Red black
JF-Expert Member
- Nov 29, 2019
- 18,159
- 58,696
Ulichoelezea ni side effects ambayo ni vaccination failure which occur if the vaccine is admistered wrong/improperly and if the chicken is not healthy at the time of vaccination.Mkuu; Atakuja mwenyewe Jerry Farm kukufafanulia lakini nakushauri uridhike na alichokuambia kwamba kuku hutokea hawezi au anapata shida kuhimili virus aina tatu kwa wakati mmoja. Yan hiyo chanjo ni Live- attenuated virus i.e. imebeba kwa pamoja virusi Hai vya ndui, newcastle (mdondo/kideri) na Fowl coryza vilivyo hafifishwa nguvu/uwezo au tuseme vimenyong'onyeshwa. Kazi ya vaccine aina hiyo ni kuushtua mwili ili ujitengenezee kinga. Hapo manake kuku anapewa uambukizo (virus) makusudi halafu mwili wa kuku unatakiwa upambane navyo na kuvishinda na hivyo kujijengea uwezo (kinga) ya kupambana tena endapo kutatokea uambukizo wa virusi vya aina hiyo ambavyo ndo Uganjwa halisi. Sasa kuku huyo mmoja anapewa kwa makusudi virusi vya aina tatu kwa wakati mmoja(Chanjo) na mwili unatakiwa upambane navyo na kuvishinda. Huo ni mzigo mkubwa na katika hali hiyo kuku anaweza kuwa ni mdhaifu na hivyo huchoka na kuzidiwa na virusi alivyowekewa (chanjo)japokuwa vimehafifishwa nguvu (attenuated). Kama kuku hatoweza kuhimili kishindo cha hiyo chanjo basi anaweza kufa. Lakini hebu kuwa na subra Jerry farms atakupa kwa undani kama unavyotaka:
what is a vaccine? na explain in short types of vaccine.(Ila ujue ni somo refu) Ni hayo tu.
Concurrent d'se , immune stress