Ugonjwa gani huu uliowapata kuku?

Ugonjwa gani huu uliowapata kuku?

Jhany97

Member
Joined
Feb 25, 2025
Posts
11
Reaction score
15
Wataalamu naombeni msaada huu ugonjwa naona ni mgeni kwangu vifaranga wanavimba macho na midomo alafu sio kama ile coryza uvimbe wake ni mgumu hautoi chochote ukibinya na sio kwamba hii ni ndui na ni vifaranga wote wa umri huu, msaada please kwa anaeufahamu huenda ni mpya. picha zake hizi👇
IMG_20250326_100723_497.jpg
IMG_20250326_100747_739.jpg
 
Wataalamu naombeni msaada huu ugonjwa naona ni mgeni kwangu vifaranga wanavimba macho na midomo alafu sio kama ile coryza uvimbe wake ni mgumu hautoi chochote ukibinya na sio kwamba hii ni ndui na ni vifaranga wote wa umri huu, msaada please kwa anaeufahamu huenda ni mpya. picha zake hizi👇View attachment 3283647View attachment 3283648
Mkuu; Usitake ndui ije au iwe kama ulivyosikia au unavyotaka iwe. Hapo kuna vitu viwili. Vit. A deficiency na ndui.
Ukifungua jicho na kubinya kidogo utaona utando mweupe ulioganda chini ya kope na hivyo vidonda uvimbe baadaye hubanduka na kuacha kidonda kibichi. Kuku hatopenda kula na huwa haoni chakula kutokana na macho kuvimba/kujifunga. Infectious Coryza haiko hivo -yenyewe huwa ni mafua makali hadi kuku anashindwa kupumua na huweza kutoa kasauti fulani wakati anapumua kwa shida.
 
Kiongozi samahani inawezekana vipi hawa vifaranga kupata ndui angali hakuna mkubwa hata mmoja mwenye dalili hizo?
 
Wapake mafuta ya nazi / asali au iodine

Wape dawa ya oxytetracycline

Wape maji yenye vitamin na usisahau majani kama lishe

Note . Usifuge kuku kama utashindwa wapa chanjo ya ndui , kideri na gumbolo.
Wapake mafuta ya nazi / asali au iodine

👆akikosa hivyo vyote atumie mafuta ya taa na wound powder.
 
Hawa muda wa kuwapa fowlpox vaccine bado mkuu kama unavyoona
Wapake mafuta ya nazi / asali au iodine

Wape dawa ya oxytetracycline

Wape maji yenye vitamin na usisahau majani kama lishe

Note . Usifuge kuku kama utashindwa wapa chanjo ya ndui , kideri na gumbolo.
 
Oxytetracycline Powder+Multvitamins Kwa Wagonjwa Mpaka Watakapo Kaa Sawa, Na jitahidi Uwatenge Na Ambao Bado Hawajadhurika Na Ugonjwa Ili Kukotroo Maambukizi Zaidi
 
Ukisema ni kideli niwape chanjo mbona ninavoelewa mm kwa uelewa wangu mdogo kuku akiwa na maambukizi hatakiwi kuchanjwa? Dada coca
Kideli.
Nunua dawa ya matone, wanyunyizie machoni, watapona kwa uharaka mno.
 
Back
Top Bottom