Ugonjwa Uliosahaulika!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa Uliosahaulika!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Sizinga, Jun 20, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Mara ya mwisho niliusoma huu ugonjwa wakati nipo shule ya msingi,zaidi ya miaka 20 iliyopita!! Huu si mwingine ni ugonjwa wa Tauni. Sijafahamu bado scientific name yake lakini ni ugonjwa unaoambukizwa na jamii flani ya Panya. Ukiumwa na Panya basi upo hatarini kuupata huu ugonjwa.

  Inasadikika kwamba huu ugonjwa ukifika mapafuni( Tauni ya mapafu) hauzidi zaidi ya masaa 8 kabla hujabadilishwa jina na kuitwa Marehemu. Ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya hewa toka kwa mtu mmoja na kwenda kwa mwingine. Kwa maneno mafupi niseme ivi, kama kuna mtu anayeumwa tauni ya mapafu amepanda basi(bus) kwa umbali wa masaa zaidi ya 10 basi abiria woooote katika lile basi watashuka wakati wameambukizwa huu ugonjwa!!

  Na tayari huko Tanga kwa current news umeshaua watu 680 hadi sasa hivi, na watu zaidi ya 7000 wameshaupata huu ugonjwa. Tunashauriwa kuua Panya majumbani kwa zaidi tuwezavyo, ni hatari. Chukua hatua!!
   
 2. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haujasahaulika mkuu. Unaitwa Plague. Unasababishwa na bacteria anaitwa Yersinia pestis. Unaenezwa na viroboto (fleas) vinavyokaa katika mwili wa panya. Plague ni ugonjwa wa panya. Binadamu anaupata baada ya kuumwa na kiroboto kilicho na bacteria. Kiroboto anapata bacteria kutoka kwa panya mwenye plague. Kwa hiyo plague mara nyingi ni zoonotic. Zoonotic ni ugonjwa wa wanyama ambao unaweza kumpata binaadamu pia.

  Panya wahusika wakubwa wanaitwa Rattus rattus na Rattus norvegicus. Haya ni majina ya kisayansi. Viroboto vinavyohusika zaidi ni aina ya Xenopsylla cheopis.

  Plague unaweza ukajitokeza kama
  • Ugonjwa wa mapafu (pneumonic plague): unaua sana na haraka
  • Ugonjwa wa tezi (bubonic plague)
  • Ugonjwa wa ngozi (pestis minor)
  Ugonjwa huu si mgeni. Uliwahi kuua robo ya wakaazi wa Ulaya kwenye karnne ya 15.

  Kwa Tanzania, ugonjwa huu hulipuka mara kwa mara huko Lushoto.

  Ni ugonjwa hatari sana kwa sababu huua sana na haraka, ingawa kuna matibabu. Baadhi ya dawa aina ya antibiotics zinaweza kutibu.

  Kwa kifupi huu ndiyo ugonjwa wa tauni (plague)

  Ukitaka kuujua zaidi, google 'plague'
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  Usikumbuke shida kumbuka zaidi maisha bora kwa kila mtz.
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Dah!mkuu Sizinga umenikumbusha mbali sana, huu ugonjwa ungesababisha wilaya nzima ya lushoto iangamizwe kwa bomu ili kuepuka huu ugonjwa kusambaa nchi nzima, miaka ya 1986s ndo ulishika kasi sana, yaani kulikuwa na mageti kika kijiji, mimi natokea mlalo, ila wale wanaotokea eneo moja linaitwa SHUME ndo waliathirika zaidi, yaani nyumba kwa nyumba mnawasiliana kwa dirishani, kama sio busara za nyerere tusingekuwepo leo, wamarekani walimshauri Nyerer kuangamiza wilaya nzima, Nyerere akakataa, walikuja madokta toka marekani, mmoja au wawili kama sikosei walikufa kwa ugonjwa huo kule shume.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. A

  ADK JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,147
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Tuombe mungu yasirudi tena
   
 6. m

  monjoshy Member

  #6
  Aug 18, 2013
  Joined: Dec 25, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Je? Panya akikung'ata kunauwezekano wa kupata ugonjwa huu?
   
Loading...