Uganda: Kesi dhidi ya Muhoozi yatupiliwa mbali

Uganda: Kesi dhidi ya Muhoozi yatupiliwa mbali

carbohydates

Senior Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
107
Reaction score
186
Mahakama Kuu ya Kampala nchini Uganda imekataa kutoa wito wa kisheria dhidi ya Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, na wenzake 17 kufuatia kesi iliyofunguliwa na mwanasheria aliyefungwa gerezani, Male Mabirizi.

Mabirizi alitaka viongozi hao wachukuliwe hatua za jinai akidai kuwa uzinduzi na uendeshaji wa vuguvugu la kisiasa la Patriotic League of Uganda (PLU) mnamo Februari 7, 2024, ulikuwa ni kinyume cha sheria kwa kuwa Muhoozi ni afisa wa jeshi anayetumikia jeshi la nchi hiyo (UPDF).

Akitoa uamuzi huo, Jaji Gadenya Paul Wolimbwa alitupilia mbali rufaa ya Mabirizi na kuthibitisha uamuzi wa mahakama ya mwanzo, akieleza kuwa mashtaka hayo yalikosa ushahidi madhubuti na ukweli wa kisheria unaothibitisha makosa ya jinai yanayodaiwa kutendeka.

Jaji alibainisha kuwa mlalamikaji alitoa hitimisho la kijinai bila kuwasilisha vielelezo vinavyohusisha mkutano huo na nia ovu ya kuvunja au kupinga utekelezaji wa sheria.

Aidha, Jaji Wolimbwa alionya dhidi ya dhana ya kulichukulia kundi lolote la kisiasa kuwa ni haramu moja kwa moja kwa sababu tu linaunga mkono nia ya kisiasa ya mwanajeshi anayetumikia jeshi.

Pia alisisitiza kuwa mahakama haina wajibu wa kuagiza polisi wafanye uchunguzi ili kuitengenezea kesi ushahidi pale mlalamikaji binafsi anaposhindwa kuweka vielelezo vya msingi mbele ya sheria.

Chanzo : itv

muhoozi-pic.jpg
​
 
Hapana, Tanzania na Uganga hazichekani kwani zote zinatawaliwa na serikali mbili ambazo hazina ridhaa za wananchi zinazowatawala.

Zikifanyika chaguzi huru na haki katika nchi hizo na serikali hizo zikapata asilimia walau 5 tu basi ziachwe ziendelee kutawala.
 
Hapana, Tanzania na Uganga hazichekani kwani zote zinatawaliwa na serikali mbili ambazo hazina ridhaa za wananchi zinazowatawala.

Zikifanyika chaguzi huru na haki katika nchi hizo na serikali hizo zikapata asilimia walau 5 tu basi ziachwe ziendelee kutawala.
Uganda wamezidi mkuu ,ni mpumbavu pekee ataiweka kwenye mizania sawa Tanzania na Uganda.
 
Back
Top Bottom