Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Aidha taarifa hiyo imedhibitisha kuendelea vizuri kwa majadiliano baina ya kampuni ya utengenezaji ndege ya Canada, Bombardier na Airbus ya Ufaransa ili kukodi ndege yanaendelea vyema
"Kufufua shirika la ndege la taifa ni mchakato, hivyo tunatakiwa kuendelea kwa uangalifu na kufuata hatua vizuri lakini naweza kuthibitisha kuwa uamuzi ulifanyika na mipango yetu kwa sasa imefika mahala pazuri
Shirika la ndege la Uganda likarudi tena mwaka ujao", Waziri wa Kazi na Usafirishaji, Aggrey Bagiire ameripoti
Hatua hii ya Uganda inatarajiwa kuwa na athari za moja kwa moja kwa mashirika ya ndege ya nchi za Kenya, Rwanda, Ethiopia na Afrika Kusini, ambazo kwa takribani miaka 15 yalitawala sekta ya usafiri wa anga wa ndani na nje ya Uganda.
Chanzo : The East African