Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 7,816
- 16,013
#HABARI:Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF), Muhoozi Kainerugaba, amezua mjadala mkali kimataifa baada ya kutoa kauli kali dhidi ya taifa la Iran kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X Aprili 2, 2026.
Katika ujumbe huo, alitoa onyo la moja kwa moja akiitaka Iran kuomba radhi kwa Uganda ndani ya siku saba.
Kauli hiyo imeibua maswali kuhusu mwelekeo wa uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Uganda na Iran, hasa baada ya Muhoozi kudai kuwa hakuna taifa lolote duniani lenye uwezo wa kuishinda UPDF kijeshi.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanasema matamshi hayo yanaweza kuathiri taswira ya Uganda katika diplomasia ya kikanda na kimataifa.
Mbali na onyo hilo, Muhoozi alidai kuwa vyombo vya usalama vya Uganda vinawashikilia watu aliowataja kuwa ni wapelelezi wa Iran waliokuwa wakifanya shughuli zao nchini humo. Hata hivyo, hakutoa taarifa za kina kuhusu idadi yao, mazingira ya kukamatwa kwao wala ushahidi wa madai hayo.
Hadi sasa, hakuna tamko rasmi kutoka serikali ya Iran kujibu kauli hiyo. Wakati huo huo, wadau wa masuala ya usalama na diplomasia wanaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya tukio hilo na athari zake kwa uhusiano wa mataifa hayo mawili.
Source: ITV Tanzania