumblefoot au uvimbe wa miguu. Unatokana na maambukizi ya bacteria baada ya kuku kujikwaruza au kuumia, au sakafu ngumu kwa mda mrefu. Msafishe na maji ya vuguvugu yenye chumvi na umpake dawa ambayo ni antibiotic. Usafi wa banda/mazingira muhimu
 
Mkuu jina la ugonjwa huwa linanitoka maana ni kimombo lakini chanzo hasa ni kuku wako wanalala kwenye sakafu hakuna maranda ama matandazo japo pia hutokea kwa sababu ya uchafu wa banda.

Tiba za kitaalamu.
safisha kidonda kwa maji yenye dawa mfn Iodine dilute.
wape kuku Tylosin au OTC.

Tiba Kienyeji
chukua majani ya mwarobaini changanya na alovera kisha yatangwe kwa pamoja na baada ya hapo osha sehemu ya kidonda kwa maji hayo.

Fanya hivyo baada ya kuosha kwanza kwa maji ya vuguvugu na chumvi kiasi safisha kisha utumi huo mchanganyiko wa alovera na mwarobaini.

Kinga

Usafi wa banda.
Wape virutubisho hasa premix zenye Vitamini A,E NK
 
Bumblefoot! Umemsaidia lakini anaweza kutumia Epson salt (inapatikana kwenye maduka ya dawa za mifugo wanaowela kwenye maji ya uvuguvugu na anazamisha miguu ya kuku humo. Magamba yakishaloana na kulainika unayabandua kisha unasafisha vidonda vizuri na kuweka ile dawa ya alamycin 10% OTC spray. Mengine umeeleza vizuri!
 
Bumblefoot! Umemsaidia lakini anaweza kutumia Epson salt (inapatikana kwenye maduka ya dawa za mifugo wanaowela kwenye maji ya uvuguvugu na anazamisha miguu ya kuku humo. Magamba yakishaloana na kulainika unayabandua kisha unasafisha vidonda vizuri na kuweka ile dawa ya alamycin 10% spray. Mengine umeeleza vizuri!
Elimu haina mwisho mkuu hata mimi bado mwanafunzi......Nimejifunza kwako pia.Ahsante sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom