Uganda: Chama tawala NRM wataka Museven aongoze hadi kifo

Chama tawala cha nchini Uganda-NRM wamemtaka Rais Yoweri Kaguta Museveni aongoze hadi kifo. Wamedai kuwa Uganda nzima hakuna anayeweza kuwa Rais isipokuwa Rais Museveni.

Tayari NRM wameanza mchakato wa kutaka marekebisho ya katiba yatakayomuwezesha Rais Museveni kugombea Urais mwaka 2021 ingawa atakuwa amevuka umri unaoruhusiwa kikatiba. Katiba ya Uganda kama ilivyo sasa inataka mgombea asiwe na umri unaozidi miaka 75.

Mwaka 2021,Rais Museveni atakuwa na miaka 76. NRM wamesema umri hauwezi kuwa kikwazo kwakuwa ibara ya katiba itabadilishwa. Wametaka wote wanaopinga jambo hilo wachunguzwe. Hadi sasa,Rais Museveni hakusema chochote kuhusu jambo hilo. Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Chanzo: ITV Habari

ndo tunavyoiga kwa wenzetu hivi
 
Madikteta ndivyo walivyo! Na hapa nyumbani napo wale ZERO BRAINS nao wameshaanza kumpigia debe fisadi, mwizi na dikteta uchwara eti atawale milele! Sijui kwa lipi hasa! Kweli mtaji wa wahuni na mafisadi ni wale waliopitia shule za kata na wenye uwezo finyu wa kuchanganua mambo kwa kina.
Hizo ndizo sifa za Madikteta uchwara kama huyu wa kwetu...kwao wizi rukhsa, upinzani marufuku, ukabila rukhsa, haki marufuku, uonevu na unyanyasaji rukhsa, hekima marufuku, ukurupukaji na uropokaji rukhsa...kwao katiba si chochote si lolote, ni kipande tu cha karatasi.
 
Nawasikitikia waganda, Mseveni ndo kisha chukua hivyo term nyingine. Ni umugabe mpaka anakufa. Kuna la kujifunza pia. wanachama wa chama cha NRM wanataka kubadilisha katiba ili Mseveni agombee urais mpaka kufa, mhusika mkuu ambaye ni Mseveni yuko kimya.

Habari za rais wetu kuongezewa muda zimeshaanza na hata hata miaka 2 haijafika, kelele hizi zitazidi kuongezeka hasa awamu ya pili, ungetarajia rais muungwana awakemee watu hawa ili hili jambo lisiwakae akilin. Kama Kagame, mwanzoni wanakuwa kimya, mwishoni wanasema wao wanafuata matakwa ya wananchi.
Mzee Mwinyi & Company. Maumivu huanza kidogo dogo. Mola atuepushe na kikombe hiki!!!!
 
Back
Top Bottom