Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,193
- 25,504
Chama tawala cha nchini Uganda-NRM wamemtaka Rais Yoweri Kaguta Museveni aongoze hadi kifo. Wamedai kuwa Uganda nzima hakuna anayeweza kuwa Rais isipokuwa Rais Museveni.
Tayari NRM wameanza mchakato wa kutaka marekebisho ya katiba yatakayomuwezesha Rais Museveni kugombea Urais mwaka 2021 ingawa atakuwa amevuka umri unaoruhusiwa kikatiba. Katiba ya Uganda kama ilivyo sasa inataka mgombea asiwe na umri unaozidi miaka 75.
Mwaka 2021,Rais Museveni atakuwa na miaka 76. NRM wamesema umri hauwezi kuwa kikwazo kwakuwa ibara ya katiba itabadilishwa. Wametaka wote wanaopinga jambo hilo wachunguzwe. Hadi sasa,Rais Museveni hakusema chochote kuhusu jambo hilo. Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.
Chanzo: ITV Habari