GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,571
- 108,925
“ Matukio ya Utekaji nchini Tanzania ni Utamaduni mpya usiokubalika, Wastaafu tusijione Shughuli ziliisha “ ( Chanzo Taarifa: MillardAyo.com )
" Suala la utekaji au Watu kupotea linaweza kuiharibia Nchi yetu heshima Duniani, linaweza kuiondolea Nchi yetu hali ya usalama ambayo tulikuwa nayo tangu tupate uhuru lakini pia hali inaweza kujenga chuki kubwa sana ya Wananchi dhidi ya Serikali popote Duniani " ( Chanzo Taarifa: MillardAyo.com )
" Hili Suala la Utekaji lisipokemewa sasa litakuja Kufika hadi katika Uchaguzi ambapo hapo linaweza kusababisha taswira ya nchi Kuharibiwa kwani wapo ambao hawatakubaliana nalo na watakuwa tayari kwa lolote lile " ( Chanzo Taarifa: MillardAyo.com )
Tukumbuke kuwa huyu Membe aliwashawahi kuwa Ofisa Usalama ( Jasusi Mwandamizi ) kabisa ndani ya Taasisi Nyeti ya Usalama wa Taifa nchini ( TISS ) hivyo kama na Yeye leo hii amefikia Kutovumilia na Kuyasema haya tena hadharani na bila Kificho wala Unafiki basi Wahusika wote au wale Maduduna ( Wapumbavu ) wachache wanaoratibu huu Upuuzi wajitathmini na wakiweza waende haraka katika Nyumba zao za Ibada Wakatubu Ukatili wao walioufanya kwa Watanzania wenzao au hata Wageni kabla Kofi la Kiama la Mwenyezi Mungu halijawashukia.
Sina tatizo na IQ yake Mzee Membe na najua ya kwamba ni Mmoja wa Watu walioshiba kama siyo Kukomaa kabisa na Udiplomasia na bahati nzuri hata huo Udiplomasia wenyewe anauweza na unampenda vile vile kuliko wengine ambao huu ni mwaka wa Tatu unaenda wa Nne hawana hata Robo Tatu ya Udiplomasia japo wanaulazimisha, ila katika Suala ya Yeye kutaka kuwa Rais wa JMT hapo ndipo nitamkatalia kutokana na sababu zangu kadhaa ila kwa leo siyo mahala pake kwa Mimi kuzitaja hapa.
Nami namalizia pia kwa kusema Wastaafu nchini Tanzania hasa wale Viongozi na waliowahi Kuongoza Taasisi na Idara Nyeti nchini Tanzania tambueni kuwa kwa kuwa bado mpo Hai basi nyie bado mnatakiwa Kupaza Sauti zenu na ikibidi hata Kuwakemea hawa Maduduna ( Wapumbavu ) wachache wanaochafua Taasisi zenu ambazo mliziongoza vyema na hazikuchafuka kama ilivyo sasa.