Ugonjwa wa Corona umevunja Muungano au Afya sio suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Kwanza nilikili kuwa Mimi ni muhanga wa kuusikia Muungano kwenye masikio ya watu tu na kusoma kidogo kweny somo la civics kidato cha tatu.

Pia nikili kuwa baadhi ya vitu nilivyoundishwa kuwa ni vya muungano nimeanza kuvisaau kutokana na muda nilio maliza shule lakini pia kutokana na mapmbano ya maisha.

Hivi ni muhimu mimi kukumbuka vitu vya muungano na visivyo vya muungano?

Any way go to the point, hivi jambo la afya ni suala la Muungano? Kama sio au ndio kwa nn taarifa za corona za TANGANYIKA na Zanzibar hazitangazwi pamoja?

Kama si suala la Muungano kwanini lisiwe sasa hasa wakati huu wa janga la ugonjwa wa corona?

Naomba elimu wana jf.na maoni yenu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii thread inaonyesha wewe siyo Great Thinker na huaistahili kuwa kwenye hili Jukwaa. Kama Unaweza ifute mapema maana ni kielelezo kuwa wewe ni MBURURA au KIAZI kama BASHITE.

Afya siyo suala la Muungano.
Hiyo ipo wazi sio suala la Muungano.

Ila ni kwa nini sio la Muungano?
 
Jikite kwenye kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na Virus vya Corona kwa namna yoyote bora na halali. Achana na mambo ya Muungano kwa sasa!
 
Mkuu, unachouliza ni Sawa na uko mlimani unauliza mawe kwamba hivi huwa yanarangi gani!!

Unategemea nini ikiwa Zanzibar ina waziri wa Afya? Kazi ya waziri wa Afya Zanzibar kazi yake ingelikuwa ni nini sasa

Jibu fupi ni kwamba, ingawa umesema kwamba vitu vya muungano na visivyo vya muungano huvikumbuki, basi weka na Hilo akilini, kama ulikuwa unakumbuka mawili ongezea na Hilo yafike matatu
 
Kweli muungano wetu ni wakilaghai, watanzania wengi hawajui hata kwanini tuliungana, eti kwasababu ya 'undugu wetu', wamasai na wanyakyusa wana undugu gani na wapemba? .
 
Hii thread inaonyesha wewe siyo Great Thinker na huaistahili kuwa kwenye hili Jukwaa. Kama Unaweza ifute mapema maana ni kielelezo kuwa wewe ni MBURURA au KIAZI kama BASHITE.

Afya siyo suala la Muungano.
Mkuu hii lugha mbona kali sana? si ameuliza tu?
 
Kwani upo? Muulize johnthebaptist asipokuambia kazi ya muungano ni kuwachagulia Zanzibar rais wao tu wakati wanapokaa kule Idodomia. Baada ya hapo kila mtu na 45 zake. Hizo 10 zinakuwaga kule bungeni wakati wa kupitisha bajeti ya Tanganyika tu.
 
Back
Top Bottom