Uganda yatangaza kufanyia marekebisho njia ya umeme hadi Kagera!

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
495
375
Serikali ya Uganda imetangaza kuanza matengenezo ya njia ya umeme kutoka uganda hadi Kagera kwa muda wa miezi 40, ili kupunguza hisia za hujuma ambazo pengine zingenaswa na Tanzania, Uganda imesema itakuwa inakata umeme kuanzia IJUMAA-JUMA PILI, kwa maana kuwa Wakazi wa Kagera watapata umeme kuanzia JUMA TATU-ALHAMIC Tu.

Lazima serikali yetu kuanzia sasa iamke kutoka usingizini ifanye kazi usiku na mchana ili Tanzania iwe moja ya nchi Imara sana katika Afrika kiuchumi, Kisiasa na kijeshi, Hatuna sababu ya kuendelea kununua umeme nchi nyingine.
 
Bado kenya sasa,sijui nao wataamkia Namanga?lakini hivi yote haya yanatokana na ile kauli ya kikwete dhidi ya kagame tu?au kuna kingine kilichojificha?sijui burundi nao wanawaza nini saa hizi?
 
Kwa Taarifa miezi 40 ni sawa na miaka 3 na miezi 4, hapa ndo serikali yetu ijifunze kutumia akili, Raslimali, iwajibike kwa wananchi wa tanzania katika kufanya kazi kwa bidii ili Nchi yetu iwe na uchumi imara, idhibiti mianya yote ya ubadhirifu, napenda sana kama Tanzania itaongoza kuwa na uchumi imara sana Afrika, hata hawa wenzetu watatuonea gere tu!
 
Hadi umeme tulikuwa "tumeomba kusaidiwa"?...

Tanzania hununua umeme Uganda kwa ajili ya nishati kwa mkoa wa Kagera, hununua umeme Zambia kwa ajili ya nishati kwa Sumbawanga, vivyo hivyo hununua umeme Kenya kwa ajili ya eneo moja la wilaya mojawapo ya ama mkoa wa Arusha au Kilimanjaro (sikumbuki vizuri hili).

Nasi kama nchi, Nishati ya Mtwara itaweza kuziuzia nchi takriban zote za Afrika zinazotuzunguka na hata ng'ambo. Kutakuwepo na ziada kubwa ya nishati itakayopatikana pale kusini.
 
...hivi huyu jamaa si pinda kasema mukulu kampigia magoti atuombee suluhu..? mbona kila habari na muelekeo wa mambo kilasiku unaonekena kinyume na matarajio yetu..? hii mijamaa m7 na pk inaonekana ina siri nzito sana, na kama jk kagusa maslahi yao basi kagusa pakubwa, sio bure...
 
Sasa mimi naona wamefanya vema hawa waganda..ili serikali ya JK iamke.
 
Tanzania hununua umeme Uganda kwa ajili ya nishati kwa mkoa wa Kagera, hununua umeme Zambia kwa ajili ya nishati kwa Sumbawanga, vivyo hivyo hununua umeme Kenya kwa ajili ya eneo moja la wilaya mojawapo ya ama mkoa wa Arusha au Kilimanjaro (sikumbuki vizuri hili).

Nasi kama nchi, Nishati ya Mtwara itaweza kuziuzia nchi takriban zote za Afrika zinazotuzunguka na hata ng'ambo. Kutakuwepo na ziada kubwa ya nishati itakayopatikana pale kusini.
maelezo kuhusu nchi yetu yanapendeza sana kuyaongea lakini ukija kwenye utekelezaja ndipo machozi yaweza kukutoka. Mfano kabla ya kufikiria juu ya gesi ya Mtwara ambayo Serikali kupitia kwa waziri Prof. Mhongo imeshasema wazi wananchi ni watazamaji, tuangalie tangia hiyo ya Songosongo imeanza kuchimbwa imeleta neema kiasi gani kwa Mtanzania aina ya Rock City na mimi?
 
Safi sana kwa kufanya hivyo labda viongozi wetu mapoyoyo wanaweza kuamka toka usingizi
 
Sio kwamba tunaomba, tunanunua. Ununuzi wa umeme toka nchi jirani ni jambo la kawaida sana hasa kama majirani mnaelewana.

Mkuu umeme wa Uganda ulikuwa wa uhakika hauna longo longo kama huu wa grid ya taifa, ulikuwa ni nadra sana kukatika.
 
Kwa Taarifa miezi 40 ni sawa na miaka 3 na miezi 4, hapa ndo serikali yetu ijifunze kutumia akili, Raslimali, iwajibike kwa wananchi wa tanzania katika kufanya kazi kwa bidii ili Nchi yetu iwe na uchumi imara, idhibiti mianya yote ya ubadhirifu, napenda sana kama Tanzania itaongoza kuwa na uchumi imara sana Afrika, hata hawa wenzetu watatuonea gere tu!
Kamwe hapo kwenye red akili ile ile iliyoleta tatizo haiwezi kutatua tatizo hata siku moja,chini ya masisiem sahau huo uchumi imara mkuu,ukiwa fisadi,muuza unga kama iddi,mkwepa kodi,muhujumu uchumi,jangili kama kinana,fisadi waliasili na uchafu mwingine mwiiingi wa kurudisha maendeleo nyuma wewe vaa nguo ya kijani tu na pita barabarani ukisema "kiguuuuuuuuuuuumu chama cha majangili" utafurahiwa sana na kuishi kama peponi hapa nchini...tunahitaji ukombozi na fikra mpya kabisa!!
 
Serikali ya Uganda imetangaza kuanza matengenezo ya njia ya umeme kutoka uganda hadi Kagera kwa muda wa miezi 40, ili kupunguza hisia za hujuma ambazo pengine zingenaswa na Tanzania, Uganda imesema itakuwa inakata umeme kuanzia IJUMAA-JUMA PILI, kwa maana kuwa Wakazi wa Kagera watapata umeme kuanzia JUMA TATU-ALHAMIC Tu.

Lazima serikali yetu kuanzia sasa iamke kutoka usingizini ifanye kazi usiku na mchana ili Tanzania iwe moja ya nchi Imara sana katika Afrika kiuchumi, Kisiasa na kijeshi, Hatuna sababu ya kuendelea kununua umeme nchi nyingine.

siyo miezi 40 ni wiki 40
soma hapa

https://www.jamiiforums.com/habari-...-mgao-wa-umeme-wa-uganda-kwa-mwaka-mzima.html
 
Ni wiki 40 miezi kumi siyo miezi 40 mzee. lakini ni Ijumaa hadi Jumapili kila wiki.
 
Msipotengeneza mazingira ya kujitegemea, mtaendelea kulalamika tu. Freedom without economic and social independence is but Neo-Slavery
 
Hata kama ni wiki 40, mwezi mmoja una wiki= 4, je wiki 40 ina miezi mingapi= miezi kumi 10 kamili, bado uchumi wa kagera utayumba tu,
 
Mleta mada atakua kakosea, sio miezi 40. Nina wasiwasi coz nahisi ilitangazwa wiki 40 ambazo kama sijakosea ni miezi 10 net!
 
wote wajinga na tuwafukuze wote halafu tubaki na watu wetu tujue namna ya kuwahudumia watu wetu.
 
Back
Top Bottom