Uganda Vs Rwanda kimenuka


Very true Mungu aepushie mbali tatizo hili. Rwanda kwanini walikuwa wanateka Uganda na kurudisha Rwanda? Kwanini PK anaamini Museveni anamsaidia Gen. Kayumba?
Sisi tuwe neutral. Kuna faida nyingi kuliko hasara.
 
Wakianza kuzichapa mimi nitaenda kupigana kumsaidia museveni maana simpendi mwizi kagame hata kama magufuli atamsaidia kagame
 
Jiwe ataweza kusuluhisha huu ugomvi? Au atamtuma Mkapa ambaye tayari mgogoro mdogo wa Burundi umemshinda?
 
Hili jambo sio jepesi kama vile tunavyolijadili humu, na ukizisoma baadhi ya comments hapo juu unaona kabisa kuna tofauti kubwa ya uwezo wa wachangiaji kwenye mambo ya diplomasia na mahusiano.

Kwanza mtambue hili, sasa hivi watu wanafanya kazi chini chini kuhakikisha hii hali haiendelei.. majasusi wanapanda ndege au tayari wapo Kigali na Kampala kusaidia kuhakikisha hakuna vita. Pili kwa kuwa ni Kenya na Tanzania peke yao ndio stable countries katika ukanda huu, ujue tu kuwa wataubeba huu mzigo wa mashauriano.

Vita ya Uganda na Rwanda HAINA FAIDA YOYOTE KWETU, zaidi sana ni HASARA. Kwanza kukiwa na vita hamna Biashara, bandari zetu na miradi yetu ya miundombinu kwa kiasi kikubwa inategemea sana amani na maendeleo ya biashara katika hizo nchi. Pili wakimbizi, ukiwa unachekelea Ug na Rw kupigana utambue kuwa ni Tanzania ndio itapokea wakimbizi wengi, tegemeeni uhalifu na ujambazi pia kuongezeka... Tatu wao wakiwa hawana amani na sisi pia hatuna amani, hujui ni bomu gani litakosewa likaja kutua Tanzania, ni lazima tutumie rasilimali zetu kulinda mipaka hivyo pesa za miundombinu, hospitali zitaenda kulinda mpaka.. na mengine mengi, bila kusahau masuala ya uhamiaji haramu n.k

So weka mihemko pembeni, ombeni hili jambo lisitokee, vita sio kitu cha kufurahia, sio jambo la kuchekelea.. vita ni damu na hasara, hakuna faida ya vita... uwe unampenda Magufuli au humpendi, ombea sana nchi yako na hekima ya viongozi wetu ili hili jambo liweze kuepukika..

Nahisi pia hili linaweza kuwa ni sababu ya reshuffle ya Foreign Ministry.
 
sasa unaogopa nini mkuu kama ujasusi wamejifunzia Bongo kwa mujibu wa historia zao.
hawawezi kuzinguana hao wanajuana, labda kama kuna kitu kingine wanataka kukitengeneza hapo.
mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…